Taarifa hii inahusu matatizo ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza nchini Algeria kutoka Tanzania kutokana na kutokupata pesa zao za mkopo kutoka bodi ya mikopo Tanzania. Tunakuomba utusaidie kupitia blog yako kutu chapishia taarifa hiyo ili  watutumie pesa hizo haraka sana.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    Poleni jamani..du shule ilivyo ngumu halafu mfukoni tena kuwe kutupu hatari tupu. Halafu serikali yetu jamani mbona kila kona inadaiwa...wanafunzi, walimu, wazee,bado deni la taifa mh tuache utani lazima hatua za haraka zichukuliwe la sivyo tuendako huko si kuzuri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Nyie vijana hali ikiendelea kuwa ngumu nendeni ubalozini kwetu hapo Algiers.Nilienda kulipa mkopo hapo kwenye tume.Nilikuta vijana wengi tu waliomaliza vyuo vikuu ndiyo wanafanya kazi hapo,nilitegemea watakuwa sharp kuwaisha pesa kwa wengine wanaozihitaji.Pesa tunazorudisha ni nyingi nilikuta Likitabu limejaa wanaorudisha mikopo..Please pesa za mikopo zisifanye kazi nyingine tofauti na lengo, zizunguke kwa Wanafunzi wengine.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Serikali ijitahidi kuweka mipango mizuri ya jinsi ya kurudisha fedha ya mikopo. Kuna kijana ana kazi nzuri tu, alisoma kwa mkopo. Amini usiamini anazungushwa kila anapoulizia afanyeje ili akatwe mshahara wake kila mwezi kulipia deni lake. Inasikitisha, maana fedha inatoka tu na hairudi ndio maana mfuko wa mikopo unaishiwa. Utaratibu mbovu, ni kuifilisi tu serikali.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2012

    mtakoma, kasomeni nyumbani kwani serikali yetu siinajulikana?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2012

    EEeh. Nyie vijana; shule mnaitafuta hadi Algeria. Nimemkumbuka mama mmoja alonambia hata Bhutan (kwenye Growth National Happiness) Watanzania wapoooo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2012

    kwanza poleni, pili-matatizo yenu yanahitaji msaada wa haraka.tatu- ni vizuri mkaanza na ubalozini-hapo mlipo algeria, kuliko njia ya mambo hadharani.sidhani kama mzazi wako akichacha unamtangaza gazetini.akili kumchwa - jifunzeni akili za mbayuwayu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2012

    Mbona ninyi mnakuwa watoto wa mama kivile ,siku tano tu ela zimechelewa mnalalamika.Pigeni BOX acheni usharobaroh!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2012

    wewe unayesema usharobaro hela zimechelewa miezi 2 na ni uzembe wa bodi ya mikopo na umoja wa wanafunzi ATSA acha kutetea ujinga

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2012

    Why Algeria? Jamani wabongo jaribuni kutafuta scholarship za maana, msiende hizi nchi za magaidi jamani, for what?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2012

    wewe nawe unae sema nchi za ugaidi umefika lini, mbona mnapondea mambo msio elewa jamani, scholarship za maana, nani kakwambia hiii sioo.. acha kupondea vitu usivyo jua undani wake..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...