Watoto wa mitaani wakiwa wamesimama kwenye moja ya gari lililokuwa linalosubiria ruhusa ya taa za kuongozea magari katika makutanao ya barabara ya Kawawa na Morogoro Rodi,Magomeni Mapipa mapema leo.Ongezeko la watoto wa Mitaani limekuwa likiongezeka siku hadi siku, pamoja na kuongezeka kwa vituo vya kulelea watoto yatima lakini bado Watoto hawa nao wanazidi Mitaani mithili ya kwamba hakuna vituo hivyo.
Watoto hao baada ya kuwa wamemaliza kuomba kwenye gari iliyokuwepo mbele.hivi ni nani wa kulaumiwa katika hili jamani??
This is a monumental problem
ReplyDeleteHawa watoto wa mitaani, sasa ni watoto, lakini miaka kumi hivi ijayo watakuwa wamehitimu kutoka chuo kikuu cha CRIME.Wengi hayawahusu kwa sababu miaka kumi ijayo, matatizo hayo hayatakuwa si yao.Nionavyo mimi serikali ingeanzisha idara maalumu na kamishina wa watoto atakayekuwa na madaraka ya kuwalea watoto hawa,preferably away from the big cities. Wapewe elimu na wafundishwe uraira na job skills.Sasa wanaomba kwa kelele na kero, kesho wataomba na bastola mikononi.
Jamii nzima yastahili kulaumiwa.
ReplyDeleteKimsingi hili tatizo linatokana na kukosa nidhamu(discipline)
Kama kinamama wangekuwa na nidhamu,kina baba pia,vijana wa kike na kiume hawa watoto wasingezaliwa hovyo,bali rasmi na kusingekuwepo na msongamano huu.
Si mnajionea wenyewe watoto waliozaliwa kwenye familia zenye nidhamu wanavyolelewa vema?
Lakini lipo swala zima la kufundisha watu wetu ambalo kwa asilimia kubwas ni wajibu wa serikial;i.
Nayo naibebesha zigo la lawama.Tunao viongozi wengi ambao nao ni chanzo cha zaa zaa hovyo.Rejea kurupushani za kuumbuana kwenye vinynganyiro vya kisiasda.
Yaani huwa sielewagi kabisa kazi za wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Watoto wanazagaa kila kona za mitaa kila siku, sasa watoto wanotajwa katika wizara hii sijui ni wakimarekani au hawajzaliwa bado?
ReplyDeleteEmbu tuelewesheni wananchi kazi hasa za hii wizara, na wajibu wao kwa jamii.
Kibanga Msese
hayo matatizo ni dunia nzima sio tanzania tu, lakini nchi za wenzetu wameweza kuyazibiti, kwa mfumo ambao umewekwa kwa ajili ya kutatua sekeseke kama hizi. Serekali ina provide kila aina ya msaada kwa viumbe kaka hawa sasa sielewi CCM ina mpango gani kama chama tawala. WIZARA YA USTAWI WA JAMII ILIKUFA ? kama bado ipo basi hio ndio kazi yao kama sijakosea. NA NI KWELI LEO WANAOMBA KWA KELELE saidia nikale ! Kesho wataomba na bastola mbele.
ReplyDelete