Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi  huu unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari  na kuleta mkanganyiko  miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Kufuatia hali hiyo Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:

  • Marekebisho  kuhusu  kusitisha fao la kujitoa  yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni 
  • kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni.
  • Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka  vyama vya wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali. 
  • Kwa kutambua  tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti ya  sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa 
  • Mwanachama  kunufaika na michango yake wakati angali katika  ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya  wanachama. Miongozo na  kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo  wafanyakazi, waajiri na Serikali kabla ya kuanza  kutumika.
  • Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya  kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa wadau. 
  • Tangazo hili halitowahusu wanachama waliojitoa kabla ya  tarehe 20/07/2012.
  • Mamlaka inakanusha vikali kwamba  sitisho la fao la kujitoa si  kwasababu za kiserikali au kwasababu mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na  michango yote ya wanachama ipo salama.
  • Hivyo, Mamlaka inawaomba wanachama na wadau wote wa  sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea  kwa lengo ya kulinda na kutetea maslahi ya mwanachama 

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji
SSRA-Makao Makuu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2012

    Kwanini hamkutoa haya maelezo wakati mnajadili kubadilisha hii sheria?? Hii tabia ya kubadilisha sheria muhimu bila kutuambia cc wenye nchi itaisha lini?? Mnasema mlijadili bunge la April ,lakini mbona hatukusikia kuhusu hili?? Hakuna hata gazeti/radio/tv walioelezea hii kitu mpaka imepitishwa?? Arghh...yaani maelezo yanatolewa baada ya rais kutia sign?? Kweli mnatuona cc wajinga.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2012

    Hiyo Miongozo HATUITAKI.. Mtushirikishe kwenye Miongozo wakati wa KUTUNGA sheria ambayo inatuhusu sisi wenyewe wafanyakazi Hamkutushirikisha why NOW matake kutushirikisha kwenye MIONGOZO? Non Sense kabisa, Hivi wewe mtu amefanya kazi miezi mitatu na kibarua kikaisha na mtu alikuwa analipwa 120,000 Hiyo NSSF yake unajua ni how Much?mpka aisubirie kwa mpk afike miaka 60 na ajira zenyewe hizi za kubangaiza ambazo serikali inaangalia tu wanapewa wageni wazawa tunaachwa unategemea hizi siku zote anaishi vipi? hiyo sheria nafikiri inaweza fanayakazi serikalini ambako watu huwa hawafukuzwi kazi, Kazi inaisha siku anastaafu akiwa na hiyo miaka 60, sisi wa sekta Binafsi Mnatuonea tu, Vimishara venyewe ndo hivyo vya tia maji tia maji, leo hii nimeachishwa kazi nina Miaka 30 ndo ni wait tena 30 years nipewe Hifadhi yangu KWELI? Are you Serious?Please msiwe kama watoto. Hata hii Mamlaka kweli inawatu wenye HEKIMA na BUSARA kweli?Nahisi ni mradi tu wa Mtu, Hiyo mifuko ya jamii yenyewe inapiga Deal kinoma na Hela zetu lakini hatupewi Share kwenye hiyo Miradi wala Riba!Basi wangekuwa hata wanatudanganyishia kutuwekea mdhamana kwenye Mabenki tuwe twapata Mikopo ya Kununua Nyumba za NHC au hata Kupewa Mikopo, As I know kuwa Hii mifuko ya Jamii ina weka Hela zetu kwenye Mabenki kwa FIX deposit accounts..Tunajua yote wanayofanya tuka kaa Kimya NOW ndio mnataka hata hichi kidogo tusikipate,Please Kuweni Serious.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2012

    si vizuri kuyalazimisha makundi mbalimbali ya wananchi kuichukia serikali yao,jinsi makundi yanavyoongezeka ndivyo hatari ya kuondolewa madarakani inavyoongazeka,wachunguze sana washauri wenu wanakowapeleka siko kabisa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2012

    Sawa, SSRA mnatuambia hili lilijadiliwa Bunge la April, kwa nini sasa mmesitisha wanachama wa mifuko ya jamii kujitoa sasa? Si ingekuwa busara kwa SSRA kukamilisha hiyo miongozo yooote kisha mtoe elimu kwa jamii na wanachama wote; mkawapa wanachama muda wa mwaka mmoja mpaka miwili kuwa kuanzia Julai 1, 2013 utaratibu wa mifuko ya jamii utakuwa hii?

