MNARA WA KUMBUKUMBU ZA MASHUJAA WA VITA VYA MAJI MAJI ULIOPO KATIKA KIJIJI CHA NANDETE KILWA...HAPO NDIPO AMBAPO VITA HIVYO VILIANZIA
MKUU WA MKOA WA LINDI LUDOVICK MWANANZILA AKISOMA MAELEZO MBALIMBALI YA HISTORIA YA VITA VYA MAJIMAJI ...AWALI ALIWEKA MSHALE KUASHIRIA KUWAKUMBUKA MASHUJAA HAO KATIKA KUENZI HISTORIA HIYO MKOA WA LINDI ULIKUMBUKA HISTORIA HIYO KWA KUADHIMISHA SIKU HIYO KIMKOA KATIKA ENEO HILO MUHIMU
MKUU WA MKOA WA LINDI AKIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WALIOFIKA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBU KUMBU ZA MASHUJAA KATIKA MNARA WA VITA VYA MAJIMAJI SEHEMU AMBAYO VITA HIVYO VILIANZIA KATIKA KIJIJI CHA NANDETE-KIPATIMU WILAYANI KILWA
VITA VYA MAJI MAJI VILIISHA TAREHE 08 AUG 1907 WASHINDI WAKIWA WATAWALA WA KIKOLONI WA KIJERUMANI NA HUKU WAKIACHA MAELFU YA MAITI YA WAPIGANAJI NA WENGINE WALIOSALIMIKA WAKITESEKA KWA NJAA KATIKA MAENEO YOTE YA VITA HIVYO NA HUU IKAWA MWANZO WA HARAKATI ZA UKOMBOZI KUFUATIA VITA HIVYO KUUNGANISHA MAKABILA MBALIMBALI NA KUDAI UHURU. PICHA ZOTE NA ABDULAZIZ VIDEO.


Licha ya kuchoma mashamba ili wazalendo wafe kwa njaa, wakoloni wa kijerumani walichoma misikiti kwa madai kuwa walikuwa wanawafunza Waislamu fundisho ili wasirudie kupigania uhuru. Zaidi ya 60% ya wapiganaji wazalendo walikuwa ni Waislamu mmojawapo aikwa babu wa babu ya rafiki yangu.
ReplyDeleteWee mdau hebu toa mambo ya udini, wengine, dini si imani ya mtu tu, mimi babu yangu alikuwa mkristo akwa mwislamu, miaka hiyoo, enzi za utawala wa wajerumani, alikua anatokea kilwa, kwa hiyo ni great great grand pa, sisi sote ni watanzania, tuendeleze nchi yetu kwa amani na upendo, kati ya hapa majina mengi yaliyojaa ni yale ya asili, asili ya kiafrica, kitanzania, ambayo ayafungamani na dini yoyote bali yanatambulisha uafrica wetu
ReplyDeleteKinjekitile Ngwale jina la kwanza aliitwa Ali !
ReplyDelete