Assallam Alleykum Ankal
Naomba uniwekee katika blog yetu hii miji miwili Nairobi na Dar ili wadau wachangie mawazo yao!
Ni mji gani kwa muonekano wa picha unaovutia?Mimi kusema ukweli wangu Dar ndo ina muonekano wa kunivutia zaidi ya Nairobi. Ila kuna wenzangu hapa wanadai eti Nairobi iko bomba. Mimi nawaambia nimetoka TZ miaka ya zamani, na kwa sasa imejengeka mno!..
Eti ni kweli Nairobi ndo mji mkuu East Africa?
Na kwa biashara pia eti inaongoza??
MDAU 
Central Dar es Salaam, Tanzania
Dar es salaam
Nairobi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2012

    ni kweri kwa sasa dar ndio dubai ya afrika mashariki na kati kwani mambo yamebadirika sana na hasa kwa wale walioondoka kipindi kirefu kilichopita ni kweri kuna mabadiriko makubwa sana kuanzia miundo mbinu hadi majengo sio kama hapo awali bongo kumekucha jamani kwa tulio nje sio kama zamani kazi kwetu kujipanga kwa maendeleo ya bongo - mdau richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2012

    Masahihisho:

    Ni kweli na wala siyo kweri.

    Asante

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2012

    si kweli huwezi linganisha Dar na Nairobi. Nairobi imeizidi Dar yetu kwa mbali sana kuanzia miundombinu mpaka majengo.

    ReplyDelete
  4. Salaam Alleykum Ndugu Mdau. Swala la kuwa ni mji gani zaidi ya mwingine lina mambo kadhaa ya kuzingatia. Sio kwa majengo au kujengeka zaidi, hasha!
    Nairobi ni jiji ambalo linatambulika kama mahali pa kuingilia Afrika ya Mashariki. Yapo mambo mengi yanayofanya hivi. Uthubutu wa wenyeji wa huko katika maamuzi ya kibiashara, nk. Mambo mengi kama mitindo ya mavazi, biasara za kimtandao, ubunifu wa mambo mengi mapya huingia kupitia Nbi kuja Dar na kwinginepo. Hta ukiangalia mtandao wa njia za mawasiliano huingilia na kutokea Nbi.Sio kwa Dar pekee, bali hata miji mingineyo ya Afrika Mashariki kama Kampala, Kigali na Bujumbura hupokelea mengi kupitia Nbi.
    Mimi ni mzalendo na mwelewa wa haya mambo nikiwa Mtanzania halisi na mwenye mapenzi na nchi yangu.
    Swala la majengo ni maendeleo yanayoibukia kwa sasa na kuna jitihada kubwa kwa sasa Dar inajendeka vizuri. Mwazo bunifu ya Mhesh. Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mipango Miji ni mkakati unaotuelekeza mengi mema ya kimaendeleo. Hayo ndio machache yangu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2012

    Nairobi bado inatisha aiseee. Bongo bado tunapambana tuwafikie. Huo ndo ukweli halisi.

    Mdau Dar.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2012

    Mbona hujaweka picha ya dar tulinganishe? Dar nadhani inaweza kuwa na majengo ya kisasa kuliko nrb kwa sababu nrb imeendelezwa zamani kuliko dar ila nadhani nrb imepangika vizuri.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2012

    Dar es Salaam inapendeza zaidi ya Nairobbery! Kwa sisi tuliofika Kibera na Mathare tunamshukuru Muumba wetu kuwa hakuna "madudu" kama vile kama Kibera na Mathare ambayo yalinfanya nitake kumwaga machozi kuona jinsi binaadamu wenzetu Waafrika wanavyoishi! Wahenga wanasema "Hata ukifagilia uchafu kuuficha uvunguni, uchafu utaendelea kuwa uchafu". Uhuru Park, Westlands na Runda haziwezi kuficha hali halisi ya Nairobbery ambayo inongoza kwa slums duniani baada ya Brazil.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2012

    Mbongo niliyekuwepo Bongo na mfuatiliaji wa Viwango AFRIKA YA MASHARIKI nasema:

    UKWELI NI HUU:

    Kila sehemu kati ya Nairobi na Dar zina sifa na upungufu zilizopishana.