    Yaani mnakuwa mbumbumbu wa kujali wananchi wanachama ambao ndio wenye fedha zao kwenye hiyo mifuko ya jamii??!! Kwa sababu TU bunge limepitisha basi ndio mmeshapata kiburi na hamkuona tena umuhimu wa kutoa elimu kwa Wanachama!!

    Wafanyakazi 600 wamesha acha kazi migodini kwa sababu ya uzembe wenu. Mnajua matokeo yake? Migodi haitazalisha, Serikali itakosa mapato...Serikali ikikosa mapato hata wale wasio wanachama sasa wataathirika na maamuzi yenu ya kukurupuka.

    Nchi hii!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2012

    Hatudanganyiki eboo!! bora kuwepo na private security fund ilio huru na maamuzi ya serikali tuwe na option ya kuexit mifuko yenu hii ambayo mnakaa na kufanyia maamuzi jasho la wananchi bila kuwahusisha. mmefanya social contributions za watu kama kodi ama ? Maamuzi mliofanya ni magumu sana kwetu kurahisishwa na hio explation yenu rahisi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2012

    Hili halikubaliki kabisaaa. Ni wakati sasa taasisi za umma zikaacha sababu za zamani katika mazingira ya sasa. Ni kweli kuwa huu ni utaratibu wa kunufaisha mfuko kwa kukuza mtaji wake na sio mwanachama. Ajira nyingi ni za mkataba na zile za kudumu zimekuwa sio za kudumu tena. Pia mimi ni muathirika na mifuko hii. Nilikuwa mwanachama wa PPF nilipotoka nililipwa michango yangu na riba kidgo sana na michango ya mwajiri sikupewa na hata mwajiri hakurudishiwa michango yake aliyonichangia. nikajiunga na NSSF nilipotoka nikaliwa michango yote ila riba ikawa ni matatizo na nililazimika kusubiri miezi 6. kwa kweli mifuko hii inanyonya tu na msaada wake ni mdogo na haiendani na hali ya ajira ya sasa isiyoaminika. Mifuko hii inajikinga na waajiri badala ya wafanyakazi wenyewe. sheria itoe uhuru wa mfanyakazi kuingia na kutoka wakati wowote. NI PESA ZAKE NA MAISHA YAKE.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2012

    HATUTAKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2012

    Ahhh!! Huu ni wizi wa mchana!! Hakuna tofauti na kibaka!! Wadau hatukushirikishwa na wala hatukusikia mjadala huu huko Bungeni mwezi April.12 Hii imeandikwa na kupitishwa kinyemela huko serikalini na vikaragosi wake. Sheria hii hatuitaki na lazima iondolewe!! Kwa nini mtuamulie matumizi ya fedha zetu wenyewe?!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2012

    HATUTAKI MANATUGUSA KWENYE VINENA SASA HATUTAKIIII MNAJUTENGEA MAZINGIRA GANI UJANANI MPAKA MTUJALI UZEENI HATUTAKIIIIII MSICHEZE NA JASHO LA WANYONGE KWANI LAZIMA KUAJIRIWA MIAKA YAKO YOTE YA MAISHA WAPUUZI NINI HATUTAKIIIIII

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2012

    NARUDIA TENA HATUTAKIIII MSILETE ZA KULETA HUKO HATUTAKIIIIIIIII HIVI JAMANI MAANDAMANO LINI ??

