Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    Hongera kwa aliyechukua picha hii. Picha za aina hii zinatukumbusha wengi ikiwepo mimi enzi hizo za mwalimu. Mama anaenda shambani na watoto. Hii ndio inaitwa familia sio kuwa na baby sitter wanini?

    Hapa watoto wanaangalia jinsi mama anavyohangaika ili kuwalea wao na baadaye watakapokuwa wakubwa basi kamwe hawatakuja kusahau. Heshima moja kwa moja. sio sawa na vitoto vitundu siku hizi facebook,internet, twitter ndo usiseme kabisa zen zemadudu kuangalia, etc.

    Ni hayo tu

    Mr Nyamaimewahi Kunikabashingoni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Mama analima na kuangalia watoto. Unaona watoto wanacheza pamoja badala ya kila mmoja kusikiliza muziki wake kwenye ipod au wakiangalia TV.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Ila sasa hawa watoto shule je? Ingawa wanaweza kujifunza mama anafanya nini, bado wanakosa kuwa watoto, wacheze na wanzao ikiwa ni shuleni, nyumbani na majirani n.k! Sidhani kama ni sawa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2012

    Mama analima kwa jembe la mkono. sehemu yenyewe inaonekana kubwa na kame. Hii inenikumbusha maisha ya vijini kwetu.

    Watoto hawa wana umri wa kucheza na takataka zilizikauka pale yaani kumuondolea mama hizo taka ili aweze kulima kwa wepesi zaidi , ingawa msaada wao utakuwa mdogo kulingana na umri wao lakini inalipa.

    Hapa watoto watajifunza kubweteka tu wakati wazazi wao wanawahangaikia. Bora wangekuwa shule, sawa lakini kama wana mama yao shambani angalau wasaidie kwa kiasi chao. then wacheze

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2012

    This is slavery. Those kids also will grow to do the same. My son at hat age he was playing instrument professionally. Today he is a song writer at age five. My daughter can do a lot with computer than most adults. The problem is not Facebook. It is when we sell our right to them.
    Mdau Obama Land

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2012

    kwa picha hii nanifunza kwamba nani kama mama na kuna usemi unaosema mtoto daima ni wa mama. mtazamo wangu tu kwani angeweza kuwaacha nyumbani lakini hakuna mtu wa kuwaangalina na si kwamba shule hawasomi watakuwa wanasoma huwezi jua labda ilikiwa siku ua jumamosi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2012

    Kwa wasiojua, haya ndiyo maisha hasa ya kijijini ambayo wengi tumekulia. Mama ndiye mlezi wa familia, anatoa jasho kwa jembe la mkono namna hiyo na hapo wawezakuta baba yeye kaenda kunywa pombe!! Wakati wa kurudi nyumbani mama huyo huyo anarudi na watoto, mzigo wa kuni kichwani na maji ya kupikia. Analala hoi na bado baba atamtaka unyumba usiku!!

    ReplyDelete
  8. Ananikumbusha mama yangu Evelyn Mhamilawa tukienda luhuji kulima na mama mkubwa mama sehimba then mimi na mdogo wangu tumebebewa msosi na togwa ipo pahitowo (hiyo lugha ya home sasa) it was funny indeed.
    D

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2012

    Hii inatokana na umaskini wetu...Huyu mama angependa sana hawa watoto wake wangekuwa shuleni mda ule yy anaenda shambani lakini inawezekana uwezo hana.Pia labda wabaki nyumbani na house girl lakini hana uwezo wakuwa na house girl.sasa kwakuwa yote hayo hayamudu na bado anawapenda watoto wake basi njia pekee ni kwenda nao shambani na uji wao na kuwaweka kwenye kivuli wanye uji na kucheza wao wawili kama picha inavyonyesha.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2012

    Mama hana uwezo wakuwapeleka watoto wake shule na ni mapacha. Bado wadogo hawezi kuwacha nyumbani wenyewe inabidi aje nao shamba aweze kulima pengine kabeba kipolo chake wale badaye jamani inatia uzuni sana

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2012

    Wewe mdau wa obama ni ignorant! unadhani kila sehemu kuna kinanda na computer? wewe una dharau ! mtoto wako kuandika nyimbo unaona ndio dela sana sio? hao watoto unadhani wanapenda kuona mama yao analia sdehemu kavu yenye ukame na wao wapo pembeni wanacheza na taka? muwe mnatafuta vitu vya kuandika sio dharau dharau tu ! subiri uone hiyo future ya hao watoto wako mpuuzi wewe!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2012

    Hahaaaa! Kazi kweli kweli. Yaani we mdau uliyeko kwa Obama Land inaonekana kichwa yako ina mushkeli au huelewi aliyeiweka hiyo picha ameuliza/anataka nini. Tumeulizwa tunaizungumziaje picha, we unakurupuka na "My son", "My daughter", upuuzi mtupu. Nani kakuuliza kama mtoto wako anaweza kutunga nyimbo au la!. Na huyo binti yako kutumia computer umeona deal mpaka utuambie. Kweli ukoloni wa fikra ni kazi. Haya wasalimie wanao hasa huyo anayejua kutumia computer sana kuliko wengi wetu sisi watu wazima. Nimalizie kwa kukunukuu,kwa mawazo kama haya yako "...is slavery". Mwisho wa kunukuu. Hihiiiiii.

    Ndimi Mdau wa Tandale kwa Mtogole.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2012

    we mdau wa obama land una akili timamu kweli?unaongelea maisha ya watoto wanaoishi marekani!umesahau kijijini kwenu eeh?

    ReplyDelete
  14. NiUmasikini tu hakuna kingine ndugu......ni hayo tu....!!!??

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2012

    Mdau wa Obama land this is not slavery: the kids are playing,not working,it's the mum who's working. Na wewe unaeuliza shule kwani shule ni kila muda jamani?Labda ni jumamosi? Na hivi shule ni nini hasa? Ni kuvaa sare na kukaa darasani? Hapa watoto hawa wanaweza kujifunza mengi zaidi kwa vitendo kuliko hata ambavyo wangejifunza darasani. Mimi nimeishi hivo kijijini na shule nilienda and I was quite good at it hadi leo. Tuache mawazo ya kifotokopi fotokopi,let's think realistically.
    Binafsi sioni tatizo lolote hapo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2012

    Were you in that area you would have done the same.This is not slavery as you try to claim!! Being in US with a child of 5 years playing instrument professionally does not necessarily mean you have achieved something to be imitated by those who are not living in your environment. OPEN YOUR EYES BRO!!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2012

    Anon:Tue Jun 05, 07:06:00 AM 2012

    I can't comprehend as to why you call this is slavery. If kids grow to do the same, why not? It is obvious that not all kids will grow playing instruments professionally or writing songs. I'm sure if you ask those kids you described that they play instruments where is food coming from they will i'm sure tell you that it is coming from the super market eg. Kariakoo etc!
    I personally grew up in similar environment but i haven't turned to be a slave. These days lots of kids spend time infront of a computer, tv or games consoles.Most of them become obese before at a very young age.

    That's all

    Mr Nyamaimewahi Kunikabashingoni

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2012

    wanawake wa siku hizi hawajihangaishi hivi hasa wa mjini ndio maana wana matumbo makubwa a.k.a viriba tumbo vya chips mayai............one huyo mama alivyo na shape mzuri !!! hahaaaa

    Hongera wamama wote wa kijijini

    Mdau

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2012

    EEEEEEeeeeeeenhe, hapo jamani ilikuwa ni kipindi cha mapumziko ya shule. Na huyo 'perambulator boy' anazungumzia kuhusu kucheza na toys!! Ina maana amekuwa ni mwerevu sana kwa kutumwa kwa kazi zenye kunichefua huko aliko! Hapa ni Afrika and we can't avoid being Africans and we prefer that situation rather than aping foreign misconducts'.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2012

    EEEEEEeeeeeeenhe, hapo jamani ilikuwa ni kipindi cha mapumziko ya shule. Na huyo 'perambulator boy' anazungumzia kuhusu kucheza na toys!! Ina maana amekuwa ni mwerevu sana kwa kutumwa kwa kazi zenye kunichefua huko aliko! Hapa ni Afrika and we can't avoid being Africans and we prefer that situation rather than aping foreign misconducts'.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2012

    wewe mdau hapa juu unayesema this is slavery,unakuwa kama wewe siyo mbongo mwenzetu?wewe mwenyewe ulipitia maisha ya taabu kuliko hii picha hapa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2012

    hii picha inatufunza jinsi wanawake wanavyotesema kila kitu wanafanya wao, lakini tukijiuliza walipo changia viuongo vya uzazi na kuzaa alikuwa peke yake?
    kweli watoto wanahitaji kuwa shule lakin ada ya kulipia shule ipo wapi mama hana pesa baba muhusika akiipata pesa na yake na vimada vyake na pombe kwenda mbele kwa sababu yeye ndo mwanaume au vipi?

    kwa amani watoto wanacheza mama penginewa kawaambia kaaeni hapo mcheze ili nimalize kazi msinisumbue.

    kuna mdaau kadai wangesafisha hizo taka taka ile mama amalize haraka ni kweli lakini analijua hilo kwamba watoto bado wadogo japo kuwa ndo udogo ndo unafundishwa lakini bado wadogo hata wangekuwa wangu ningewaacha wacheze kidogo, huwezi kujua kama walishamsaidia mama toka nyumbani,

    watoto wetu wa nyumbani wanakuwa vizuri sana licha ya mazingira magumu lakin watoto wa siku hizi ukiwaleta majuu utashika adabu zako kila leo ipod, tv,cell phone na adabu zimekosekana na hapo mzazi anaona vibaya kumkanya eti mtoto akiwa mkubwa hatompenda

    kazi kweli ipo ulizi wa watoto wetu majuu na wanajifanya kujua mengi kumbe wa nyumbani ndo wanaojua na kuana hali halisi ya maisha ilivyo

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2012

    @Mdau Obama Land. Mbona wewe unajikweza na kujifanya wewe ndo kila kitu? Au kwavile uko huko marekani na hilo boxx. Eti... slavery?? wewe hujioni ulivyo slavery wa hao jamaaa?? Acha zarau...pengine wewe au mzazi wako alipitia life hili....

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2012

    Mimi hii picha ningeipa title "NANI KAMA MAMA?" bless her and the kids.

    Mdau Jun 05, 07:06:00AM; Usimkufuru Muumba, na acha Mambo ya maskini akipata, matako hulia mbwata! Majority ya Watanzania bado wanaishi vijijini, kilimo ndio source ya kipato, ni kitu cha kawaida kabisa watoto kama hawa kwenye hii taswira kumsaidia mama kazi.
    It reminds me the old good times we use to visit and help Bibi (RIP) with her shamba work, it taught me determination, self control and indefatigability.

    Hongera kwa Mama huyu pichani, hopefully watoto wataenda shule umri ukifika,who knows what the future holds for them, hope this experience has taught them delayed gratification, go on kids, go on kids, you don`t have to play an instrument at 5 or compose music to be deemed bright.
    God bless.
    Dr Gangwe Bitozi, MD. (mjukuu wa mkulima)

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 05, 2012

    mdau hapo juu uliyeandika kwa kikerewe ni pumba tupu. sasa huko vijijini ina maana kila mtu ana uwezo wa kuwa na vitu hivyo ulivyovitaja? hawa watoto wametulia pengine mida hiyo wenzano wa kucheza nao wapo mashuleni...na au wapo na wazazi wao wakiwa katika shughuli kama hii. ipo mida ya watoto wa vijijini kucheza pamoja. sasa wewe unayeleta huo utamaduni wako wa kimagharibi sijui una fikra gani.......ndio wote nyinyi binti yako wa under 10 analiwa denda sebuleni then unasema ni maendeleo. ndugu hapo umechemka

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 05, 2012

    Hapo ndo mfumo dume unavyojidhihirisha ba yuko nyumba ndogo akistarehe. Naona ni siku ya Jmosi, watoto hawajenda chekechea mama kanona bora aende nao shamba maana dunia imeharibka kuwaacha pekee nyumbani waweza dhurika na binadamu wabaya.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 05, 2012

    Ni nani kama Mama..wanawake wanasifa ya kuweza kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja.waingereza wanasema MULTITASKING.This is just a symbol of how important women are in human development.
    Mdau US

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 05, 2012

    wewe mdau wa Obama land-unasumbuliwa na kasumba tu ya ukoloni mambo leo, eti computer na kakizungu kako ka kuombea mtindi, wewe subiri wakati hao hao wanao watakapolitumia neno F juu yako au kukuitia polisi -punde utakapowaambia wafunge hiyo computer wakalale kesho shule. au unawakuta wanaangalia picha za nguvu kwenye computer, hapo katika akili yako utaona poa tu maana uko kwenye Obama land, wenzio wote wamekubali heshima na jadi zetu na ndiyo maana watanzania tuko tofauti na weusi wa huko uliko-kiustaarab., Acha zako bwana we. Zebedayo

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 05, 2012

    Yeah because the lady in the picture looks like someone who can afford music lessons for her kids. If you live a privileged life then good for you but it doesn't hurt to be gracious about it too

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 05, 2012

    du picha hii imenikumbusha mama yangu tulipokuwa wadogo, kila jumamosi tulikua tunaenda shamba na mama lakini kwetu utulivu ulikuwa mdogo tulikua tunaparamia mipera kama hatuna akili nzuri he he
    mdau UK.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 05, 2012

    Huyo mdau wa Obamaland ni kijana wa fleva na pengine hata hao watoto hana ila anaandika tu kutokana na hisia zake kwamba yuko marekani hivyo anajiona yuko juu na haya matatizo hayamuhusu anataka tuya abolish tuige wamarekani. Vijana wa fleva ndivyo walivyo, wanapenda sana makuu na kujifananisha na watu wa jamii fulani. kwanza huko marekani kwenyewe waafrika wanadharauliwa na wamarekani weusi yeye anajiona amefika kwa kuwa anaishi utumwani. Ujinga mtupu.

    Mdau,
    Ushambaland, TZ

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 05, 2012

    Ki ukweli nami myambo nimepita hapa na sasa niko ugaibhuni nakula bata kama engeneer wa son, sioni ubaya ni process ya maisha tu. Hata dada sasa ni dr hapo dar kutoka kijijini muleba.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 05, 2012

    Nilichogundua kwenye hii picha ni kuwa huyu mama na watoto wake mapacha au waliopisha umri kwa kidogo sana, amekuja kupiga picha ya ku'act kama analima. Ni mchana wa jua kali ambapo kikawaida, tungeona wapi amelima kama angelikuwa amenza asubuhi au labda wakati anatupa jembe lake la kwanza na hapohapo anapigwa picha. Pili, kwa tujuao maisha ya kijijini huyu mama amepiga pamba za mtoko kwani amemechisha mtandio na kilemba...halafu akalime kweli!!! Tatu, nadhani tungeona hawa watoto wakitoka vijijasho japo kama wapo hapo mda mrefu kdogo.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 05, 2012

    Wabongo bwana. Yaani we ukipata bahati ya kukaa marekani basi. Umeshajisau ulipotokea! Jamni tujifunze kuwa humble sio vikashfa vya kilibukenu. Nazungumzia huyu mdau wa (5 year old daughter), music lessons na facebook sijui! ata haeleweki.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 06, 2012

    niko obama land too, hawa watu wasiwadanganye kuwa huku ni rahisi , yea wako ktk comp mana hakuna watoto wenzao wa kucheza nao,back to picture, wea iz ze husband, no school or ni jioni? na hilo ni jembe ama fimbo anafukia kitu, all, she will never ended up with BP or obesity like ze obama land pipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...