    1.NAIROBI:
    SIFA
    -Kibiashara ipo juu zaidi ya Dar inaongoza Afrika ya Mashariki, inafuatiwa na Kigali-Rwanda.

    -Miundo mbinu Nairobi imejitahidi kuweka hadi 'Flyovers' yaani barabara za juu ili kupunguza msongamanao wa watu mjini, huku Treni zikitumika kuhudumia wakazi wa Jiji na Vitongoji vyake.

    -Majengo, wamejitahidi sana mfano yale ma Super Market Jijini Nairobi yanayokuwa na ngazi za mikanda ni makubwa na pia pana Mradi mkubwa TATU CITY upo mbioni kuwekwa hewani.

    UPUNGUFU:
    -Kiwango cha mgawanyiko wa hali za watu ni mkubwa, kulingana na hali zao, jiji linaongoza Afrika ya Mashariki kwa kasi ya kukua kwa Umasikini.

    -Hali ya maisha ni ngumu,vitu kuwa bei ghali na fedha kuwa ngumu kwa wengi wa wa wakazi wa Jiji huku Mabilionea wachache wakila maisha maziwa kwa asali.

    -Hali ya Usalama ni tete kutokana na vita dhidi ya Al Shabaab, huku kiwango cha uhalifu kikiwa juu zaidi ktk Afrika ya Mashariki.

    -Flyovers huku zikiwa hewani zimejengwa chini baadhi ya maeneo barabara ni mbovu na kukithiri kwa uchafu sehemu za pembeni ya Jiji(sio katikati), pana Jalala kubwa sana linaongoza Afrika ya Mashariki lipo Nairobi.
    -----------------------------------
    1.DAR ES SALAAM:
    SIFA
    -Kiuchumi na Kibiashara inayo nafasi nzuri zaidi ingawa imezidiwa na Nairobi, masoko ya Hisa yana tija zaidi kwa wawekezaji kuliko Nairobi kuliko imarika zaidi (Mfano Soko la Hisa Dar mwaka 2011 limeshinda World Finance Award ktk most performing Stock Market of the Region).

    -Mfanya Biashara ktk Eneo la Afrika ya Mashariki na Kati anapata tija zaidi kama biashara yake itafanyika ktk Mzingo unaohusiha Dar Es Salaam, kuchukua bidhaa Dar au kuleta bidhaa Dar,,,tazama wimbi la watu kutoka hadi nchi za nje ya eneo la EAC Zambia,Malawi,Msumbiji n.k

    -Miundo mbinu Dar bado ipo ktk hatua za kuwekwa mfano mpango wa mabasi yaendayo kasi DART, pia mpango wa Usafiri wa Treni kwa wakazi wa Jiji ungali upo mbioni haujakuwa ktk mwenendo bado, pana mipango mingi endelevu mfano KIGAMBONI CITY upo mbioni ukifuatiwa na Daraja la NSSF.

    -Majengo, wamejitahidi baadhi ya maeneo kiasi.

    -Usalama upo Dar zaidi kuliko Nairobi.

    -Lishe Dar ina vyakula vizuri na kwa bei rahisi kuliko Nairobi.

    -Dar ina unafuu wa kiugumu wa kimaisha zaidi ya Nairobi, ni pagumu, fedha pia ngumu na heka heka, hakuna socil life watu wako mbio mbio sana kufukuzana na maisha wakati Dar watu wanaweza kufanya kazi na kukaa ktk vijiwe wakinywa kahawa na kubishana na maongezi.

    -Starehe, Dar ina Paradiso kuliko Nairobi, ingawa maeneo ya kujivinjari Nairobi ni mengi zaidi ya Dar mfano Club za Usiku za kiwango cha Billicanas ktk Nairobi zipo zaidi ya 50 na nyingi kiingilio ni Free!, lakini tatizo ni FWEZA BIN MAWE!!! kwa wengi wa wakazi wa Jiji la NBI labda wanaostarehe wengi wao ni Wageni wapita njia.

