| Taarifa hii inahusu matatizo ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza nchini Algeria kutoka Tanzania kutokana na kutokupata pesa zao za mkopo kutoka bodi ya mikopo Tanzania. Tunakuomba utusaidie kupitia blog yako kutu chapishia taarifa hiyo ili watutumie pesa hizo haraka sana. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA |
Home
Unlabelled
TAARIFA KUTOKA KWA WANAFUNZI NCHINI ALGERIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Poleni jamani..du shule ilivyo ngumu halafu mfukoni tena kuwe kutupu hatari tupu. Halafu serikali yetu jamani mbona kila kona inadaiwa...wanafunzi, walimu, wazee,bado deni la taifa mh tuache utani lazima hatua za haraka zichukuliwe la sivyo tuendako huko si kuzuri.
ReplyDeleteNyie vijana hali ikiendelea kuwa ngumu nendeni ubalozini kwetu hapo Algiers.Nilienda kulipa mkopo hapo kwenye tume.Nilikuta vijana wengi tu waliomaliza vyuo vikuu ndiyo wanafanya kazi hapo,nilitegemea watakuwa sharp kuwaisha pesa kwa wengine wanaozihitaji.Pesa tunazorudisha ni nyingi nilikuta Likitabu limejaa wanaorudisha mikopo..Please pesa za mikopo zisifanye kazi nyingine tofauti na lengo, zizunguke kwa Wanafunzi wengine.
ReplyDeleteDavid V
Serikali ijitahidi kuweka mipango mizuri ya jinsi ya kurudisha fedha ya mikopo. Kuna kijana ana kazi nzuri tu, alisoma kwa mkopo. Amini usiamini anazungushwa kila anapoulizia afanyeje ili akatwe mshahara wake kila mwezi kulipia deni lake. Inasikitisha, maana fedha inatoka tu na hairudi ndio maana mfuko wa mikopo unaishiwa. Utaratibu mbovu, ni kuifilisi tu serikali.
ReplyDeletemtakoma, kasomeni nyumbani kwani serikali yetu siinajulikana?
ReplyDeleteEEeh. Nyie vijana; shule mnaitafuta hadi Algeria. Nimemkumbuka mama mmoja alonambia hata Bhutan (kwenye Growth National Happiness) Watanzania wapoooo.
ReplyDeletekwanza poleni, pili-matatizo yenu yanahitaji msaada wa haraka.tatu- ni vizuri mkaanza na ubalozini-hapo mlipo algeria, kuliko njia ya mambo hadharani.sidhani kama mzazi wako akichacha unamtangaza gazetini.akili kumchwa - jifunzeni akili za mbayuwayu.
ReplyDeleteMbona ninyi mnakuwa watoto wa mama kivile ,siku tano tu ela zimechelewa mnalalamika.Pigeni BOX acheni usharobaroh!
ReplyDeletewewe unayesema usharobaro hela zimechelewa miezi 2 na ni uzembe wa bodi ya mikopo na umoja wa wanafunzi ATSA acha kutetea ujinga
ReplyDeleteWhy Algeria? Jamani wabongo jaribuni kutafuta scholarship za maana, msiende hizi nchi za magaidi jamani, for what?
ReplyDeletewewe nawe unae sema nchi za ugaidi umefika lini, mbona mnapondea mambo msio elewa jamani, scholarship za maana, nani kakwambia hiii sioo.. acha kupondea vitu usivyo jua undani wake..
ReplyDelete