Jiji la Dar es salaam kama lilivyokamatwa leo kwa lensi ya jicho la 
samaki (fish-eye lens) ya 15mm. Katika makala ya Jumapili tutaongelea  kamera na lensi za kuanzia libenbeke na kupiga picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    Maeneo mengine ya Jiji letu ni mazuri sana. Tatizo tu ni kwa walio -design hapo awali walibana sana mitaa kana kwamba Tz tulikuwa na shida ya ardhi. Wangetanua hizo barabara kidoooogo kama mara mbili tu ya hizo kungependeza zaidi. Nasikia miji iliyowahi kutawaliwa na wajerumani haikupangiliwa vizuri kama ile iliyotawaliwa na waingereza.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2012

    Jamani Dar inapendeza kweli kwelii. It is so beautiful as per this picture

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2012

    Mh Michu ndo unarudi toka ukerewe.Naona JK alikuonea huruma ili uoshe macho kwanza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2012

    Kilichobaki Dari Salaama ni kutoa kero hizi kuu tatu(3)au vitu hivi:

    1.Kuhakikisha usafi zaidi Jijini.

    2.Kuleta neema ya angalau mlo mmoja wa Bure wa Mchana wa Msaada kwa wenye njaa,,,ni vile kama mnavyoona Jiji lilivyo zuri na kupendeza wapo wanaochana bata na wapo wenye njaa balaa utawaonea huruma,,,unakuta mtu anatokea Kimara Bonyokwa kwa miguu anaingia mjini asubuhi anashinda na njaa kutwa huku mabosi wakijichana na misosi mikali Mchovu anarudi kapa nyumbani!

    Kila kitu chini ya jua kinawezekana!

    Ni kiasicha kuongea na Wadau Wakuu katikati ya Jiji la Dar kama

    -Misikiti Mikubwa,
    -Makanisa Makubwa,
    -Maofisi ya Ubalozi Jijini na
    -NGO's

    Ili wawe wanafanya Ibada na Huduma ya Kijamii ya kutoa Dishi la bure la mchana kwa masikini Jijini.

    3.Kuilegeza 'Sarafu' angalau iwe laini kidogo kuisaka!

    KWA KUZINGATIA PICHA YA DAR YA JICHO LA SAMAKI NA MAMBO HAYO MATATU (3) DHAHAMA AU KERO KUU KWA WAKAZI WA JIJI INAWEZEKANA DAR IKAGEUKA PARADISO!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2012

    Dar Es Salaam ktk Taswira ya jicho la samaki,

    MAN AND DEVELOPMENT:

    Kama Mdau wa nne (4) hapo juu anavyochangia Anonymous wa Tue Jul 17, 07:12:00 PM 2012, Lengo ni HALI BORA NA USTAWI WA JAMII KWA KUAKISI MAENDELEO YAENDANE NA MUONEKANO WA JIJI LA DAR!

    Kwa huduma za Dishi la bure itakuwa ni mpango mzuri wa manufaa kwa pande zote.

    Watoa huduma Asasi watanufaika kwa kupata GOOD CREDIBILITY na THAWABU, huku akina mama Lishe wasiwe na wasiwasi kuwakosa wateja wa chakula baada ya Mipango ya chakula cha bure kutoka ktk Asasi.

    Kwa kuwa lengo ni hali bora na ustawi wa jamii, Akina mama Lishe wanaweza kushirikishwa kwa kuandaa chakula ili kuwahudumia wakazi wa Jiji kwa Malipo kutoka ktk Asasi.

    KWA MPANGO HUU PANA UWEZEKANO HUU:

    1-JAMII YA WAKAZI WA JIJI WENYE MAHITAJI WAKAFIKIWA KWA UFANISI MKUBWA.

    2-LISHE YA KIWANGO BORA (HYGIENIC/ NUTRITIONIC) IKATOLEWA KWA JAMII.

    3-UWEZESHAJI KWA MAMA LISHE UKAIMARIKA ZAIDI KULIKO BIASHARA WAIFANYAYO AMBAYO HAINA UHAKIKA NA MAUZO YA KUBAHATISHA KWA SIKU.

    4-ASASI ZITAKUWA ZIMEJITUMA VILIVYO KWA KUIHUDUMIA JAMII IPASAVYO.
    KULIKO KUWA NA UTITIRI WA NGO's AMBAZO NYINGI ZIMELAUMIWA KWA UBUTU WA KUJITUMA HUKU KUKIWA NA REKODI MBAYA YA MATUMIZI MABOVU YA RUZUKU.

    HIVYO PANAKUWA NA COMPLETE CIRCLE OF SUSTAINABLE DEVELOPEMNET WITH NURTURING SOCIAL CREDIBILITY ON ONE ROOF.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...