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2012

    nAFANYA KAZI KWA MKATABA ...HAYO MAMBO WAPENI WATU WA SERIKALINI WENYE UHAKIKA WA AJIRA SISI MTUACHE HATUTAKIIII HAMJUI TUNAFANYISHWAJE KAZIII HATUTAKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2012

    kwa staili hii mimi hata hainiingii akilini....yaani huu ni ubabe tu kwa sababu mmeshika mpini ndio mnafanyahivyooo?? ila mkumbuke hata mpini huwa unavunjika wakati wakukata...there is always another side of the coin...
    MASWALI???
    -HIVI NANI KAWAMBIA ANATAKA MIKOPO YENU.
    - MNAFIKIRI KILA MTU ANASHIDA YA NYUMBA???
    -SERIKALI INASHAURI WATU TUWE WAJASIRILIA MALI...NA ASILIMIA KUBWA YA WAFANYAKAZI WENGI TUNATAFUTA MITAJI TU HUMU..THN TUWEZE KUJIAJILI...SASA KWA MPANGO WENU HUU WAKUTUKABA KWEUPEEE MNAFIKIRIA MALENGO YA UJASIRILIA MALI UTAFIKIWAAAA..???
    -YAANI HUU NI WIZI MTUPU..
    mfano: umenipa hela yako nikushikie kwa muda fulani, halafu ukija kabla ya muda nasema ukope...!!! laa sivyo nisubiri hadi miaka 55 au 60 hivi utanielewa kweli???? HEBU FIKIRIA TU MWENYEWE HATA UKIMSHIRIKISHA MWANAO WA SHULE YA MSINGI KUHUSU HILI ATAJUA NI DHULUMA TU...
    -KITU AMBACHO KINACHO NIACHA HOOI KULIKO VYOTE ETI SSRA MNADAI Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.HIVI MLISHINDWAJE KUJADILIANA NA WAHUSIKA KABLA HAUJA SAINIWA....!!!PESA ZANGU MWENYEWE NA NINAHAKI YA KUZIPATA PALE NINAPO ZIHITAJI...

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 26, 2012

    Dam them all waliopitisha sheria hii coz hawajui wananchi wao wanaishi vipi.....wamekopeshana hela zetu wanashindwa namna ya kuzirudisha in a short run ...ndio maana mnapanga mipango yenu ya long run...we are seriously bored and am telling you the truth your disturbing the peace we had. hawa SSRA ndio kwanza wachanga then they are telling us this upuuzi....yaani unatoa sheria then baadae ndio unatoa mwongozo for what!!! while the law is there... very stupid! I know you forced to implement things kimaslahi zaidi ndio sababu mko hapo mlipo na misimamo yenu. but its ok! all the best with you fake mwongozi read it by your own.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 26, 2012

    kweli waliotunga hii sheria na walioipitisha wanatumia vichwa kufuga nywele,patachimbika na mtatengua tu haya maamuzi hakyanani msituletee upuuzi wenu hapa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 26, 2012

    Hatutakiiiii kwani maandamano lini?? kama mngetoa hata miezi sita kuwa sheria hii itaanza tengeacha kazi ili tuchukue mafao yetu.mnatudhulumu kikuvu kwa sababu mmeshikilia dola huu ni wizi tena wizi wa nguvu ,wizi wa utake usitake

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 26, 2012

    This is ridiculous! Vijana wa sasa tunaisha leo siyo kesho. Wengi hutuna mpango wa kufanya kazi za kuajiriwa hadi kustaafu bali tunatafuta mitaji tujiari. Hivi serikali inapopiga kelele watu wajiari bila kuwapa mitaji wanategema nini?Sisi wengine tunategemea michango yetu iwe mitaji mambo ya kufikisha miaka 60 ni mawazo mufilisi kabisa na haikubaliki! Kama serikali inajali wastaafu ingeonesha mfanoi kwa wazee wa Africa masharika wanaopuliziwa maji ya kuwasha kila siku. Kwa hili serikali ya CCM iwe makini kama inataka kuendelea kututawala. Hivi inawezekana kukopeshwa nyumba ya m.60 au 80 wakati umechangia m. 10 au 15 tu? Kwa waleo wanaocha kazi na kujiunga na mashirika ya kimataifa yenye mifumo yao ya pension kama UN, AfDB na mengineyo inakuwaje? Hii SSRA naona inajitahidi kuiondoa CCM madarakani!!! Kwa hili wafanyakazi tupo pamoja!!!!! Acheni kupima kina cha maji kwa maji kwa miguu yote!!! Patachimbika!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 26, 2012

