FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ALI OTHAMAN ARABA WA TANGI BOVU, MBEZI BEACH, TUNATOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWA WATU WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KWA HALI NA MALI KATIKA MSIBA WA MPENDWA WETU MKAMBA ALI OTHMAN ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 4 MAY 2012 KATIKA HOSPITAL YA TAIFA YA MUHIMBILI NA KUZIKWA TAREHE 6 MAY 2012 NYUMBANI KWAO MAKANYA WILAYA SAME, MKOA WA KILIMANJARO.

SI RAHISI KUTAJA MAJINA YA WOTE WALIOTUFARIJI NA WANAONDELEA KUTUFARIJI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA WA MPENDWA WETU SHUKRANI ZETU ZIWAEENDE NDUGU WOTE UPANDE WA BABA NA MAMA, MAJIRANI WOTE WA TANGI BOVU NA MAKANYA, MARAFIKI WOTE WA MAREHEMU MKAMBA PAMOJA NA WAFAMILIA..TUNAWASHUKURU KWA UPENDO NA UKARIMU MLIOTUONYESHA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA KUUGUZA NA MSIBA WA MPENDWA WETU NA MWENYEZI MUNGU ATAWALIPA YALIYO MEMA.

PIA TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA AROBAINI YA MPENDWA ETU MKAMBA ALI OTHMAN ITAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI TAREHE10 JUNE 2012 MAJIRA YA SAA TANO ASUBUHI NYUMBANI KWAO TANGI BOVU, MBEZI BEACH DAR ES SALAAM.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEEN
INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJI’UN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    mwenyezi mungu amjaalie amsamehe mja wake huyu makosa yake na ampe malazi pema peponi amin,

    na awape nguvu wafiwa wote katika kipindi hichi kigumu kwao mwenyezi mungu awapeni wepesi amin

    kutoka pemba

    ReplyDelete
  2. Na muwe pole wafiwa, Mwenyez Mungu awape nguvu, subira na faraja khususan katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Mwenyeez Mungu amraham mja wake huyu, amughufirie kwa yote na amjaaliye Jan'natu N'naeem - AMEEN. "IN'NA-LIL'LAHI-WAIN'NA-ILAY'HI-RAJIUN"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...