Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu.

Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.

Licha ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

“Tunaiheshimu Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.

Kikosi cha Stars kinaongozwa na nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris. Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.

Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.

Mbali ya Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Msafara wa Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2012

    Ankal naomba nitoe comments off-topic hapa. Kwenye stori ya Hasheem Thabeet (undoubtedly the most successful Tanzanian sports 'export' and by far the richest {God bless and protect him}), kuna mdau anayejiita Che Guevara (what a fake!) amedai eti kuwa Hasheem anachezea timu ya 'mchangani'. Ukweli ni kuwa Brother Hasheem anachezea Portland Trail Blazers (one of the elite NBA teams in USA)na mshahara wake wa mwaka mmoja tu unaweza kuwanunulia huyo Che uchwara wazazi wake, ndugu zake na wajukuu wao nyumba 10 za kifahari (at 500,000 US Dollars a house). Watanzania wacheni tabia za wivu na kuwachukia watu waliofanikiwa. Tuwaige watu waliofanikiwa wawe chachu (inspiration) kwetu. Huko UK wanasema "Don't quarrel with success" ha ha ha ...long live Hasheem and keep up the good work dude! Baba wa Kambo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    Kila lakheri Simba na Aden Rage!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    Ankal tusaidie sisi watu wa ughabuni vipi tutaweza kuziangalia match za Taifa stars live? Kama kuna Mtu anajua hebu tuelekezeni vipi tufanye kwa Internet or satellite ahsante.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2012

    namsikitikia KIM ameanza vibaya tayari, pumzi za nguvu uwanjani hazipo(Haruna moshi, Cholo, Nurdin) sijui hao waliobaki sijui watapumua vipi uwanjani, afadhali angewaita Shindika, Machupa na Nizar akazugazuga nao kidogo. Haya ndio mpira wetu bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...