Taifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.
Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen imefikia Hotel 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...