Home
Unlabelled
Rais Kikwete na Mama Salma Wakagua mahindi Shambani kwao kijijini Msoga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mmeona mafunzo kwa Vitendo?
ReplyDeleteEnyi Mafisadi na wezi mtumie nafasi hii kama mafunzo kutoka kwa Kiongozi wetu!
Mtu mzima hasomeshwi hufunzwa kwa vitendo!
Mhe. Raisi JK anajaribu kuwapa mwamko ya kuwa hata Kilimo na shughuli halali za uzalishaji ndio mtindo sahihi wa maisha badala ya WIZI ,UFISADI NA UBADHIRIFU!
MANAGEMENT SCIENCE /SAYANSI YA UENDESHAJI:
Inatueleza ya kuwa mwenendo wa mtu hutokana na hulka na pia hulka hutokea kuwa maradhi.
Mfano mtu mwizi anakuwa amepata maradhi na kamwe hawezi kuendesha shughuli zingine za kawaida za uzalishaji na kujiingizia kipato!,,,NDIO MAANA FISADI ANAWEZA KUIBA HADI SHS. 1 BILIONI LAKINI UKAJA KUTA BAADA YA MUDA FULANI BAADAE HANA HATA SHILINGI MOJA AMEFILISIKA!!!
SAAFI SAANA DK. KIKWETE, NIMEIPENDA HII, KAMA OBAMA NA MKEWE WANAVYOTOKA PAMOJA, HII IMETULIA NASI TUTAIGA MFANO WA KUTOKA PAMOJA, MAANA WATANZANIA WENGI BADO HATUPENDI KUONGOZANA NA WAUME NA WAKE ZETU, SAAAFI SANA.
ReplyDeleteSafi sana JK, inafurahisha hakika. Inatakiwa shamba lako liwe shamba darasa!
ReplyDeleteHaya Wananchi mnaelekezwa muachane na Wizi na Ufisadi mrudi kwenye Kilimo kwanza!
ReplyDeleteHapo sasa Rais wetu anaonyesha kwa vitendo juu ya kuipa sekta ya kilimo kwanza kipau mbele,sisi wananchi tunatakiwa kuiga mfano,basi hata kama huna ardhi ya kulima shamba au huna pesa nyingi za kugharamia shamba kubwa basi hapo ulipo hata kama unapanga chumba kimoja badala ya kuweka kopo la mua kata makali ya maisha pandikiza mboga za majani kama sukuma wiki kwenye mkebe,mboga hiyo kila ukichuma inachipua tena majani mboga mapya hivyo hutakosa mboga na pia unauhakika wa kula mboga safi ambazo ziko kwenye mazingira safi,ukipanda miche mitano kwenye mikebe mitano tosha kabisa kwa matumizi wakati wowote.Tuzingatie kilimo,bila kula maisha hayapo,huo ndio ukweli wenyewe,hongera sana rais wetu.
ReplyDeleteMuheshimiwa kanikuna kwelikweli yaani hilo nifundisho kubwa kwa watanzania waliojaliwa neema ya ardhi na wenye uwezo wa kupanda zao lolote likakubali, jamani watanzania wenzangu MSIWE WAVIVU WA KUFIKIRI NA KUJITUMA mnabaki hoo mfumuko wa bei wakati mtu unanguvu zako na unaweza kujilimia mbogamboga kwa wingi na ukapata chakula bora kabisa na ziada ukauza. Haya sasa mkuu huyoo anawaonyesha kwa vitendo na wengine kazi yenu kushinda kwenye mabaa na manight club MNANIKERA SANA NYINYI WENYE TABIA YA UVIVU NA KULALAMIKALALAMIKA BILA MPANGO, AKILI MNAZO HAMTAKI TU KUZITUMIA TUBADILIKE WATANZANIA MWEEEEH!
ReplyDeleteI am soooooo proud of you, your Excellence!!! Inapendeza sana. Just imagine, kama Baraza lote la Mawaziri wangekuwa na mashamba kama Mheshimiwa Rais.......kwa kweli hata wananchi wangekithamini sana Kilimo, tofauti na hali ilivyo sasa. Hongera sana JK na Mama Salma. Big up your Excellence !!!
ReplyDeletetuige mfano wa maraisi wetu,Mwl Nyerere alikuwa na mashamba na mifugo mpaka sasa,tucheki juzi mkapa ana mashamba ya nyasi mpaka ya mifugo na tulishuhudia juzi alipotoa ng'ombe wa2 kwa ajili ya kitoweo,haya huyu nae kikwete ana shamba,ndio tukae na kujifunza jamani huku kwenye kilimo ndio kwenyewe kwa kuwekeza...
ReplyDeleteyaani nyie! mlitegemea kweli rais wetu asiwe na shamba, mawaziri nao wanayo mashamba ya kutosha na ardhi kubwa ya kuwatosha, wananchi wengi wanaatamani kilimo lkn hakuna ardhi, ardhi zimekaliwa na vigogo. Raisi wetu asante kwa picha hii imenikumbusha machungu mengi.
ReplyDelete