Na Jackline Swai, Arusha.

JESHI la polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani kimeanzisha operation maalumu ya kukagua madereva ambao hawana leseni mpya za udereva pamoja na vyeti vya kuonyesha vyuo vya udereva walivyosoma.

Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika kuwa asilimia kubwa ya madereva wana leseni mpya ambazo ni feki na wamezipata kwa njia ya panya bila kupitia shule mbalimbali za udereva na kupatiwa vyeti vya kuhitimu masomo hayo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoani Arusha,(RTO) ,Marison Mwakyembe wakati akizungumza ofisini kwake kuhusiana na hali halisi iliyo hivi sasa na kuwepo kwa wimbi kubwa sana la leseni feki zinazotolewa kwa madereva katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa, walianzisha operation hiyo july 4 mwaka huu ambapo hadi sasa hivi wameweza kukamata jumla ya leseni feki 7 huku madereva wake wakiwa hawana vyeti vya kuhitimu chuo cha udereva , hali ambayo imepelekea jeshi la polisi kuwa makini zaidi kutokana na hali hiyo.

Alifafanua kuwa, operation hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza wimbi kubwa la ajali zinazotokea kila siku kutokana na kutokuwa na madereva wasiojua sheria za barabara kutokana na kutopitia vyuo vya udereva na kupatiwa elimu hiyo.

Alisema kuwa, kufuatia hali hiyo madereva hayo walinyang’anywa leseni hizo feki na walipotakiwa kwenda kuleta cheti cha kuhitimu udereva hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupeleka ,hivyo aliwataka kwenda shule kusoma na kupata vyeti hivyo ndipo waweze kupatiwa leseni zinazohitajika na sio kupitia njia za panya.

Mwakyembe aliongeza kuwa, asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipitia njia za panya kupata leseni hizo ,ambapo wengi wao wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kuanzia 500,000 hadi 600,000 kupitia njia za panya ili kupata leseni mpya, ambapo amewaonya mara moja kuacha tabia hiyo kwani ni hasara kwao pamoja na kuwa na leseni lazima waende shule wakasome na wapate vyeti vya udereva.

‘Mimi nashangaa sana jamani madereva tunawaelimisha kila siku waende shule kusoma na kupewa cheti kwani gharama yenyewe ya kusoma ni 200,000 tu,na wanasoma kwa muda wa wiki mbili tu,lakini wanaishia kudanganywa na watu wa mitaani na kupoteza kiasi kikubwa sana cha fedha bila kujua kuwa wataingia gharama mara mbili, hivyo ni lazima dereva yoyote awe na cheti cha udereva na leseni yake’alisema Mwakyembe.

Alifafanua zaidi kuwa, katika operation hii wanayofanya hivi sasa kila dereva ni lazima aende shule kusoma na kupitia sheria zote za barabarani ,na atatakiwa kutembea na leseni katika gari lake sambamba na cheti chake cha shule aliyosoma , na hii ni ili kudhibiti hali ya leseni mpya feki ambazo zimeenea kwa kasi sana.

Aliongeza kuwa, ni lazima wamiliki wa magari kuhakikisha wanakuwa na sheria zao katika kuwakabithi magari madereva waliosoma na wenye vyeti badala ya kuridhika na leseni ambazo wanakuwa nazo kwani wengi wao wanatumia leseni ambazo ni feki .

Aliongeza kuwa, dereva yoyote ambaye atabainika kutokuwa na cheti na akikutwa na leseni ni lazima aonyeshe na cheti kama hana ananyang’anywa leseni yake na kwenda kuleta cheti au kwenda shule ili kupata leseni iliyo sahihi.

Hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka madereva hayo kufuata kanuni na sheria za barabara kwa kuvaa unifomu, kuwa na leseni na vyeti vyao ikiwa ni pamoja na kutosimamisha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa ili kuweza kufuata sheria na kupunguza ajali mbalimbali za barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kama imefikia wakati tunafikiri watu wanahitaji formal education kwa ajili ya kuendesha gari basi na tuanze ku-introduce elimu mashuleni hasa high school(form 5/6) kwa kuwa wakati huo vijana wengi wanakuwa wamekwishafikisha umri wa miaka 18 na wanaruhusiwa kuendesha kisheria.Vijana hawa wafundishwe sheria za usalama barabarani na mambo mengine ya msingi.Wafanye mitihani na kupewa cheti ambacho watatumia kuonesha wamepata elimu ya udereva kna usalama barabarani kabla ya kufanya mtihani wa kuendesha gari na hatimaye kupewa leseni mara wanapofaulu.

    Kwa watu wenye umri wa miaka kama 25 na kuendelea sidhani kama wanahitaji kwenda darasani hasa.Tutengeneze vitabu ambavyo mtu atasoma kabla ya kuanza kuendesha gari,vitakuwa na sheria za usalama barabarani na mambo ambayo ni msangi dereva anapaswa kufahamu.Watu wajisomee hivi vitabu na tunawape mtihani kupima maarifa.Wakifaulu tunawapa mtihani wa kuendesha gari na kuwapatia leseni.

