Miss Sinza 2012, Brigita Alfred katikati akiwa na mshindi wa pili, Judith Sangu (Kulia) na Esther Mussa (Mshindi wa tatu kushoto) pamoja na warembo wengine, Mariam Miraji na Nahma Said amabo walishika nafasi ya nne na tano.  

MREMBO Brigita Alfred usiku wa kuamkia jana alitwaa taji la Redds Miss Sinza baada ya kuwashinda wenzake 13 katika kinyang’anyiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge).
Brigita alionekana tokea mwanzo kuwa ataibuka uwa mshindi kwani aliuteka umati wa mashabiki wa masula ya urembo katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kinywaji cha Redds, Dodoma Wine, Lady Pepeta, Flexi P, Jackz Cosmetics, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com na Screen Masters.
Kwa ushindi huo,Brigita alipewa shs 500,000 na tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya Redds Miss Kinondoni. Mshndi wa pili katika kinyang’anyro hicho alikuwa Judith Sangu aliyezawadiwa sh. 400,000 na mshindi wa nafasi ya mshind wa tatu ilikwenda kwa Esther Mussa na kupewa shs. 300,000.
Mariam Miraji alishinda nafasi ya nne nay a tano ilikwenda kwa Nahma Saidi.  Warembo wote hao watano walipata tiketi ya kushindana katika mashindano ya Miss Kinondoni.
Warembo wengine waliobaki, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John,  Eva Mushi, Vailet John, Christina Samwel, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi na Merina Mushi walipewa  zawadi ya kifuta jasho cha shs 100,000 ila mmoja katika shindano hilo lilopambwa na bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Brigita na hongera sana sana Juddy. You are beautiful and talented, and the judges saw that too. love mingi, big sis

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2012

    Ama kwa hakika huyo Bi Brigita ana stahiki kutwaa taji hilo!!! La hashaa hakupendelewa ni stahiki yake!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...