Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni jambo lisilokubalika kwa mwanamke kupoteza maisha wakati akijifungua kwa sababu uja uzito siyo ugonjwa.
Aidha, rais Kikwete amesema kuwa pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kupunguza vifo vya akinamama wakati wa uzazi na mipango mingine ya uzazi bora, bado tatizo linabakia kubwa na zinahitajika juhudi zaidi ili kuondokana na tatizo la vifo wakati wa uzazi.
Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Alhamisi, Julai 19, 2012, wakati alipokutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Pathfinder International, Dkt. Purnima Mane, Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo lisilokubalika kabisa kwa mwanamke kupoteza maisha wakati akijifungua. “Uzazi siyo ugonjwa na kwa hakika ni jambo lisilokubalika kwa mwanamke kupoteza maisha wakati akijaribu kutoa maisha kwa binadamu mwingine. Hili ni jambo ambalo Serikali itaendelea kupambana nalo hadi kulifikisha mahali pazuri zaidi.”
Rais Kikwete amesema kuwa ni kweli kuwa Serikali yake imekuwa inafanya juhudi kubwa katika eneo hili lakini bado tatizo ni kubwa na zinahitaji jitihada za ziada. “Tumefanya jitihada kubwa na kupata mafanikio ya kujivunia lakini bado kazi ni kubwa.”
Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa akinamama 578 kati ya 100,000 hupoteza maisha wakati wa uzazi, idadi ambayo imeshuka kutoka miaka minne iliyopita wakati takwimu zilionyesha kuwa akinamama 790 kati ya laki moja walikuwa wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.
Miongoni mwa maamuzi ambayo Serikali imechukua kukabiliana na tatizo hilo ni pamoja uamuzi wa kupunguza umbali wa kufikia huduma za afya kwa kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata na hivyo kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana katika umbali usiozidi kilomita tano.
Serikali pia imeamua kuwa kila zahanati ama kituo cha afya lazima kiwe na huduma za kuhudumia wazazi na waja wazito.
Serikali pia imechukua hatua za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ambao ni moja ya chimbuko kubwa la vifo vya akinamama waja wazito.
Dkt. Mane ambaye anatembelea Tanzania kwa mara ya kwanza amemsifu Rais Kikwete kwa uongozi wake katika masuala ya afya na masuala mengine. “Uongozi wako katika suala hili ni jambo linalojulikana duniani pote. Tunakushukuru sana kwa sababu wewe ni bingwa wetu na msemaji wetu mkubwa katika mapambano ya usalama wa akinamama waja wazito.”
Pathfinder International ni shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali ambalo malengo yake makuu ni kushughulikia afya za akinamama na kuboresha uzazi. Katika Tanzania, Pathfinder International linaendesha miradi tisa kwa sasa katika maeneo ya ukimwi, masuala ya uzazi na uzazi wa mpango.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Julai, 2012



kwa kweli hilo kwetu tuna mwendo mrefu kwani sheria za Afya hazijawabana sana madaktari kwa hapa uingereza Daktari anakuwa na mshike mshike ikimtokea tofauti na kwetu shughuli zote hazifanywi kwa ushahidi ila kwa wenzetu kila hatua inawekewa ushahidi kwani ikitokea mzazi akafa watu wake wanakuja juu na vyombo vya habari vinabeba bango hivyo mpaka sheria za wizara zipite kwanza kujenga utamatuni wa evidence na kuwa answerable na makosa.
ReplyDeleteTamko lako limekuja wakati juzi kuna mama kajifungua na kufariki huko Handeni kwa sababu ya kukosa matunzo kwani mume wake alimkimbia na kumwacha na mimba na watoto wengine.
ReplyDeleteMweshimiwa raisi hali hii ni mbaya sana hasa vijijini na sijui kama hawa watendaji wanashughulikia vipi na hali kama hizi,watu kama hawa washitakiwe kwa kukwepa majukumu.
Ni kweli uja uzito sio ugonjwa lakini kuna mambo mengine yanasababisha mpaka ionekane ni ugonjwa.
Watakosaje Kufa wakati hospitali hazina vifaa hata gloves mtu anamfungulisha kwa kutumia kanga yake halafu unasema wasife at the sametime unatimua madaktari we unadhani vifo vitazuirika pasipo daktari???????
ReplyDeleteMkuu najiuliza sipati Jibu
Nina rudia tena tagazo hili siyo la ukweli. Administration ya Rais Kikwete, ina fahamu wazi kwamba imeshindwa kuwa sadia wakinamama wasiyo marafiki au jamaa toka Rais amechukuwa madarka. Msaada utaonesha kwamba marafiki na jamma ndiyo wana faidi siyo wakinamama wegeneo! Rais Kikwete ana fahamu yeye binafasi kwamba hakuna Imani kwenye administration yake!
ReplyDeleteJamani kweli kama umeme unakatika wakati wa kufanya csection itakuaje, wakati mwingine generator linaishiwa mafuta, madaktari wamegoma, hakuna vifaa vya kufanyia upasuaji, hospitali ni kilometer 10, Daktari hajalipwa cha juu, mama mjamzito amekosa pesa ya kulipa! Yale yaliyotokea Temeke, sasa kwakweli hapa kuna kuokoa maisha ya mama mjamzito? Tuwe wakweli kwani bajeti ya chai ya ikulu katika fiscal year ni 15bilions na zinatolewa zote! bajeti ya wizara ya afya ni 63.5 bilions zinazotolewa kwa mwaka 13bilions kweli hapo kuna uwiano na tutamaliza matatizo ya vifo vya kina mama wajawazito kweli? Ankal huu ni mwezi mtukufu usipoweka ujumbe huu mwezi huu hautakuwa na maana kwako! Asante nimeandika kwa machungu makubwa!
ReplyDeleteNi kweli kabisa, serikali ni vizuri ifanye kampeni ya "ujauzito sio ugonjwa, kwa nini wanawake au watoto wafe?". Nchi nzima iwekwe mikakati ya kuzuia vifo hivi, kwani saa nyingine vinasababishwa kwa makusudi
ReplyDelete