Mgeni rasmi Bw. Mosess Mwidete (DAS Wilaya ya Rungwe) akijitayarisha kukabidhiwa kombe.
Aslaam aleikhum Mjomba Issa Michuzi.
Sherehe za kukabidhi kombe kwa wanachama wa Laxmi Darts Club – Wanyambala zimefanyika mjini Tukuyu siku ya Jumapili 10/06/2012 na kufana sana. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mosses Mwidete ambaye ni DAS wa Wilaya ya Rungwe.
Katika hotuba yake aliipongeza sana timu ya Darts Tukuyu kwa kutwaa Kombe la Taifa la Darts kwa upande wa kinamama katika mashindano yaliyofanyika Mjini Morogoro hivi karibuni.
Aidha Mwidete aliipongeza Laxmi Darts Club kwa juhudi zao za kukuza michezo Wilaya ya Rungwe, kwani michezo ni furaha, inajenga afya bora na pia kudumisha mahusiano mazuri katika jamii, pia aliwataka Vijana kushiriki katika michezo mbali mbali ili kujiepusha na mambo ambayo hayakubaliki katika jamii ikiwa ni pamoja na uvutaji bangi vijiweni, madawa ya kulevya na pengine michezo itawaepusha Vijana katika
kujiingiza kwenye ngono sisizo salama na hatimaye kupata UKIMWI na hata kujiingiza katika Ujambazi.
Naye Mlezi wa Laxmi Darts Club Bw. Robert Shedafa alipotakiwa kutoa neno la shukurani, alimshukuru mgeni rasmi kwa kukubali mwaliko wa kuja kulipokea Kombe na kushiriki na wanachama kusherehekea.
Pia alihimiza vijana kushiriki katika michezo kwani michezo inaweza kuwaletea ajira.
Kwa ujumla sherehe hizi zilifana sana kama inavyoonekena kwenye picha zilizochukuliwa seheme ya tukio.
Habari na picha ni Mjomba Juma wa Tokyo, Mbeya.
Wanachama wakisherehekea.
Sherehe ilifana sana, wanachama wa Laxmi Darts wakiburudika.
Kumbe Darts mchezo mzuri sana ni kunywa na kula mapocho tuuu............
ReplyDelete