Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo

Njee ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara.

Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutairiwa.

Bwana Chebundo anasema kuna wabunge zaidi ya 120 na wafanyikazi wa bungeni ambao wameonyrsha nia yao ya kutairiwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza atari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.

Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka wa 2007 shirika la WHO inasema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri wanaume.

Jana, wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi.

Wabunge hao wanachochea wanaume nchini Zimbabwe kukubali kutahiriwa, kama njia mojawapo ya kupumguzu maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Hii nikutokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa karibu robo ya wanaume wote nchini Zimbabwe wameambukizxwa virusi.CHANZO BBC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    wazimba kumbe ma stelingi wa kihindi?...lol (govinda)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Na wabunge wetu wafuate utaratibu huu haraka iwezekanavyo jamani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Si Zimbabwe tu, naamini hata bongo pengine zaidi ya 50% ya wanaume/wavulana hawajatahiliwa. Ukienda Asia ndo haswaaaaaaa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2012

    Khaaaa Makubwa haya!

    Yaani mpaka mtu unapanda Jukwaani unapigana Kiume kutafuta Ubunge kumbe bado mzigo unao kibindoni huja onana na Dakitari?

    Enhhh inafikia unaapishwa na kuiniga Bungeni lakini bado unao 'mpira' wa soksi iliyo wazi mbele kibindoni!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2012

    Sasa Wajameni unakutana na Mwanamke aliyekwisha pitiwa na Mwanaume huyu mwenye hilo (2o...ba)

    Mfano ulikuwa hujui na inafikia watu wanakunong'oneza wanakwambia kuwa Bwana 'Karumanzira' anayejulikana na watu wooote ya kuwa bado analo amekwishapita hapo kwa Bibie!

    Hapa inakuwa vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...