Na Mashaka Mhando,Handeni
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapteni Honest Ernest Mwanossa, amemwagiza Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, kufuatilia matuminzi ya shilingi milioni 54 zilizojengewa zahanati ya kijiji cha Kweingoma wilayani hapa kufuatia jengo hilo kuonekana likiwa limejengwa chini ya kiwango.
Kiongozi huyo alitoa agizo hilo juzi alipokuwa amekwenda kwenye kijiji hicho kufungua zahanati hiyo iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa gharama ya fedha hizo lakini kiongozi huyo ameikuta zahanati hiyo kuta zake zikiwa zimepasuka huku milango na madirisha yakiwa ya kiwango cha chini kabisa.
"Mkuu wa wilaya nakuagiza fuatilia matuminzi ya fedha katika zahanati ile, nimeifungua tu basi lakini sikuridhishwa nayo maana imekuwa na mapungufu mengi ukiitazama tu maana kabla hajaijakaliwa tayari kuta zake zimepasuka, milango hairidhishi, hii inaonekana wasimamizi wa jengo hili, wamefanya ili mradi ni jengo la serikali aiwezekani wachukuliwe hatua,"alisema Kapteni Mwanossa.
Kiongozi huyo aliridhishwa na jengo la ofisi ya Mtendaji wa kata ya Kwamatuku iliyojengwa kwa shilingi milioni 18 lakini jengo hilo lilionekana kuwa zuri na hivyo kumpongeza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni Hassain Mwachibuzi na mkuu wa wilaya hiyo kwa kuhakikisha jengo hilo limesimamiwa vizuri na fedha yake imeonekana.
Kapteni Mwanossa alisema lazima wakuu wa wilaya wawe makini katika kusimamia miradi ya maendeleo kwani baadhi ya watendaji wanatumia mwanya wa fedha za miradi kuzitumia vibaya wakijua kwamba serikali haiwezi kuwafuatilia hatua ambayo inasababisha serikali hasa Rais Jakaya Kikwete kusemwa vibaya ilhali imekuwa ikitoa fedha nyingi za maendeleo.
Alisema watendaji hasa wa halmashauri wamekuwa wakifanya kazi kwa manufaa yao binafsi na kushindwa kufuatilia majukumu ya Kitaifa kwa kuchukua fedha za miradi kujenga nyumba zao za kuishi hatua ambayo kwa sasa haiwezi kuachiwa kwani watendaji hao wamekuwa wakiandika risiti za uwongo jihalalishia fedha hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya agizo hilo, Mkuu wa wlaya hiyo alisema kuwa tayari amemwagiza mkuu wa idara ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo kuwachunguza Msimamizi wa mradi wa TASAF wilaya ya Handeni na Mhandisi wa ujenzi wa wilaya hiyo kujua ni namna gani fedha hizo zimetumika lakini jengo limeharibika kabla ya matuminzi yake.
"Nimemwagiza kamanda wangu wa TAKUKURU afuilie suala hili, maana sikuwahi kutembelea jengo hili kabla kutokana na kushughulikia matatizo ya ukosefu wa maji katika mji wetu wa Chanika...Lakini sasa nitaanza ziara katika vijiji kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ili wale walioharibu tuweze kuwashughulikia," alisema Muhingo.
Alisema tatizo kubwa katika wilaya hiyo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la ardhi ambapo kumekuwepo na migogoro mingi inayosabbishwa na watu kuhodhi ardhi nyingi bila kuzilima hatua ambayo inawafanya baadhi ya wananchi wakose maeneo ya kulima.
Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu umebeba ujumbe wa kuhamasisha Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 26 mwaka huu unaosema "Sensa ni Msingi wa Mpango wa Maendeleo Yetu," wenye kauli mbiu Shiriki Kuhesabiwa tarehe 26 Agosti, 2012, ikiwemo mabadiliko ya katiba ukieleza "Jitokeze kutoa maoni' pia wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiongozwa na Kapteni Mwanossa, wamekuwa wakiuelezea ujumbe uliozoeleka wa suala la Rushwa, Ukiwmwi na madawa ya kulevywa.
Naomba msaada ndugu Mwenyekiti...hivi Kiongozi wa mbio za mwenge anaweza kumwagiza Mkuu wa Wilaya juu ya jambo fulani? Kwa maana nyingine ni nani mkubwa kati ya Kiongozi wa mbio za mwenge na Mkuu wa Wilaya? Naomba nieleweshwe.
ReplyDeletehata mie nimeshangaa sana kuhusu hili suala,hivi ni kweli mkuu wa wilaya anaweza kuamriwa na kiongozi wa mbio za mwenge nani mkubwa kati ya hao wawili? naomba kueleweshwa pia asante.
ReplyDeleteMnashangaa nini wakati nchi haijui kufuata protocali kwani hapa kila mtu anaamua kufanya anachoona kwake ni sawa.
ReplyDeleteKwa hiyo hata huyo mkimbiza mwenge ameona hicho ni cheo kukubwa sana usije shangaa akatoa oda hata kwa RC?!!!!
Hiyo ndiyo Tanzania yetu
Hongereni sana Wa Tz.
wadau wenzangu hiyo ndo bongo hiyo hamjui kwamba mkuu wa kukimbiza mwenge ndo rais kwa sababu bado anafikra za muazilishi wa mwenge. ha ha ha bongo bongo mtajijuuu
ReplyDelete