    UPUNGUFU:
    -Miundo mbinu hasa ya majitaka bado kabisa Jijini Dar ukilinganisha na NBI.

    -Foleni za magari ni kali Dar Nairobi ni nafuu kwa kuwa wamejitahidi ktk miundo mbinu, flyovers ingawa baadhi ya maeneo barabara bado mbovu, huku wakitumia Treni kwa Usafiriashaji wakazi Jijini,,,msongamano wa watu ni mkubwa sana Dar kuliko Nairobi.

    -Hali ya maisha ni ngumu,ila niya wastani kuliko NBI.

    -Hali ya makazi ni duni kwa wakazi wengi Jijini Dar ,wengi wangali wanatumia vyoo vya Passport size (visivyo ezekwa),milango ya gunia, huku wakienda Mabafuni kwenda kuoga na ndoo mikononi na makopo ya kuogea!.(na wakitumia muda mwingi kukaa ktk foleni ya kukoga bafuni hasa nyakati za asubuhi),,,wakati Nairobi maeneo mengi Makazi yameboreshwa zaidi huku maeneo machache wakiishi makazi duni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2012

    Mimi ni mkazi wa Dar na huwa natembelea Nairobi mara kwa mara. Ukweli ni kwamba DAr bado sana kimaendeleo, tumezidi kuwa na siasa zisizokuwa na tija. Dar kuchafu mno, vumbi mtindo mmoja, hata hizo lami chache zilizopo hazijulikani kama ni lam, vumbi tu na hazina viwango, barabara nzuri Ali Hassan Mwinyi tu. Nairobi angalau kusafi kidogo na wanajenga super highways za nguvu! Dar tunabebwa na bahari tu; tungekuwa makini Dar ingekuwa bonge la jiji

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2012

    Bado huwezi kulinganisha Dar na Nairobi kwa sasa, ila miaka michache tu ijayo tutawaacha mbali!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2012

    Kuna vitu hata havihitaji kulinganisha. Nairobi is far and well developed beyond Dar Es Salaam. Sio tuu kwa majengo na barabara pia kuna parks, golf courses na mengineyo mengi. Satellite towns zimeendelezwa sehemu zinajitegemea. Tusilinganishe visivyowezekana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2012

    Mdau,
    Swali hilo wapelekee NSSF wanaotaka kujenga jengo la ghorofa 30 Nairobi ili wakupe majibu kwa nini sio Dar es Salaam!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 04, 2012

    Mi naona Nairobi ndio mji mzuri kuliko Dar, angalia mpangilio wa majumba, utaona kuwa kuna nafasi ya kutosha kati ya jumba na jumba,barabara za kutosha, kuna bustani kadhaa katikati ya jiji, kitu ambacho ni nadra kwa Dar. piga picha ya jijini dar namaanisha posta, jiulize kama kuna nafasi ya kutosha kati ya B.Mkapa tower na NBC, NMB n.k.
    Tanzania ina nafasi nzuri ya kutengeneza miji yake kwani mambo mengi ya kimataifa pamoja na biashara kwenda nchi jirani zinaifavor. Arusha kuitwa Geneva of Africa ilikuwa ni nafasi murua ya kutengeneza miji yetu katika mpangilio mzuri. bahati mbaya saaana hawa maafisa mipango miji wanazunguka kwenye viti tu hawaendi uswahilini kuanngalia namna watu wanavyojenga makazi yao, inakuja baada ya miaka 30, utasikia "tunabomoa, umejenga ambapo hapatakiwi" inaingia akilini?
    Sio siri Watanzania 97% hatutekelezi majukum yetu vizuri na kwa wakati.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 04, 2012

    OK HOW MANY SHOPPING PLAZA DAR MNAZO COMPARED TO NAIROBI? NAIROBI WANAZO 8. SUPERMARKET KAMA ZA SHOPRITE WANAZO at least 32 IN NAIROBI.
    OK, HOW MANY ROAD HIGHWAY OR MOTOR WAYS OR FLY OVER MNAZO BONGO?
    nAIROBI THEY ARLEADY HAVE TWO AND THREE TO COME.
    kenyatta airport has more than 10 GATES for arrive/departure. how many dow we have in Dar airport?

