Mharisi wa gazeti la Jamhuri, mpiganaji Manyerere Jacton (kati) akiwa na viongozi wa UAMSHO baada ya kufanya nao mahojiano huko Zanzibar. Usikose mahojiano maalumu ya viongozi hawa wa UAMSHO na Gazeti la Jamhuri Jumanne wiki hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    safi sana michuzi kwa kuweka hii kitu, na mheshimiwa manyerere tafadhali mkuu uandike yote waliosema ili jamii ipate kujua ukweli kwamba hawa watu sivyoo wanavyo wafikiria, ni viongozi wenge busara na sera zo,si wahuni wala watu wa udini.Wanatete nchi yao period.
    umenifurahisha sana mheshimiwa manyerere kwenda kuwahoji wakuu hawa ubarikiwa sana bwana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    SULUHISHO LA KUDUMU LA MUUNGANO KWA PANDE MBILI:

    WANAOPINGA MUUNGANO NA WASIOPINGA MUUNGANO,

    KUPANGA UENDESHAJI WA MAMBO KWA PAMOJA HAKUWEZI KUVUNJIKA KWA GHAFLA KAMA WANAVYOTAKA WANAODAI KUVUNJA MUUNGANO.

    IELEWEKE DIRA, UENDESHAJI WA JAMII NA MWNENDO WA UTAWALA HUGHARIMU NA UWEPO WA KUJITOA MUHANGA KWA MALI WAKATI NA RASILIMALI.

    MUDA UNAVYOENDA MFANO TOKEA MUUNGANO MWAKA 1964 PANA GHARAMA ZIMEPITA PANDE ZOTE MBILI YAANI BARA NA VISIWANI.
    -----------------------------------
    SULUHISHO:
    -----------------------------------

    ZIPIGWE KURA ZA MAONI NA MATOKEO YAAKISI UAMUZI KAMA MUUNGANO UENDELEE AU UVUNJIKE:

    PAWEPO NA ULE MPANGO WA URAIA WA NCHI MBILI (DUAL CITIZENSHIP)

    ENDAPO KURA ZITAPIGWA HALAFU MTU ASIYERIDHIKA NA MATOKEO ITABIDI AHAME VISIWANI NA KWENDA NCHI YA PASIPOTI YAKE YA PILI ILI KUPISHA MABADILIKO ASIYOYARIDHIA.

    1.KAMA WAPINGA MUUNGANO WATASHINDA, BASI WANAOUNGA MKONO MUUNGANO WAHAMIE BARA AU WAENDE NCHI ZINGINE KWA URAIA WA NCHI YA PILI.

    2.ENDAPO WASIOPINGA MUUNGANO WAKISHINDA WAPINGA MUUNGANO WAJIANDAE KUHAMIA (OMANI) AU WAENDE NCHI ZINGINE KWA KUWA NI WAZI HAWATATAKA KUJA BARA.

    HAPO NDIO UTAKUWA MWISHO WA MALUMBANO!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Assalam Alaykum!

    Ni hatari sana kutafuta kufikia malengo kwa mgongo wa Dini!

    Masheikh msitafute umaarufu kwa njia hatari kama ya machafuko!

    Kwa nini msihubiri Dini pekee?,,,au kama vipi kwa nini msijisajili kama Wanasiasa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2012

    MADAI YA KUVUNJA MUUNGANO:

    Ni sawa na uwezekano wa watu 13 wanaokula sinia moja la ubwabwa hakafu watu wa 3 kati ya hao 13 wakataka mchuzi wenye pilipili umwagiwe juu ya ubwabwa!

    Mbaya zaidi hao wanaodai mchuzi umwagiwe hawazingatii kama wenzao 10 waliobaki huenda nawa 'Vidonda vya tumbo' hivyo kikanuni hawali pili pili!

    WAPINGA MUUNGANO -3
    WASIOPINGA-10

    Kwa msingi wa mfano huo ni dhahiri ya kuwa matakwa yenu Wapinga Muungano hayatimiziki wala hayatekelezeki!!!

    HAKUNA SERIKALI HATA MOJA DUNIANI HATA IWE YA KIISLAMU KAMA YA SAUDI ARABIA INAYOWEZA KUTEKELEZA MADAI KAMA HAYA YA WALA UBWABWA WA 3 KATI YA 13 KTK KUNDI !!!

    YAANI NDANI YA KUNDI LA WALA UBWABWA 13 WALA UBWABWA WA 3 WAWAENDESHE KIMAAMUZI WALA UBWABWA 10..... HAIWEZEKANI!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2012

    Assalam Alaykum,

    Masheikh haiwezekani Serikali ikawaajiri wananchi wote Visiwani kuwa Watumishi wa Serikali!

    Hii hata JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN, UFALME WA SAUDI ARABIA, NA SERIKALI YA USULTANI YA OMANI waziwezi !!!

    Nchi ina watu 5 Milioni Wafanyakazi Serikalini (AKIWEMO MAALIM MWENZENU SHEIKH SEIF SHARRIF HAMAD hawazidi 100,000) !!!

    Hivyo ninyi Masheikh Baada ya Mihadhara (YA MAFUNZO YA DINI YA KIISLAMU NA SIO UCHOCHEZI NA FUJO) pamoja na wengine 4,900,000 mshike majembe mkalime mashambani ama mkavue samaki baharini!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2012

    Dini ni mfumo mzima wa maisha ya binaadam...bila ya dini tungekuwa tunaishi kama wanyama hapa duniani....kwasababu watu wangekuwa hawajui chochote, ila dini ndio inayotuongoza lipi baya, lipi zuri...na ndio maana tunaenda misikitini, makanisani, mahekaluni na sehemu nyengine kutokana na imani ya mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...