    NAFIKIRI WAAJIRIWA WA HII MIFUKO WAMELEWA NA MIKOPO MIKUBWA WANAYOKOPESHANA KWA KUTUMIA PESA ZETU KUPITIA HII MIFUKO NA HAWANA SHIDA NDOGO NDOGO WALA SHIDA ZA MITAJI... AU MNAFIKIRI HATUJUI?!... KUMBUKENI WENGINE HATUFAIDIKI... MIMI NAOMBA MTUPE MWEZI MMOJA TU ILI KWA AMBAO WANATAKA KUENDELEA KWA HUU UTARATIBU WENU WABAKIE KWENYE MIFUKO NA WASIOTAKA WATOKE HALAFU MUONE.... NDIO MTAJUA KAMA KWELI KULIKUWA KUNA USHIRIKISHWAJI KWENYE HAYA MAAMUZI.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 26, 2012

    Kwa mtu mwenye akili wala hakupaswa kuja na ajenda ya kusema miongozo inakuja.Uliona wapi sheria ipite bila kupata maoni ya wanachama halafu miongozo ndo ikajadiliwa! Watu wanalazimishwa kukatwa hela zao na mifuko ambayo kwanza hawaitaki na hawanufaiki nayo halafu mwisho wa siku unalazimishwa tena usichukue mafao yako hadi utimize miaka 55 au 60, hii ni ajabu saana. Imefika wakati sasa kujiunga na hii mifuko ya pensheni iwe ni HIYARI na siyo kulazimishwa. Inakuwaje watu wachache ambao mara nyingi hizi hela wala haziwahusu wawe na sauti na maamuzi tena makubaw mbele ya JASHO la wengine? Tumpeni uhuru wa kujiunga au kujitoa muone kama mtabaki na idadi ya kutosha kama mnafikiri watu wa-mind sana hiyo mifuko yenu! Aaaaah, ina-bore saana!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 26, 2012

    NI WAZI KWAMBA WAHUSIKA WA HII MIFUKO NA VIGOGO WAMELEWA MIKOPO MIKUBWA WANAYOKOPESHANA KUPITIA FEDHA ZETU KUPITIA HII MIFUKO... AU MNAFIKIRI HATUJUI?! TUNAJUA WENZETU MNAAJIRA ZA KUDUMU NA HAMNA SHIDA NDOGO NDOGO WALA SHIDA ZA MITAJI... MNALIPANA VIZURI NA MNAKOPESHANA KUTOKA HUMO HUMO KWENYE PESA ZETU.... CHONDE CHONDE MSISAHAU TU KUWA HILO NI JASHO LA WAFANYAKAZI... NA NI HAKI YAO. HAYA MAAMUZI YENU YANAONYESHA DHAHIRI KWAMBA MNAANZA KUSAHAU MMILIKI HALISI WA HIZO PESA NA KUMPANGIA MAISHA YAKE. EMBU FANYENI JARIBIO LA KUTOA MWEZI MMOJA ILI WATU WANAOTAKA KUBAKI KWENYE MIFUKO KUENDELEA NA HUU MPANGO WENU WABAKIE NA WASIOTAKA WATOKE... NAAMINI MTAPATA PICHA NZURI SANA NI JINSI GANI HAYA MAAMUZI YENU NI SHIRIKISHI!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 26, 2012

    You have killed people's self-employment intention. It was real a source of capital to many - please please undo for good sake

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 26, 2012

    Mimi nilidhani kuundwa kwa SSRA ndiyo kungeleta nafuu kwa wananchi wachangiaji katika hii mifuko ya hifadhi ya jamii kumbe ndiyo imekuja kuongeza maumivu. Bure kabisa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 26, 2012

