Kaka Michuzi, naomba unisaidie kuuliza wadau huyu Mbu Ni Mbu wa aina gani? Nimemkuta leo nyumbani kwangu asubuhi. Ana kila kitu kinachofanana na mbu ila muundo wake umekaa kimaajabu. Wale wataalamu wa viumbe na wadudu msaada tutani tafadhali
Asante
Mdau Mgori JT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    Zebedayo says. huyu inawezekana ni mbu mwitu, ni mkubwa zaidi ya mbu wa kawaida,mbu wa kubwa kama hawa san sana hupatikana Canada wakati wa kiangazi (summer time) hao wa Canada hawana madhara ila wanauma tu tena sana.Huyo wa kwetu siju,ila tahadhari mdau na alivyomkubwa ,uwezekano upo akabeba hata ukimwi. