Matawi ya Miti yamepunguzwa,sana hii ni nzuri,lakini badala ya kuondolewa kwenda kutupwa katika sehemu inayostahili, inakusanywa hapo hapo na kuachwa. Huu ni uchafu kwa kweli....hapo ni usoni mwa Ubalozi wa Ufaransa,Kinondoni.

By Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hapana mdau huo siyo uchafu, bali ni karaha tuu kwa waendesha magari. Miti na majani haiwezi kuwa uchafu. Kinachonishangaza ni kwanini katika nchi ambayo nishati ni adimu kwanini akina mama ntilie bado hawajachangamkia kuni hizo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    kwa kweli hii sio sahii,maana uchafu unaonekana vibaya sana. tena hilo eneo lenyewe linaonekana ni karibna eneo fulani nyeti sana.
    kwa wenzetu nchi zilizo endelea wana mashine ambaazo matawi kama hayo anasagwa(shreader) na kutumika kama mbolea ya kuwekwa hata ktk miti yenyewe au bustani nnyingine (mulch)hata bongo inawezekana,sido mko wapi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    Inaweza hata kusababisha excedent pumba city cancel go to hell nyinyi watu mnakula pesa tu kila siku tu jiji mnajuwa kuwamwagia wamachinga biashara zao tu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    PRUNING YENYEWE NI UHARIBIFU.HII KAZI INAHITAJI WATAALAMU

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    hapana wadau huo si uchafu, bali ni mbolea

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    Tazama baada ya kuipunguza matawi ilivyokuwa mibaya. Sehemu hiyo (ama kote penye nafasi kama hiyo katika barabara zetu) panahitaji miti iliyochanua vizuri. Tatizo jamaa wanapanda miti yoyote tu badala ya miti maalum ambayo haihitaji kubaki hovyo namna hii hata ikipunguzwa matawi.Ni ukatuni tu kila kona.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2012

    Hiyo ni mbolea sio uchafu. Organic manure which safe and environmental friendly.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2012

    Uchafu ni kitu chochote kilicho mahali ambapo si pake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...