Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, Mfuko wa hifadhi ya jamii ni mfumo ambao jamii husika imejiwekea kwa lengo la kuwakinga watumishi wa umma au binafsi (waajiriwa) dhidi ya matukio yasiyotarajiwa (Contingencies). Matukio hayo ni kama maradhi, ulemavu, kupoteza kazi, kuacha kazi kwa sababu ya uzee (kustaafu) aidha kwa hiari au kwa lazima, na mengineyo ikiwamo huduma za matibabu, ghalama za msiba ikiwa mteja atafariki au kufiwa na mtu ambaye mfuko husika huchangia. Vile vile iwapo mteja atafariki kabla ya kustaafu basi mafao yake hulipwa kwa warithi wake ambavyo huweza kusaidia kusomesha watoto wa mhusika.
Hifadhi kutoka kwa jamii ni haki ya kila mtu kama ilivyotajwa na katiba ya jamhuri ya Muungao wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) katika ibara ya 11, ibara ndogo ya (1) kwamba:
“Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekerezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kupata elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi...”
Hivyo hivyo, ndivyo inavyotaja ibara ya 22 ya Tamko la Ulimwengu la haki za Binadamu la mwaka 1948, ambayo pia inataja kuwa ni haki kwa kila mtu kupata hifadhi ya kijamii kupitia utaratibu uliowekwa.
KWA NINI KUNA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII?
Kujibu swali hilo na
Umandika vizuri. Itume makala yako ssra ili tuweze kuitumia kuelimisha wengine. Tafuta contact za ssra kwenye tovuti
ReplyDeleteTanzania hakuna mazingira hayo tunataka pesa zetu mara tufukuzwapo na wahindi
ReplyDeletewewe wewe wewe ishia huko huko hujui kazi wengine tunafanya kwa mipango ya muda mfupi
ReplyDeleteHAKUNA MTU ASIEJUA ULICHOZUNGUMZA, MIE BINAFSI NIPO TAYARI KUCHANGIA HATA MIAKA 70 WAONGEZE LAKINI POINT HAPA JE UKIACHA KAZI AU MKATABA WAKO UMEISHA AT THE AGE OF 30 AU VYOVYOTE VILE KABLA YA KUFIKA MIAKA HIYO UTAISHI VIPI, TUNATAMBUA KWAMBA MWANZO ILIKUWA ENDAPO HUJAPATA KAZI KIPINDI CHA MIEZI 6 UNARUHUSIWA KUCHUKUA MAFAO YAKO, JIWEKE KAMA WEWE NDIO LIMEKUKUTA HILI UMEFANYA KAZI MIAKA 10 ALAFU SALIO LAKO KTK MFUKO WA JAMII LINASOMA MILLION 20 ALAFU MKATABA WAKO UMEISHA NA UMEKAA URAIANI MIAKA 2 BILA KAZI NA HAPO UNA MIAKA 30 UTAJISIKIAJE HASA UKIZINGATIA KAZI KATIKA SEKTA BINAFSI MTU ANATUMIKA MPAKA MUDA WA KUANZISHA SHUGHULI ZA KIUCHUMI HANA HIVYO KAZI IKIKATIKA MAANA YAKE ANAKULA SALIO MPAKA LINAISHA(UKIJIBU HILI NADHANI UTAELEWA KWANINI WATU WANAPINGA). KILA MTU ANA MALENGO YAKE NA TUMESHAONA WAZEE WENGI WAMEPEWA MPAKA 100 MILLION MWISHO WA SIKU WAKAZIMALIZIA KUJENGEA NA KUNUNUA MAGARI, KAMA ULISHINDWA KUJENGA AU KUNUNUA GARI KIPINDI CHA UJANA WAKO UNADHANI UZEENI NDIO UTAWEZA?
ReplyDeleteUtaratibu uliotangazwa na SSRA ndio hasa ambao unahitajika kufuatwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo inalenga kupunguza makali ya maisha kwa mtumishi pale anapostaafu kwa kuwa uwezo wake wa kufanya kazi unakuwa umepungua. Na huu ni utaratibu unaotumika sehemu nyingi duniani hata ukiangalia nchi zetu za jirani , Kenya, Rwanda na Burundi wanafuata hivyo.
ReplyDeleteKwa hapa Tanzania, suala hili huenda sasa lingekuwa limezoeleka iwapo kungekuwa na msimamo kwa upande wa Viongozi kwani mnamo mwaka 1997, NPF ilibadilishwa na kuwa NSSF kwa lengo la kuleta mafao yaliyobora na yatakayomuwezesha mtumishi kulipwa pensheni mpaka mwisho wa uhai wake. Mojawapo ya vigezo ilikuwa ni kuacha kulipa mafao ya kujitoa ( withdrawal) ambayo yanalalamikiwa kwa sasa. NSSF ilijaribu kutekeleza suala hilo, ila kwa shinikizo la wabunge ilishindwa kutekeleza ingawa kisheria wanafanya hivyo kinyume na makosa na sasa wamejikuta wanaendesha mifumo miwili tofauti.
Kutokana na uwepo wa SSRA nadhani ni vema wakilisimamia hili mpaka mwisho wake kwani watu watakuja kuzoea tu. Changamoto iliyopo ni kuwa kila jambo lina wakati wake, fedha za kwa ajili ya uzee zitumike wakati huo na kwa sasa hoja ya kwamba watu wanaachishwa kazi na kukosa cha kufanya ni kuwa hilo ni changamoto kwa serikali na sisi wenyewe wananchi kuhusu nini cha kufanya wakati tuna nguvu zetu na ajira zipo. Ni vema kuwepo na Taasisi ambazo zitaweza kuwafanya watu wapate mitaji pndi wanapofikwa na janga la kukosa kazi na Seriakli kwa kiasi kikubwa awe ni guarantor, vilevile wakati umefika sasa wanachi tuwe na chachu za ujasiriamali kwa maana ya kwamba hata tunapokuwa kazini pia tuwe na njia nyingine ya vipato. Ikumbukwe asilimia inayolamikia kuhusu kusitishwa kwa suala hili ni asilimia 1% wakati kuna maelfu ambao hawajashirikishwa kwa njia moja au nyingine. Nawaasa wafanyakazi wenzangu tuchukulie hilo kuwa ni changamoto kwetu na kuweza kuwa na njia mbadala wa kuyakabili maisha. Tatizo kubwa sie wafanyakazi ni kuwa kama tumezoea kudekezwa na hivyo kulemaa, tuamke sasa na tuwe na mawazo mbadala badala ya kuleta malalamiko yasiyo na maana. Wengine wameweza kwa nini sisi tushindwe. Nawaasa pia SSRA kuendelea kuteteta uamuzi wake kwani tutakuja ona faida zake siku za usoni
Kwetu hapa sasa pesa za wafanyakazi ndo source ya pesa inayoweza kufukiwa kwa urahisi na serikali kwa miradi mbalimbali;nyumba za polisi,hosteli za wanafunzi,vyuo,bunge,umeme nk wakati huohuo wakuu wanatoa misamaa mikubwa ya kodi kwa wezi wa raslimari za nchi: gesi, dhahabu tanzanite,zikichotwa kama hazina mwenyewe na kila mwaka mkaguzi mkuu wa serikali anaonyesha madudu ya upotevu.Swali hadi sasa mamilioni yangu nyie NSSF mmenisaidiaje wakati mnafungua shampain na kujivunia mafanikio ya kuzungusha pesa zangu.
ReplyDeleteNyinyi mnaongea tu hamjui watu tunahanya kiasi gani,sisi tunahitaji pesa zetu kama tulivoingia mkataba nao kwamba tukimaliza au kufutwa kazi tunapewa chetu hizo habari zingine hatuzitambui sisi na hatuko tayari kufanywa watumwa ndani ya nchi yetu hii dhuluma tena kubwa,acheni utani kwenye jasho la watu tafadhli
ReplyDeletewewe anony unaeetea uozo hapo juu akili kweli huna, hapa tunataka mafao yetu anytime sababu usimamizi wake ni mchafuuuuuu! wanazitafuna hizo hela, wanawekeza ktk biashara kubwa kabisa kwa faida ya nani? wanajilipa bunus za kufa mtu je mi mwanachama vipi? so sie mishumaa au? acheni hizo bwana, ikumbukwe watz hawana fedha mishahara bado mididogo sana, otherwise tuue hiyo mifuko as ndo mabakuli , wanafanya kazi gani si kama tra tu? kukusanya usipopanda?