    Hizi ndo taratibu zilivyo kwa nchi zilizoendelea kwa mfano Marekani.Mimi nafikiri imefika wakati nchi yetu kwenda kujifunza kwenye nchi nyingine.Mambo mengine hayahitaji rocket science ni "ku-copy na ku-paste"...twenda tukaangalie wenzetu wanafanya nini na sisi tuige na kubadilisha mambo machache ili mfumo uendane na mazingira yetu.Otherwise tutaendelea kupiga yowe tu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    Wanatoa wapi hizo leseni feki? Mnataka kutibu dalili za ugonjwa badala ya ugonjwa wenyewe? Na hizo leseni ni feki kweli ama unalitumia hilo neno vibaya? Naamini hizo leseni zinatolewa na polisi, na wala sio feki.

    Mimi siamini kuwa ili niendeshe gari nilipaswa kwenda shule. Sikwenda shule na ni muda mrefu sasa ninaendesha gari bila hitilafu. Hayo ni mambo ya kikoloni, mnataka ku-complicate vitu ambavyo hata sio. Mzazi, ndugu ama rafiki yako anaweza kukufundisha, tosha. Muwakague na hao wanaotoa mafunzo ya udereva kwenye hizo driving schools kubaini kama walienda mafunzoni kwanza.

    Nendeni na wakati, acheni hayo mambo ya kizamani zamani mnatuboa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    Kwa nini wizara isitumie database yake vilivyo waanza kutoa points kama ulaya na kufungia watu hii italeta discipline kidogo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2012

    Wadau naomba kuuliza kama International Driver's Licence inaweza kusaidia kupata Tanzanian Driver's Licence kwa mfumo wa kubadisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2012

    Leseni kuwa Fake siyo kutokuwa original na kutotolewa na polisi. Leseni inaweza kutolewa na Polisi na bado ikawa fake kwavile haikufuata utaratibu unaotakiwa wa kuhakikisha kuwa Dereva ana sifa zinazomruhusu kuwa salama barabarani. Tatizo siyo kuwa na leseni iliyotolewa na mamlaka, tatizo ni kuwa na leseni wakati huna ujuzi wa kuwa barabarani bila kuhatarisha maisha ya watu. Kwamfano, kuna waendesha mabasi na malori wengi ambao hawajawahi kuhudhuria shule, wala kozi ya uendeshaji na wamefundishwa tu na madereva wenzao wakati wao ni ma Otingo, Makondakta...sasa mtu kama huyu hata akipata leseni halali lakini hakufuata utaratibu wa kufundishwa kuendesha ina maana gani? Leseni inaishia kuwa kadi tu ambayo ni "timed-bomb" kwavile huyu mtu kunasiku atasababisha vifo au majeraha mabaya kwa wananchi. Je, mamlaka ya Leseni ina utaratibu gani wa kuhakikisha kuwa kila mwenye leseni amepata elimu ya kuwa barabarani salama? Mdau-CA, USA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    WELL... Kwa mtazamo wangu kwanza hizo zoezi lenyewe mpaka sasa linaonyesha failure kwani tangu Julai 4 hadi sasa wamekamata madereva 7, inaonyesha jinsi gani rushwa ilivyokithiri.
    Kuhusu suala la madereva kuwa na vyeti ili wapate leseni, huo mfumo ungeangalia(sijui kama ndivyo wafanyavyo) umri wa dereva na ana leseni kwa muda gani. Kuna waliopata leseni za miaka ya 60,70, 80 kipindi ambacho details za watu zilikuwa kwenye makaratasi na siyo kwenye kioo.
    Leo umtoe mzee wa miaka 50/60 akae darasani kusomea udereva kwa wiki mbili wakati ameanza kuendesha kabla ya sheria za barabarani hazijawa za kuchanganya kama ilivyo sasa.
    Tatizo huo ni mradi wa mkuu fulani ambaye hana ada ya shule ya mtoto au anataka kufanya harusi ya bintiye/son kwa hiyo anafikiria jinsi ya kuchangisha fedha za kuendesha shughuli hiyo.
    Hiyo inawapa mwanya wenye magwanda meupe kula nyama kila siku huku jioni wakiishia kwenye PUB kushushia ngano baada ya kazi nyepesi ya kushibisha mfuko.
    Sheria za usalama barabarani zinatakiwa zirekebishwe kuanzia ngazi ya juu hadi chini. Leo hii kuna watoto wa wakubwa wanataka kuendesha mashangini ya baba zao, hao leseni wanapata wapi? Hatuwaoni madarasani wala kwenye vijigari vibovu ya mafunzo.(L cars)
    Jamani tusiige tembo kunya mavi makubwa. Amekula vingi na kwa muda mrefu kabla hajayaachia hayo makiligimba mweee. wabongo nyie kila kitu kuiga tuuuuuuuu. Mtapasuka misamba...shwine nyie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...