Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na walimu wa shule za sekondari na za msingi mjini Mafinga mkoani Iringa, leo katika ukumbi wa Southern Highland, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama tawala cha CCM mkoani humo. Katika mazungumzo hayo Nape alipata fursa ya kusikiliza kero za walimu na kujadili nao jinsi ambavyo serikali itakavyoweza kuyatatua.
Walimu wa shule za sekondari na msingi wa mjini Mafinga, wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipozungumza nao leo kwenye ukumbi wa Southern Highland mjini Mafinga mkoani Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MliakuvanaJune 16, 2012

    Southern Highlands School: http://www.southernhighlands.ac.tz/

    Inaonekana baridi imepamba moto! Manake kila mmoja ametinga koti au sweater!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2012

    Viongozi wa CCM unganeni na Nape katika kufanya kazi ya Chama .....chama bado imara na kinawanachama wengi hivyo ni wajibu wa viongozi kuitumikia nchi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2012

    Ndiyo bwana, manake wanakuwa kama wamemwachia Nape peke yake. Tukisema viongozi wetu wanakitosa chama, wanapiga kelele. Nauliza, hasa ninyi wajumbe wa Sekretariet ambao siyo viongozi pia serikalini, mbona mnamwachia Nape kazi yote? I would expect that you'd meet once a month, asses the party performance (among masses), coin a strong msg (ili mfanane, pia kwa malengo mtakayojiwekea mwezi huo - for the particular 'zone' you will visit, siyo kila mtu anasema lake au mbaya zaidi - mnapingana ama hata kurumbana!)
    Jamani eh, BILA CCM IMARA, NCHI ITAYUMBA. Huo ndiyo ukweli wenyewe.
    Mwanachama wa CCM, Italy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...