    Upepo utapita!!! mtapiga kelele mtajipa pressure bure na mambo yatakuwa kama walivoamua! hii ndio Tanzania, ila ipo siku yalotokea Misri na kwengine yatatokea huku kwa jinsi nchi inavoendeshwa kibabe namna hii!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 26, 2012

    SSRA, you have no right to dicide on our money! No way, no way! Don't try to tell the public that memebers don't know how to manage their own money, and you want to assist on behalf. No, a big Nooo! That's not accepted, let everyone decides on his/her own on the best way of handling his/her money. Who are you by the way to play that role. You are not different from other "Mafisadis" we know! Get it clear that "You have no such right to decide on the best way of managing someone's money"!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 26, 2012

    Hakuna logic kabisa ya kumfanya mtu asubiri miaka yote hiyo ndo achukue chake. Kwanza piga picha hii, mfano kama mimi niliajiriwa nikiwa na miaka 19 mpaka nifikishe miaka 55 nitakuwa nimefanya kazi kwa muda wa miaka 36 na kila mwezi nakatwa hela yangu tena nyingi tu na swali la kujiuliza hapa ni "Je nitaishi miaka mingine 36 baada ya kustaafu??" sidhani, sasa kwanini nisipewe pesa yangu nikatumia wakati bado nina uwezo wa kufaidika nayo kuliko kusubiri mpaka nizeeke? na bado nikisha fikia umri huo wa kustaaafu nitapanga foleni mpaka nichoke na nitapigwa kalenda (njoo kesho)mpaka nakufa bila kupata mafao yangu.

    SIKUBALIANI KABISA NA SHERIA HII. hasa kwangu mimi niliye ajiriwa na shirika binafsi. NINA NDOTO ZA KUJITEGEMEA MBELE YA SAFARI KWAHIYO TAFADHALI SANA NATAKA PESA YANGU WAKATI HUU AMBAPO BADO NINA NGUVU YA KUIZALISHA.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 26, 2012

    Tafadhalini SSRA tafuteni njia nzuri yakufanya jamii iwatambue msimguse kipofu watu wanahasira na hali ngumu ya maisha.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 26, 2012

    NYIE ACHENI UJINGA. AVG LIFE YA MTANZANIA NI 45 MPAKA 52 KWA HIYO MIAKA 55 YENU WATU WATAKUFA WATAACHA PESA ZAO. NA HIYO NI DHULUMA KABISA ILA MNATAFUTA MATATIZO MAANA HAYA NI MAISHA YETU MNATAKA KUYACHEZEA. SISI TUTAAMUA LIWALO NA LIWE VILEVILE

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 26, 2012

    Nadhani imefika wakati wa serikali kuruhusu kuanzishwa kwa mifuko binafsina kama wako tayarini vizuri kutujulisha wananchi.Tanzania ya sasa sio ya miaka ya themanini au tisini ni Tanzania mpya, mifuko inayojiendesha binafsi kama hapa UK ni mingi na serikali ikiruhusu tupo tayari kuishauri jinsi ya kuanzisha ambayo wananchi wataruhusiwa kuwa na maamuzi ya kujua wapi wainvest pesa zao za pensheni na kwa wale wasio na utaalamu watashauriwa na washauri sehemu ya kuweka pesa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 26, 2012

    CONTRIBUTION YANGU HADI JUNE 2012 NI 15M, NIMEACHISHWA KAZI JANA, NA SASA NINA MIAKA 35, JE BAADA YA MIAKA 20 HIYO CONTRIBUTION YANGU YA SASA YA 15M ITAKUA NA THAMANI ? KWA KUZINGATIA HII INFLATION ? VERY PAINFULL