    THEY HAVE A nEW CENTRAL BUSINESS DISTRICT (CBD) NA OLD cbd. je sie wabongo tuna CBD ngapi DAR?

    the lists goes on and on....

    lets face it Nairobi is far bigger and better than DAR.

    I live in Nairobi na Na Dar naijua.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 04, 2012

    TOFAUTI:

    NAIROBI:
    -Mji umepangika, majengo ni wingi wa wastani machache hivi (sio utitiri kama Dar) ila ni makubwa na marefu zaidi kuliko ya Dar, pia slums (makazi duni) zipo lakini maeneo machache tena yanayojulikana, mfano kule Mathare n.k.

    -Mji kieneo umejikusanya eneo moja.
    -Barabara zimewekwa pana na eneo la kati la kutosha.
    -Unaweza kuimaliza Nairobi kwa siku moja.
    -Magari ya Usafiri Jijini (Matatu's) yanekwenda kwa mwendo wa mzunguko Jijini,,,hakuna ile nenda rudi, nenda rudi ya Daladala kama Dar,,,aliyoilalamikia Kondakta Mekuu.

    .......... ............
    .......... ............

    DAR ES SALAAM:
    -Mji haujapangika ingawa umejengeka sana kwa wingi wa majengo kuzidi Nairobi, unakuta Gorofa limejengwa lakini limezungukwa na slums , hizo slums (makazi duni) yamelizunguka Jiji zima.

    Mfano ''Bwana Dulla Jeba'' yeye ni Super Star na mtoto wa Mjini mkazi maarufu sana hapa Jijini Dar ambaye ni mjuaji kupita kiasi akiwa Jijini, ukikaa ktk Gorofa moja juu Summit City Centre mfano pale PSPF au PPF Towers unaweza kwa Darubini ya lenzi kali kumshuhudia akiwa amebeba kopo na ndoo ya maji ya kuogea tokea anatoka nyumba kubwa hadi anafika maliwatoni mpaka akijisaidia au akikoga ktk choo cha ''pasipoti size'' huko kwake Keko Machungwa!

    Kitu ambacho Nairobi ni maeneo machache sana (yanahesabika) yenye maisha kama hayo ya Dulla Jeba wa Dar!

    -Mji kieneo umesambaa kote, huku maeneo mengi yakiwa ni Makazi duni au holela.
    -Barabara ni nyembamba na eneo la kati sio la kutosha kati...labda hizi za mpango Mpya wa miundombinu.
    -Huwezi kuimaliza Dar kwa siku moja.
    -Magari ya Usafiri Jijini (Daladala) yanekwenda nenda rudi,,,kama aliyoilalamikia Kondakta Mekuu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 04, 2012

    Una compare aple and pears dear. Wenzetu wako juu kama dege la Obama. Kalagabhao

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 04, 2012

    BONGO DASLAAM BADO KABISA KWA NBI !

    Mdau Anonymous wa Wed Jul 04, 01:52:00 PM 2012

    Hahahaha niache nicheke kwanza,!!!

    Huyo jamaa ''Dulla Jeba'' makazi yake sio Keko Machungwa yeye ni mtoto wa Mjini na Mkazi wa Ilala Shariff Shamba kwa Maalwatan na Wajanja wa Jiji!

    Sasa ili na sisi tuweze kung'oka kwenye tope tutajinasaba angalau na Nairobi inatakiwa tufanye hivi:

    1.Tujitahidi kuzibia mifereji hasa ile ya katikati ya Jiji inayokera kitu ambacho huwezi kuona katikati ya Nairobi, sio siri wao wamejitahidi kwa hilo,,,mifereji ipo lakini hukoooo pembeni.

    2.Tuwe na hadhi ya mpangilio wa Makazi, watu kama akina Dulla Jeba wa Ilala Shariff Shamba wanatakiwa wahamie Kisarawe mashambai ili waweze kutumia vyoo vyao vya Pasipoti size badala ya kuchanganyika na wenye majengo ya magorofa Mjini.

    Hatukatai uchafu hata majiji makuu duniani upo, lakini sio city centre!!!

