Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe ( mwenye Kaunda suti) akiangalia moja ya Injini ya Treni ambayo imefanyiwa matengenezo makubwa ikiwa ni mpango wa kufufua vichwa vinne vya Treni katika Kaarakana ya TRL Morogoro.
 Baaadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania , katika Karakana ya Morogoro,  wakiomba dua iliyotolewa na mmoja wa mfanyakazi wa dini ya kikristu kwa ajili ya  kumwombea afya njema Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe aliyetembelea Karakana hiyo Juni 23, mwaka huu na pia kuiombea Kampuni hiyo iweze kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi kipindi hiki cha kufufuliwa kwake.
 Dua kwa Waziri
 Baadhi ya wahandisi na mafundi wa mitambo wa Karakana ya TRL Morogoro wakiendelea kutengeneza moja ya Injini aina ya 89 XX yenye uwezo ni kuvuta behewa 20 hadi 30 , matengenezo makubwa ya Injini ya uwezo huo hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa vichwa vya treni.

Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe ( wapili kutoka kulia mwenye Kaunda suti) akiwaameongozana na baadhi ya watendaji wa kuu wa Kampuni ya TRL akiwemo na Meneja Mkuu Mhandisi Amani Kisamvu ( watatu kutoka kulia) wakielekeza eneo maalumu lililoandaliwa kuzungumza na wafanyakazi wa Karakana ya TRL Morogoro , hiyo ilikuwa  ni moja ya majukumu yake ya kutembelea sekta  zilizopochini ya Wizara yake. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    MHESHIMIWA MWAKYEMBE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WACHACHE WA CCM WANAO FANYA KAZI ZAO KIKAMILIFU. KAMA CCM INATAKA KUBAKI MADARAKANI WAMSIMAMISHE MWAKYEMBE KAMA MGOMBEA WA URAIS 2015.
    MWAKYEMBE NI MTU SAFI, MSOMI, MWANASHERIA, HAOGOPI MTU, MCHAPAKAZI NA AMEONYESHA UWEZO WAKE NDANI YA CCM. WAKILETA MGOMBEA MWINGINE WA KUBABAISHA , CHADEMA INACHUKUA NCHI MCHANA MCHANA. BY THE WAY WHERE IS HON FILIKUNJOMBE? HE IS ANOTHER STRONG MAN WITH PRINCIPLES.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...