Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika AU leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili jijini Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo jioni.Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe.Joram Biswaro Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Looking presidential Prez!
ReplyDeleteHivi haiwezekani tukaomba katiba ibadilishwe kidogo tumuongezee raisi muda kidogo hata miaka mingine mitano? Najua waosha vinywa mtakuja na maneno meengi ya kukasirika lakini ukweli utabaki pale pale kwamba JK ni mzalendo wa kweli na anachapa kazi. Katika maraisi waliopita yeye na Mchonga ndo walikuwa na uzalendo wa kweli na nia halisi kwa maendeleo ya taifa letu.
ReplyDeletemdau wa pili hujui kuwa nchi iko kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba? Hujui pia kuwa sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba imemkabidhi rungu kwenye haya marekebisho? Ashindwe mwwenyewe tu.
ReplyDelete