    Nairobi inazingatia usafi kati kati ya Jiji wako makini sana tofauti na Dar !

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 04, 2012

    OK, tumejitahidi isipokuwa tatizo lipo kwenye viwango kwa kweli havikuzingatiwa hasa kule kwenye uyoga wa vikwangua anga Kariakoo!

    Jamaa wameijenga Kariakoo kiswahili sana kupita maelezo!

    Mitaro inazibuka ovyo Kariakoo, majengo mengine mapya mabomba ya maji safi yanaingiliana na mabomba ya maji taka!

    Mengi ya majengo ya Karoakoo, wakazi walio makini wanaishi standby wakiwa na miamvuli au parachute za kujiokolea kama wasafiri wa Ndege angani!,,,ni vile muda wowote majengo yanaporomoka.

    Ujenzi wa majengo mengi Kariakoo haukuzingatia viwango na sifa, Kandarasi nyingi ni zile za JITUME CONSTRUCTION LTD. pamoja na WAKWETU CONTRACTORS CO.LTD. ,ambazo unakuta mfuko mmoja wa simenti badala ya toifali 15 hadi 20 wanafyatua tofali 100 hadi 200 !

    Kwa mtaji huo utafananisha majengo ya Dar na Nairobi???

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 04, 2012

    wadau naomba mtupe taarifa sahihi

    je ni jengo gani katika africa mashariki imejengwa kwa hela nyingi zaidi,

    je ni jengo gani lina urefu/ghorofa nyingi

    je ni mji upi unaongoza kwa kuwa ujenzi, majengo mengi yana jengwa kwa mwaka

    fanyeni research halafu mtapata jibu wenyewe, msitowe maoni bila ya kufanya uchunguzi au kwa kutazama kijisehemu kidogo cha picha

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 04, 2012

    kama mnaongea East Africa naona mmesahau Kigali Rwanda..one of the best and cleanest of all na unajengwa kwa utaratibu unaoeleweka

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 04, 2012

    Nairobi pameendelea zaidi kuliko Dar kwa namna nyingi sana. Ila kwa upande wa umiliki wa mali, mali nyingi Dar zinamilikiwa na wananchi wakati Nairobi mali nyingi ni za wageni na ni wananchi wachache sana wanamiliki mali. Mfano mzuri ni majengo. Unaposifia magorofa ya Nairobi pia ukumbuke kuwa si ya kwao. Haya magorofa machache na mafupi mafupi ya Dar ni ya kwetu wenyewe.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 04, 2012

    Mdau wa hapo juu usinichekeshe. Ya kwenu wewe na nani? Kusema kwamba mali inamilikiwa na wenyeji ni changa la macho tu... swala tujiulize mwenyeji hasa ni nani? Ndugu wa mheshimiwa au mlalahoi... ukweli ni kwamba kama ilivyo Nairobi na Dar mwenye hela yake ndiye mwenye mji wengine wote ni vitega uchumi iwe Nairobi au Dar...

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 04, 2012

    Huwezi linganisha DAR na Nairobi, kuanzia miundo mbinu na utaratibu wa mji. Ni sawa na kulinganisha Marekani na Tanzania. Nairobi ipo mbali sana.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 04, 2012

    Mdau bado anatafuta maeneo ya kulinganisha na Nairobi. Labda tusubiri kwa sasa Nairobi bado ni Bab K. kwa Dar.

    ReplyDelete
  25. hebu kueni na akili
    dar ya leo sio ile ya 80s...mambo yamebadilika sana tena sana dar ina majengo mengi sana na tena ya kisasa kuliko nairobi hata ukiringanisha ukubwa wa city nairobi inaingia mara mbili na robo kwa dar..so tuongee tukiwa na evidence na uhakika...alaf kingine dar inamzunguko mkubwa wa kibiashara...kingine tanzania inaongoza kwa watalii kuliko kenya ambapo wamefika 3million per year..kingine tanzania kuna bus rapid system ambapo nairobi hakuna...dar ina population kubwa na pia ina sehemu nyingi za starehe ambazo nairobi hakuna

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...