Meneja wa kitengo cha uchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Mwanaidi Mahiza akitoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa karatasi za madodoso ya Sensa ya watu na makazi 2012 kwa waratibu wa Sensa kutoka mikoa na wilaya zote nchini katika mafunzo ya awali yanayoendelea mjini Morogoro.
Waratibu wa Sensa ya watu na makazi wakipitia moja ya dodoso litakalotumika wakati wa Sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka huu na kujifunza namna sahihi ya kuweka vivuli/ alama wakati wa kukusanya taarifa za kaya.
Waratibu wa Sensa ya watu na Makazi 2012 kutoka katika mikoa na wilaya zote nchini wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Morogoro. Katika mkutano huo wa mafunzo mambo mbalimbali yanajadiliwa yakiwemo masuala ya Bajeti, Ushiriki wa Viongozi katika Zozi la Sensa, Utunzaji na ujazaji wa madodoso wakati wa Sensa, namna ya kuwapata makarani wa Sensa na vitendea kazi.
Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bara na ile ya Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,viongozi wa mkoa wa Morogoro na waratibu wa Sensa ya watu na makazi 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Alphayo Kidata (mstari wa kwanza katikati)mjini Morogoro.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    Hivi kweli Serikali ina nia ya dhati ya kuepukana na tatizo la ajira kwa vijana wetu? Kwa nini zoezi zima la sensa haliwashirikishi vijana waliohitimu UDSM, EA Statistical centre? sina uhakika kama kuna wahitimu wa UDOM. Watoto wa watu wamesota sana chuoni kwani takwimu ni somo gumu sana, lakini wamezagaa mjini wanahangaika hapa na pale, hasa ukizingatia kuwa mwajiri wao mkuu ni Serkali. Matokeo yake kazi zao wanapewa vigogo kama wabunge na hawa waratibu. Kwa nini fursa kama hizi wasipewe watu walihitimu katika hii fani? kwanza ni wachache mno. Hawafiki hata mia moja. Nina shaka na "rate of accuracy ya sensa ya mwaka huu!!!" Ni aibu sana, tuna wataalamu ila hatujui jinsi ya kuwatumia. Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Hakuna sababu ya kuvunja Muungano, kwa kuwa Takwimu zitaweka bayana kila kitu na hao wanaolalamika kuwa Mapato ya Visiwani yanaliwa na Bara itafikia tamati sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...