Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeanza vyema mchezo wake wa kwanza wa mashindano ya VIVA world Cup uliochezwa jana saa 4 usiku katika uwanja wa Francios Harir ndani ya jiji la Ebril, Kurdistan kwa kuwabamiza bila huruma timu ya Ratia kutoka bara la Ulaya mabao 6 kwa bila.

Heros walicheza kwa umakini mkubwa katika dakika 20 za kwanza, wakijaribu kuusoma mchezo. Iliichukua Heroes dakika 33 kupata bao la kwanza lililofungwa na Khamis Mcha (Viali) ambae katika mchezo huo amefunga ha-trick. Mabao mengine mawili aliyafunga katika dakika ya 41 na 57.

Wafungaji wengine wa heroes walikuwa ni Abdi Kassim (Baby) dakika ya 51, Awadh Juma alieingia kipindi cha pili aliifungia Heroes mabao 2 katika dakika za 88 na 90 za mchezo.Katika mchezo huo, Zanzibar Heroes walionekana kuelewana vyema,kuanzia nyuma, kati na safu ya ushambiliaji.

Wapenzi wengi waliodhuria walivutiwa sana na kiwango cha mpira cha Zanzibar heros, huku wakipongeza na wengine wakitabiri inaweza kufika fainali. Wachezaji wote wako na afya njema, hakuna majeruhi huku wakiwa na ari kubwa ya kuchukua kombe hilo kwa nchi wasio wanachama wa FIFA.

Katika mechi nyengine, wenyeji Kurdistan waliwashinda Western sahara kwa 6-0, na mechi ya Awali Dafur walifungwa 15 na Nothern Cyprus.

Zanzibar heroes itacheza mechi yake ya pili kesho usiku na ikishinda watajihakikishia kucheza nusu fainali

Mdau na kiongozi wa msafara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2012

    HII ndio ZANZIBAR .....hongereni sana watoto na wembe huu huu ndio tutakaokuja kuwanyowa watanganyika baadae ....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2012

    Well done guys keep it up?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2012

    Unapokuwa unaandika habari tafadhali jaribu kuwa na ufasahaa kidogo. Leo ni Juni 5 si April moja siku ya wajinga duniani. Nikuulize, kabla ya Zanzibar kuifunga hii timu, je ulishawahi kuisikia hapa duniani? Hii nchi japo iko bara la Ulaya ya mashariki lakini ni duni shinda hata Zanzibar yenyewe na haifai kufananishwa na nchi zingine za Ulaya. Sema tu Zanzibar imeifunga timu ya wakurdi (Kurdikistan)basi, sio timu ya Ulaya. Unatupotosha, ungekuwa unauza magazeti mbona ungetupata leo na nyumba ya ghorofa ungejenga.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2012

    Hongera Zanzibar. Anon #3 pole kwa wivu. Kiriba hicho, unacho babu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...