Kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali katika maisha, leo benki ya NMB imezindua promosheni iitwayo jenga maisha yako na NMB itakayomwezesha mteja wake kuingia kwenye droo na kushinda tani ya saruji, mabati ya kuwezeka, amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano Bw. Imani Kajula amesema “wateja wengi wanaweka amana ili kutimiza malengo mbalimbali na ndio maana, benki ya NMB imezindua promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB itakayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye akaunti zao za NMB Bonus Account au NMB Junior Account kupata riba ya kuvutia hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana kilichowekwa” .

Kupitia droo ambazo zitachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo, sio tu zitawaongezea watanzania tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea..

Fungua NMB Bonus Account au NMB Junior Account leo na ushinde!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...