Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Mohamed Abdelaziz wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi leo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini Tanzania.
Rais Abdelaziz akiagana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama
Kwa heri ya kuonana
Safari njema....






Muandishi acha kupotosha fanya uchunguzi wa kina kabla hujaandika.Nchi uliyo itaja haitwi SARHAWI bali inaitwa SAHRAWI au SAHRAOUI ni neno la Kiarabu maana yake ni kutoka SAHARA haswa WESTERN SAHARA[Jangwa la Sahara Magharib].
ReplyDeleteUkiwa Rais bwana, yaani unaweza kusafiri kwenda nchi nyingine kuangalia picha za ukutani tu kisha unageuka.
ReplyDeleteunonymous. 2, nadhani uelewa wako ni mdogo sana, kuna safari za viongozi za aina vyingi, ziara hii ilikuwa ya mazungumzo kati ya Mhe. JK na Mhe. Abdulaziz ya ana kwa ana, kuna mambo mengine ili kuongeza uzito wahusika wamalazimika kuonana badala ya kupigiana simu, hiyo ni aina moja ya safari za Viongozi, mfano marais wa nchi za EAC wamekuwa wakija Ikulu mara kwa mara mchana wanafanya mazungumzo na Mhe. JK kisha jioni wanarudi kwao. Kwa ufafanuzi zaidi ingia katika tovuti ya Chuo cha Diplomasia au Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
ReplyDelete