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 26, 2012

    Haya mambo ya kuiga kila kitu nchi za mgharibi ndio inatupa shida. wakibadilika kidogo nanyi mnabadilika hamuangalii hali halisi ya ajira kwenu na madhara yake. Kwanza mimi binafsi sioni haja ya kuweka pesa zangu kwenye hiyo mifuko, kwani bank hazipo, si mtu unaweza kuweka standing order kila mwezi pesa yako ikatwe iingie kwenye current account ambayo utaweza kuiaccess kwa muda fulani kuliko kuwatengenezea watu ajira halafu wanakugeuka. Wafanya kazi woote wa mifuko ya jamii wanajigeuza kwenye viti vya kuzunguka, kutwa nzima kwenye viyoyozi, asilimia kubwa ya wachangiaji wanasota na kazi ngumu kila siku. Halafu hao tuliowaajiri wanakuja na agenda ya kucheza na mabosi wao. Tutafuta mifuko yote kila mtu afungue kibubu chake halafu tuone. Huu uamuzi nashawishika kuuweka upande wa upumbavu kabisa.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 26, 2012

    Hiyo mifuko mmeshaonja utamu wake mnavyoweza kujiendeleza na sasa mnataka kuibia wananchi wazi wazi. HUO NI WIZI KABISAAAAAAAAAAAA. Mimi nimeajiriwa na shirika binafsi na ajira zenyewe mnazijua leo unakuja kazini asubuhi unakutana na barua mezani ya kufukuzwa nitakula nini mpk nifikishe hiyo miaka 55? Huo ni uonevu kabisa haswa sisi tulioko mashirika binafsi. Mnatajirisha wazungu wanaokuja mnatusahau sisi?? Haiwezekani!!!!! hapa sasa kuna mnalo tafuta

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 26, 2012

    Halafu nyie mnaiga nchi za wenzenu wakati wananchi wanakufa kwa njaa? Mbona mnaeta hatari nchini? Nchi za wenzetu ajira zao zina security hata ukiacha kazi maisha yanaendelea hapa kwetu kweli bila kazi utaishi? huku ukisubiri ufike 55???? Hii haingii akilini hata kidogo. Msiwe wabinafsi jamani haya maisha mnayotutakia ni magumu sana. angalau tunajipa moyo tukifukuzwa kazi unapata pa kuanzia nyie wenyewe mnajua kazi zilivyongumu kupata leo hii mtu akuambie subiri miaka ya kustaafu huku watoto wangu wakifa njaa

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 26, 2012

    Hizi ni sheria za kidkiteta, unashikilia ela yangu mpaka utakapoamua kunipa,
    Kwanza tunazulumiwa sana shs 10,000 ya leo sio tena sh 10,000 baada ya miaka 10. sasa baada ya muda huo unanipa ela ile ile ya kale eti ndo mafao yako. itasaidia nini wakati thamani yake imeisha. ebu fikirini kwa makini thamani za ela kwa vipindi vya miaka tofauti. wewe unakuwa kama benki kwa muda fulani nikitaka ela yangu toa. this is not real indeed

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 26, 2012

    How much interest is one paid per annum for having his money with the pension funds. Now these pensions funds invest this money with financial institutions at rates that are above t bills. This new law will enable them to stay longer with your money and properly earn that interest until you reach that age of 55/60. Daylight fraud.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 27, 2012

    Michuzi umebania coment yangu kuhusu haya mashirika kuwekeza kwenye mabenki sa faida imewakolea wanatoa sheria ili watajirike, ni dhambi kubwa hata vitabu vya dini vimeandika. manunguniko ya watanzania ni juu yao na Huyo aliyesaini hiyo sheria. Mungu ni mwema ataonyesha njia kwa wanyonge.Wengine wameajiriwa wanahudumia wazazi wao sa kama wakiachishwa kazi, nao wasubiri hayo mafao wakati wazazi wanateseka. Ama kweli Dunia sasa inakoelekea Mungu anajua kwani yanayotokea yanatukumbusha ishara zilizoandikwa katika vitabu vitakatifu. Watu watapenda sana pesa na anasa kuliko vitu vingine.Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake wakumbuke kutenda mema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...