Watoto wa mitaani wakiwa wamesimama kwenye moja ya gari lililokuwa linalosubiria ruhusa ya taa za kuongozea magari katika makutanao ya barabara ya Kawawa na Morogoro Rodi,Magomeni Mapipa mapema leo.Ongezeko la watoto wa Mitaani limekuwa likiongezeka siku hadi siku, pamoja na kuongezeka kwa vituo vya kulelea watoto yatima lakini bado Watoto hawa nao wanazidi Mitaani mithili ya kwamba hakuna vituo hivyo. 
Watoto hao baada ya kuwa wamemaliza kuomba kwenye gari iliyokuwepo mbele.hivi ni nani wa kulaumiwa katika hili jamani??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    This is a monumental problem
    Hawa watoto wa mitaani, sasa ni watoto, lakini miaka kumi hivi ijayo watakuwa wamehitimu kutoka chuo kikuu cha CRIME.Wengi hayawahusu kwa sababu miaka kumi ijayo, matatizo hayo hayatakuwa si yao.Nionavyo mimi serikali ingeanzisha idara maalumu na kamishina wa watoto atakayekuwa na madaraka ya kuwalea watoto hawa,preferably away from the big cities. Wapewe elimu na wafundishwe uraira na job skills.Sasa wanaomba kwa kelele na kero, kesho wataomba na bastola mikononi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Jamii nzima yastahili kulaumiwa.
    Kimsingi hili tatizo linatokana na kukosa nidhamu(discipline)
    Kama kinamama wangekuwa na nidhamu,kina baba pia,vijana wa kike na kiume hawa watoto wasingezaliwa hovyo,bali rasmi na kusingekuwepo na msongamano huu.
    Si mnajionea wenyewe watoto waliozaliwa kwenye familia zenye nidhamu wanavyolelewa vema?
    Lakini lipo swala zima la kufundisha watu wetu ambalo kwa asilimia kubwas ni wajibu wa serikial;i.
    Nayo naibebesha zigo la lawama.Tunao viongozi wengi ambao nao ni chanzo cha zaa zaa hovyo.Rejea kurupushani za kuumbuana kwenye vinynganyiro vya kisiasda.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    Yaani huwa sielewagi kabisa kazi za wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Watoto wanazagaa kila kona za mitaa kila siku, sasa watoto wanotajwa katika wizara hii sijui ni wakimarekani au hawajzaliwa bado?

    Embu tuelewesheni wananchi kazi hasa za hii wizara, na wajibu wao kwa jamii.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    hayo matatizo ni dunia nzima sio tanzania tu, lakini nchi za wenzetu wameweza kuyazibiti, kwa mfumo ambao umewekwa kwa ajili ya kutatua sekeseke kama hizi. Serekali ina provide kila aina ya msaada kwa viumbe kaka hawa sasa sielewi CCM ina mpango gani kama chama tawala. WIZARA YA USTAWI WA JAMII ILIKUFA ? kama bado ipo basi hio ndio kazi yao kama sijakosea. NA NI KWELI LEO WANAOMBA KWA KELELE saidia nikale ! Kesho wataomba na bastola mbele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...