Redd's Miss Singida 2012,Zena Mondi (katikati) akiwa na mshindi wa pili Rehema Marwa (kushoto) na wa tatu Eliza Diamond mara baada ya kumalizika kwa shindano lao na kutangazwa mshindi.shindano hili limefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Aqua mjini Singida
Warembo walioingia tano bora.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikabidhi zawadi kwa Zena Mode, baada kuibuka mshindi, shindano la Redd's Miss Singida, lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Aqua mjini Singida. Mshindi wa kwanza amepata sh. 400,000, wapili sh. 300,000 na wa tatu sh. 200,000. Akifungua shindano hilo, Nape ameahidi kwamba CCM itatoa ajira kwa Miss Singida kama atafanikiwa kuingia katika tatu bora katika shindano la Miss Tanzania na kwamba CCM inayatambua mashindano ya urembo hapa nchini.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimtuza Khadija Kopa wakati akitoa burudani katika shindano hilo
Muimbaji wa muziki wa Taarab nchini,mkongwe Khadija Kopa akitumbuiza mashabiki wakati wa shindano hilo mjini Singida.Picha na Bashir Nkoromo.







Nimeamini Singida kuna Warembo.
ReplyDeleteKwa nini hawa watoto wetu wasibaki na nywele zao za asilia wakati wa mashindano haya? Binafsi naumia kuona hizo nywele zisizo asilia zikichangia kuonyesha urembo wa wasichana wadogo.
ReplyDeleteAnon. wa pili hapo juu, Kizazi cha zamani sio cha leo hii, ukiangalia warembo wa siku hizi kuanzia utosi mpaka unyao bandia tupu, kumi kwa mmoja utakaemkuta yupo kiasilia na vigumu akafika hapo walipo hao. Nadhani tufike wakati tujaribu kinyume chake, badala ya kuangalia huu urembo bandia/madukani, tujaribu na kutafuta warembo asilia nadhani itapendeza na kuwanusurisha na mengi wasichana wetu/watoto wetu wa kike.
ReplyDeleteIla jamani huyo mwenye 'nguo nyeupe kwa kweli alistahili' sijui tu kimetokea nini?
ReplyDeleteKwa mw'ume yeyote wa kiafrika na aseme kama hajavutiwa!
"uzuri wa kondoo mkia bwana!!"
wewe mtoa maoni wa mwisho, jua kwamba ,katika mashindano haya ,siyo sura pekee inayomfanya mshindani ashinde NO kuna mengi sana huangaliwa hapa, (1) muondoko,(2) kupozi (3)na kikubwa zaidi anapojieleza ,hapa sasa ni ngoma kweli kweli maana kinaangaliwa upeo wake wa kufikiri na kufafanua jambo common sense. wewe kwa vile ni kalaga baho umeona sura tu- wasalam alekoum.Zebedayontishin
ReplyDeleteKinachoangaliwa katika judgement ni zaidi ya urembo. Ufahamu wa mambo mbali mbali, kujiamini n.k. hivyo kama mshindi alistahili kwa muonekano wa macho ya watu tu haitoshi. Ndiyo maana mara nyingine, majaji huonekana wamependelea kwa vile watazamani hudhani mrembo ni yule mzuri wa sura, umbile n.k
ReplyDelete