Nia na madhumuni ya ujumbe huu ni kuomba Meya wa jiji la Dar kupitisha sheria ili baadhi ya mitaa kama wa Kongo na ile iingiayo mjini maeneo ya posta kuwa ya kutembea na miguu tu,kama jinsi ambavyo wameweza wenzetu huku Russia.
Mwanzo wa mtaa unaonekana kukiwa kumesimikwa vyuma vya kuzuia magari,mitaa hiyo hakuna pikipiki wa baskeli,wakati wa siku za mapumziko kuna kuwa na wapandisha farasi na punda na michezo ya watoto.
Mwanzo wa mtaa unaonekana kukiwa kumesimikwa vyuma vya kuzuia magari,mitaa hiyo hakuna pikipiki wa baskeli,wakati wa siku za mapumziko kuna kuwa na wapandisha farasi na punda na michezo ya watoto.


mji msafi kweli tena unangara, hata mchanga hamna
ReplyDeleteJamani wenzetu wanafanya nini kupata usafi kama huu.
mdau kwani unafkiri hawajui kinachofanyika kwa wenzetu,kigali tu wamejaribu wameweza sembuse sisi,viongozi hawataki kuwajibika sio kama hawawezi,tuendelee hivi hivi.
ReplyDeleteNi kutimiza tu majukumu na kufuata sheria..kukiwa na sehemu za kutupa uchafu na watu wakatupa uchafu sehemu husika na wale walio na jukumu la kusafisha na kuzoa uchafu wakafanya ipasavyo miji yetu iakuwa safi.
ReplyDeletemdau uliyeleta wazo naungana nawe kwamba ni kweli ipo mitaa bongo ingeweza kua hivyo.
ReplyDeleteila kumbuka hadi leo hii town planning kwetu ni msamiati mgumu sana pamoja na wataalam tulionao bado mambo ni mabaya.
nchi nyingi zinachukua town planners hata kutoka nje mfano mzuri ni India ambao pamoja na kua na town planners wengi tu bado wanachukua wengine kutoka nje for complete city planning, sisi tunashindwa kuwatumia waliopo, tunashindwa kukodi planners from abroad, tunashindwa ku-implement even simple policies and strategies, tunashindwa kujiamulia na kutekeleza miji yetu iwe vipi nk.. labda tunasubiri msaada kwa yote, kwani hata waliosoma hawaonekani, wenye mamlaka ya kutunga sera hawaoni, raia wenyewe hatujastaarabika ,, kila mtu anafanya atakavyo so ni vigumu kua na mji or streets kama ulozotuonesha kwenye picha hapo.
yapo mengi ya kufanya kuanzia sasa ili tufike huko kama vile kwanza kubadilika kitabia, kujali, kependa usafi, nk.
pili ni mipango miji kwetu imekufa sio kwa dar tu bali hata mikoani serikali imelala kabisa katika suala hili na kutokuona umuhimu wake until kila mji uwe kama dar ndo watashtuka.
ukimuiga tembo kula boga uta.....
ReplyDeletekabla ya kuanza kukimbia jifunze kutembea.
Wazo zuri lakini huoni kama kuna haja kubwa kwanza ya kukomesha ujengangaji wa nyumba kiholela na pia kuboresha mitaro dar nzima? Kuzuia magari kutopita sehemu kubwa kutasaidia nini kama njia zenyewe zote zinajaa maji ikinyesha mvua ndogo tu!!!!!
Nchi inayoongoza kwa usafi duniani ni Singapore. Unadhani ni kwa nini? Huko ukitema hata mate chini unalipishwa faini ya maana. Kuna masinki vituoni ya kutema mate na maji yanatoka na waweza kunywa tape water kwa nini uteme mate chini?
ReplyDeleteHapa nachotaka kusema bila sheria binadamu hana ustaharabu. Nipo hapa Netherlands, the Hague wadutch ni wachafu sana japo nchi ina infrustructure zoote, yani mi mbwa yao inakunya hovyo hovyo ukitembea kama uangalii chini basi viatu vitarudi havitamaniki.
Kwa nini? Sheria haziwi enforced ingawa nasikia zipo.
Binadamu bila kibano ni mchafu tu. Theory ya tragedy of the commons ina apply hapo.
Sisi ni masikini sikatai; lakini waweza kuwa masikini na bado msafi; mshatembelea nyumba ya wazaramo nyie. Uwanja umefagiliwa saaaafi; si mpaka uwe na rami ndo uwe msafi bana.
Mbona Mwanza na Moshi wanaweza. Ndiyo, wanatakiwa kuongeza juhudi, lakini tayari wanaweza. Swali hapa ni kwa miji mingine kama Dar, n.k., kwa nini wachafu?
ReplyDeleteBongo kumekucha jamani,jiji linaonekana kama majuu?
ReplyDeleteMi na mchango tofauti kidogo.Kuna suala la kucontrol aina za magari yanayopita mtaa fulani.Nimeona Uingereza wakisema mtaa huu mwisho ni tani tatu basi mwanzo na mwisho mwa mtaa wanaweka mambomba mazito kama magoli ya mpira ambayo urefu wake say kwa tani tatu labda ni maroli madogo madogo.
ReplyDeleteUtakuta mbasi mkubwa mitaa ya mtogole au semi trailer.Tabu tupu
KILA KITU KINAWEZEKANA, TATIZO NI KWAMBA WATU WENGI HAWANA ILE 'SENSE OF BEUTY' UCHAFU DAR JAMANI UMEZIDI, WAKUU HEBU IGENI MJI WA MOSHI ULIVYO MSAFI, YOTE HIYO NI KUJITUMA. VIJANA WASIO NA KAZI WAPEWE HIZO KAZI KWA UJIRA WA KILA SIKU, PILI WAFUNGWA WA VIFUNGO VYA NJE WAFANYE HIZO KAZI, JIJI LINGEBADILIKA.
ReplyDeleteHilo wazo lako naliunga mkono. Mungu atusaidie watanzania tupende usafi wa mazingira yetu.
ReplyDeleteViongozi chukueni Hatua ya usafi wa mazingira.