Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Dk. Wilbrod Slaa wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chama cha CHADEMA,Marehemu  Bob Makani, leo kwenye Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akikumbatiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Dk. Wilbrod Slaa wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chama cha CHADEMA,Marehemu  Bob Makani, leo kwenye Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Nape akimsalimi Hajjat Shida Salum, Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kwenye msiba huo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimpa pole Mbunge wa Rombo,Mh. Joseph Selasini, wodini, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Selasini amehamishiwa Muhimbili kutoka KCMC, kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mkono alioumia katika ajali aliyopata hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita. (Picha na Bashir Nkoromo wa Daily Nkoromo Blog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...