ReplyDeletekwangu mimi maisha yangu ni haya ninayoishi sasa nikiwa na nguvu zangu.Maisha ya miaka 30 ijayo nitayaandaa mimi mwenyewe. Nasisitiza tupeni hela zetu tujiandalie wenyewe maisha yetu ya uzeeni. Mbona hao wabunge wenu wanachukua hela zao pindi tu wanapoacha ubunge?. Mpaka sasa nina milioni 40 kwenye mfuko mmojawapo lakini bado napanga nyumba nalipa kodi kila mwaka. Hui mfuko hauwezi hata kunikopesha nijenge nyumba.Nahitaji kulipa ada za watoto wangu sasa hivi na sio baada ya miaka 30. Swala la matumizi ya hiyi pesa ni la mtu binafsi. Hizo definition zenu za maana na purpose ya pension to is irrelevant. Sijawahi kuandamana lakini kwa hili nitaandamana.
ReplyDeleteKalekwaa
Tena wapuuzi mbona hawakupita kwenye makampuni binafsi na kushuhudia ubaguzi wa rangi unavyoendelea sina mpango wa kuajiriwa mika yote nataka pesa zangu , nilishaona salia ni 15M Zitanitosha sana kuanzia
ReplyDeleteWE TUNATAKA HELA ZETU. SISI TUNAFAIDIKAJE NA HIYO HELA WANGEKUA WANATOA HATA MIKOPO TUNGEWAELEWA LAKINI HATA UKIWEKA SH. KUMI LEO UTAJA LIPWA HIYO HIYO MIAKA 55 IJAYO WAKATI WAO IMEWAZALISHIA HATUTAKI NAHITAJI NINAPO ACHA KAZI NIPATE HELA YANGU NIJUE NINI CHA KUFANYA. SASA KAMA NAACHISHWA KAZI HARAFU NIJE NIICHUKUE BAADA YA MIAKA 55 HAIINGII AKILINI. WAKATI TUNASUBIRI HIYO MIAKA HAMSINI BASI WATUPE MIKOPO ILI NASI TUNUFAIKE.
ReplyDeleteNashukuru sana mtoa hoja ya haja. Nusura nilainike kwa maelezo yako lakini ulivyohiyimisha tu nikashtuka. Mimi naona nia na madhumuni ya sheria ya kuanzishwa kwa mifuko hii ni nzuri ili tusipoteze nguvu kazi mapema kwa sababu ya "frustrations" za kustaafu . Lakini hatuoni kuwa kuna haja ya kumuokoa huyu mfanya kazi ambaye kafukuzwa kazi na yuko mtaani na watoto wanasoma na hana nyumba!!! ina maana sifa za kuokoa mtu huyu katika jukumu la kusomesha na kujenga nyumba mpaka awe amefikia karibu ya kufa???? tafsiri za dictionary zisitutishe sana maana tumeziandika wenyewe (Kinyago umekichonga mwenyewe halafu kinakutisha-Mzee Yusuph). Malamiko haya usiyashangae ndiyo yatakayobadilisha tafsiri ya pensheni. Wewe kwa sababu ni mwanafunzi na hapo unajua ukibadilisha chochote lazima utafeli na hutapata degree yako hivyo lazima uyaache kama yalivyo ni tofauti na mfanya kazi ambaye "keshaingia ndani ya ngoma" sasa ndio anajua mshindo wake. Bwana elimu yako uliyotoa hapa ni ya muhimu kujua maana ya mifuko hii lakini haiwafungi wananchi kulalamika maana sheria zinabadilishwa kila siku baada ya kupitwa na wakati. Na ndio maana sasa tuna tume ya warioba inafanyia kazi mambo hayo. Utasema ohhh shirika la kazi duniadi limesema...limesema...!! shirika la kazi duniani ndio sisi, tuna wawakilishi huko watasema watanzania wanasemaje kuhusu mifuko hii. Namalizia kwa kusema kuwa mifuko ni ya muhimu lakini wigo wa vigezo upanuliwe kulingana na washika dau watakavyopendekeza. Kuomba pesa yako uliyokatwa kwenye mshahara wako sio jinai. Ni suala linalojadilika. Kwa kumalizia , wafanya kazi wasishinikizwe kujiunga na mifuko hii, na hili litasaidia kupunguza malalamiko maana mtu atakuwa amejiunga huku akiwa anajua vema sheria na taratibu za mifuko husika.
ReplyDelete