Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Washington DC, Marekani jana tarehe 23 JUNE 2012 Wamekabidhiwa gari aina ya Chevy Suburban na Mwanachama wao mpya Ndugu Hussein Kauzela Msabaha.
Akiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi Majimbo mengine ya Marekani.
Naye mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu kwenye kukijenga Chama.


Pigeni boksi vijana acheki ushabiki.
ReplyDeleteHongera kaka Hussein kwa kujitolea. Anayesema uache ushabiki anakosea kwani ni wajibu wa kila mtanzania kuonesha mfano katika kuijenga nchi yake. Usiposhiriki kuijenga nchi yako unataka nani akujengee. Box nalipigwe na bado maendeleo siasa ipigwe.
ReplyDeleteUnamaana gani?the comment makes no sense.please be clear .
ReplyDeleteKwa kweli Vijana mnastahili pongezi kwa kazi mnazofanya za kuitangaza Chadema Ughaibuni. Endeleeni na moyo huo mpaka kieleweke.Pia natoa pongezi kwa mdau aliyejitolea gari kwa ajili ya shughuli za chama.
ReplyDeleteBox lipigwe na bado siasa ipigwe. Kubeba box hakumaanishi huwezi ukafanya siasa. Mdau wa pili amesema vizuri hata kama kakosea kiswahili. Nchi inaongozwa na wanasiasa kwa hiyo ili kila mtu ashiriki vyema kuleta maendeleo ya nchi yake ni lazima ama yeye mwenyewe aingie kwenye siasa ama wape shavu wanasiasa. Demokrasia huijui?
ReplyDeleteGari hilo halina viwango kabosa!
ReplyDeleteKwa nini Mhe. Freeman Mbowe anayetumia gari Toyota VX-V8 la Serikali lenye namba KUB asipeleke Washington-DC kwenye tawi la Chama lile Range Rover VOGUE lake la ziada analolimiliki?
Yeye anatumia magari mawili Luxury wakati Tawini Marekani wanatumia gari chakavu!
Haya si ndio yale matanuzi ya kuagiza ndege mpya wakati wa matatizo ya kiuchumi ya Mfalme Muswati wa Swaziland?
Mnaota ndoto za chana, kama alivosema mdau wa kwanza mie nasema mnapoteza pesa yenu buree chadema kuchukuwa nchi labda baada ya miaka 10,000,000 kama dunia itafika huko
ReplyDeleteJohn Mnyika kazi kwako.
ReplyDeleteIngiza Vitz yako kwenye Kontena uitume Marekani kwenye Tawi jipya la chama kwa kuwa hilo gari ni 'mkweche' Marekani watalizuia kutembea muda si mrefu!
Tafadhali Mbunge kinusuru Chama!
mbona la zamani?
ReplyDeleteMNYIKA !
ReplyDeleteChama chako kipo legelege tuma gari lako Vitz Marekani likatumiwe na Chama kwa kuwa lile la msaada Tawini viwango chini.
Baada ya kulituma gari lako Toyota Vitz MAREKANI unafikiri utatumia usafiri gani?
Jibu ni kuwa inabidi Uonyeshe msimamo wako wa Kisiasa kuwa wewe si legelege kwa utatumia usafiri kama Waziri Mkuu wa Uholanzi wa kupanda Baiskeli!