Baada ya kibali cha kuwazika nchini Tanzania wahamiaji toka Ethiopia waliofariki ndani ya lorry walilokuwa wanasafiria kutolewa na Serikali yao ya Ethiopia, Serikali ya Tanzania iliamua mazishi ya Raia hao wa Ethiopia kufanyika Juni 29, 2012 Alasiri Mkoani Dodoma na Morogoro kwa baadhi ya miili iliyokuwa imehifadhiwa hospitali ya Mkoa Morogoro na kazi inayoendelea hapa ni ya uchimbaji wa makaburi.
Vijana 84 wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakipita mmoja baada ya mwingine wakitoa heshima zao za mwisho na kuwaaga ndugu zao kwa kutupa udongo kwenye makaburi yaliyohifadhi miili ya wenzao waliopoteza maisha katika tukio la kusafirishwa kwenye Lorry.
Kijana Chafamo Yosef (kulia) Muamiaji raia wa Ethiopia akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi kwa jinsi ambavyo wamepatiwa msaada na serikali ya Tanzania tangu siku walipokutwa wametelekezwa, miongoni mwa vitu alivyoahidi akifika nchini kwao Ethiopia ni kuwaelezea watu wa Ethiopia kuwa walidanganywa na kusababishiwa matatizo makubwa hadi baadhi yao kupoteza maisha lakini wao Mungu amewanusuru, wameona nchi nzuri ya Tanzania, wamekutana na serikali nzuri iliyowahudumia kila kitu, na wananchi wenye mioyo ya huruma na ukarimu.
Raia wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kuwaombea sala wenzao waliopoteza maisha wakati wa shughuli ya mazishi.
Safari ya mwisho ya kuwasindikiza na kuwahifadhi katika nyumba zao za milele wahamiaji 43 (21 Dodoma, 23 Morogoro) kutoka Ethiopia waliopoteza Maisha ilihitimishwa kwa kazi ya kufukia makaburi iliyofanywa na vijana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mazishi hayo.
Wahamiaji hawa (walionusurika) wamekuwa watu waliozamia katika sala na maombi baada ya kunusurika kifo ukizingatia baadhi ya wenzao walikufa katika tukio hilo, kila baada ya chakula jioni wanapewa muda wa kufanya maombi.
Wahamiaji kutoka Ethiopia walipatiwa kila aina ya msaada wa muhimu uliohitajika kwa wakati kama malazi, mavazi, chakula dawa, matibabu ya kisaikolojia nk
Mtoa huduma ya kwanza wa Msalaba Mwekundu akimfunika mmoja wa wahamiaji kutoka Ethiopia ambaye alikuwa na tatizo la maumivu kifuani.
Mabaki ya vitu, miongoni mwake chupa za maji zikiwa nyingi na vifurushi vya sukari na mikate ambavyo walikuwa wanatumia wahamiaji hao kama chakula kwa ajili ya kujinusuru uhai wakiwa ndani ya lorry lililowasafirisha likiwa limefunwa pande zote bila kuruhusu hewa kupita, masalia haya badae yaliteketezwa moto.
Vijana walioandaliwa kwa ajili ya shughuli ya Mazishi wakishusha miili ya Marehemu kwenye nyumba zao za milele (makaburi) ikiwa ni hatua za mwisho za kuhitimisha safari ya mwisho ya kuwapumzisha watu hao waliopoteza maisha.
Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakilia kwa uchungu muda mfupi baada ya miili ya Wenzao waliopoteza maisha kuwasili eneo la maziko mjini Dodoma, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro.
Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wamejipanga mistari miwili wakionekana wenye huzuni muda mfupi baada ya kuwasili eneo lililoandaliwa katika Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuwazika wenzao waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro. Picha zote na Jery Mwakyoma



Mimi nasema na sisi watanzania tuache kuwa wakatili hawa jamaa hawataki kuhamia hapa wanapita njia tu. Kwa nini msiwe mnawaacha wapite zao badala ya kuwakamata kila mara mpaka wanafikia hatua ya kufungiwa kwenye kontena lisilo na hewa.
ReplyDeleteHawa jamaa siyo watu wabaya ni wapita njia wanatafuta maisha walishe familia zao na kusomesha watoto.
Mbona kenya imewaacha wakapita na sisi tuwaache wapite waende huko south africa.
Tuwe na roho za kumwogopa Mungu na kuwatendea wengine kama ambavyo tungependa kutendewa sisi wenyewe
Matatizo ya mipaka ya wakoloni.
ReplyDeleteOne Afrika, one people and all these problems will disappear
Kwakweli inasikitisha sana jamani wanatia huruma.Haya sio maisha ya kuishi mtu kuikimbia nchi yako na kwenda kutafuta maisha bora kwingine.Serikali za kiafrika hazina huruma hazina maarifa yoyote ya kuwatafutia vijana ajira na kujiwezesha kimaisha.Wameaga kwenda kutafuta maisha ili wajiwezeshe pamoja na kuwasaidia familia zao lakini wameishia kuzikwa na watu baki bila hata familia kutoa heshima zao za mwisho.Hili ni somo tosha kwa viongozi wetu walifikirie sana na mungu awasamehe hukowaliko na awape pepo.
ReplyDeletemimi sijaelewa: walifungiwa kwa nguvu humo kwenye hilo lori, kama ni hivyo na nani? ama walikubaliana wakalipa na hela? nipo nyuma ya wakati jamani msinipige vijembe nielimisheni kwanza ili niweze kuchangia!!! fanyeni haraka nina hasira sana na damu iliyomwagika bure
ReplyDeleteONE US$ !
ReplyDeleteONE US$ !
ONE US$ !
Hehehe picha ya kwanza juu, ina maana huo wa hizo moja moja ndio ushahidi au ndio kusema zingine 'zimekwisha hifahdiwa'?
Jamani zingine (100's US$ na 50's US$ ziko wapi ?
Bandugu !
ReplyDeleteEnhhe hivi unaweza kuwa katika safari ndefu kutoka Ethiopia hadi Malawi kwa miezi yote hiyo ukiwa na akiba ya DOLLA MOJA?
halafu walikuwa wanapata muda wa kupumzika maana maji na hizo juice ni za bongo. RIP vijana yote ni kutafuta maisha.... Vita vibaya sana uroho wa madaraka mbaya sana, ukabila mbaya sana. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete