Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar 

Wananchi wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kilichotangaza kufanyika kwa mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba mjini hapa, kimetii amri ya Jeshi la Polisi kwa kutoonekana kwa muumini ama viongozi wa kikundi hicho katika viwanja hivyo.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema leo kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na hivyo kutojitokeza tena kwa wafuasi wa kikundi hicho kama ilivyotangazwa awali.

Inspekta Mhina amesema Kikundi hicho cha Uamsho kupitia kwa Kiongozi wake Sheikhe Farid Hadi, juzi kilijigamba kufanya Mhadhara mkubwa leo arasili katika viwanja vya Lumumba mjini hapa hata baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko, kimeshindwa kufanya hivyo kufuatia agizo la Jeshi la Polisi lakuwataka wasitishe vinginevyo wangekabiliana na mkono wa dola.

Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Mussa Ali Mussa, alitangaza kuupiga marufuko mhadhara huo na kuwataka wananchi na waumini kutohudhuria na kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo angechukuliwa hatua kali.

Kufuatia agizo hilo, Polisi wa Operesheni maalum leo, walimwagwa katika viwanja vya Lumumba huku magari yenye askari wa kutuliza ghasia yakiranda kwa kila eneo kumkabili yeyote atakayekaidi na kufika kwenye viwanja hivyo kwa madhumuni ya kuhudhuria mhadhara huo.

Hatua hiyo ya Polisi imeweza kudhoofisha kabisa hali ya majigambo ya viongozi na wafuasi wa Kikundi hicho cha Uamsho waliotangaza kufanya mhadhara huo hata baada ya serikali kupiga marufuku.

Viongozi wa kikundi hicho ambao walionekana kugawanyika waliwajulisha baadhi ya wafuasi wao kuwa hali isingekuwa swari kwa upande wao kutokana na Jeshi la Polisi kusambaza makachero na askari wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanja vya Lumumba palipopangwa kufanyika kwa mhadhara huo.

Ni wafuasi wachache tu walionekana kufika katika msikiti wa Mbuyuni kwa sala ya kawaida na pengine kupata taarifa za hatima ya mhadhara huo uliopigwa stop na Jeshi la Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2012

    hao wafuasi wachache walikua kama 5000

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2012

    CHEZEA FFU,NA BADO,,HAHAHAHAHA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2012

    sio kweli,muhadhara ulifanyika kama kawaida,polisi walizingira viwanja vya lumumba muhadhara ukafanyika viwanja vya malindi hapafiki hata mita mia tano kutoka mahali walipopanga kabla,kwa maana hiyo polisi wamedanganya umma,watu walikua ni wengi sana

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    hii taarifa ni ya uongo sana na niyaupendeleo pia , muhadhara umefanyika tena mkubwa sana tu , na muhimu sio lumumba wala malindi muhimu ni ujumbe umefika tu . acheni kupotosha habari.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2012

    haukufanikiwa kufanyika lumumba lakini umefanyka uwanja wa malindi-msikiti wa mbuyuni...na watu wamejaa,,,polisi walizingira.....
    ila ulimaliza salama na watu wakaondoka salamaaaaa

    ReplyDelete
  6. bwana mkubwa me comment yangu haiekwi..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2012

    soma habari hii http://zanzibaryetu.wordpress.com/2012/06/03/mhadhara-wafanyika-kwa-amani/#more-10137

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2012

    MADAI YA KUVUNJA MUUNGANO:

    Isiwe tabu tukakabana makoo bila sababu, ukweli wa mambo ni kuwa,

    1.Isijengeke dhana kuwa Bara inaikalia Zanzibar kwa sababu wanaopinga Muungano wanazidiwa kwa idadi na wasiopinga.

    Haiwezekani mfano idadi ya wote iwe 3,000,000 huku Wanaopinga wawe 100,000 halafu wakapewa na kuwaacha 2,900,000 HII HATA DUNIA ITATUSHANGAA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    2.Sio kweli kwamba Zanzibar inaitegemea Bara kwa kila kitu.

    3.Vile vile, Zanzibar isijenge mtazamo kuwa inavyonywa mali zake na Bara.

    KAMA WATU WANADAI KUVUNJA MUUNGANO WATUMIE UTARATIBU UNAOKUBALIKA BADALA YA VURUGU NA FUJO!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2012

    Mhadhara wafanyika kwa amani Zanzibar licha ya marufuu ya Polisi

    Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi kwa hai ya amani. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.

    Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.

    Maelefu ya waumini walihudhuria katika viwanja vya Malindi katika manispaa ya mji wa Zanzibar ambapo viongozi wa jumuiya hiyo walikutana na kukaa msikitini na kuanza kwa sala ya alaasiri na baadae kuanza mhadhara ambapo awali baadhi ya watu walikuwa wakiogopa kusogea katika ameneo ya msikiti huo kutokana na ulinzi mkali kuka kando ya barabara zote za darajani, malindi na barabara ya kuendea Bwawani.

    Akizungumza kwa njia ya simu Kamishana wa polisi Mussa Ali Musa alisema mhadhara wa Lumumba haukuweza kufanyika kwa kuwa jeshi la polisi lilitekeleza amri ya serikali ya kutoruhusu mihadhara na mikusanyiko katika kipindi hiki.

    Lakini alisema kufanyika kwa mhadhara huo katika viwanja vya Malindi wanahesabu kwamba bado hapo ni maeneo ya msikiti na hivyo hawajakataza watu kuendelea na shughuli zao za kidini iwapo watadumisha amani na usalama wa nchi.

    Akizungumza katika mhadhara huo Sheikh Farid Hadi Ahmed amesema jumuiya na taasisi za kidini zitaendelea kufanya mihadhara yake na wataendelea kudumisha amani kwa kuwa lengo lao ni kutoa sauti yao ambao wanadai Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.

    Sheikh Farid alitoa pongezi kwa jeshi la polisi na kamishna Mussa kwa kufahamu lengo la jumuiya hizo na kueleweshana namna ya kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Zanzibar wamegawanyika kutokana na misingi yao ya kivyama.

    Chanzo: zanzibaryetu.wordpress.com

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2012

    muhadhara umefanyika na nchi yetu tutaipata kwa khiari aulazima ,tumejitolea roho zetu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2012

    jua halizibwi kwa kiganja kaka!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2012

    michuzi muhadhara huu ulifanyika bro tena ulikuwa bab kubwa na ujumbe ulitufika kisawa sawa jinsi ya kuendeleza mustakabadhi wa kudai taifa/nchi yetu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2012

    Samahani administrator, Hivi kutumia logo ya uamsho katika taarifa hii ni kuifanya ionekane kuwa ni taarifa kutoka uamsho wenyewe? kufanya iwe na mvuto au kuonesha kuwa polisi wamefanikiwa sana? Nadhani tuongee na tupashane habari za kweli. Sishajiishi uchafuzi wa hewa; lakini picha inayoonekana kwenye habari hii ni kuchafua hewa na kujeruhi hisia. Kuchafua hewa ni pamoja na kusema uongo. Mbona Muhadhara ulifanyika, na Polisi waliounona? Iwe Lumumba au penginepo popote.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2012

    Kaazi kweli kweli. Ila michuzi hapa unachemsha sana nilitegemea nembo ya jumiki ingewekwa kwa taarifa yao rasmi lakini hivi unavyofanya nadhani si sahihi. Ni sawa na mtu kupost na flana na jina lako afu sio wewe.Halafu kwa nembo hii si mara ya kwanza.

    sesophy@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...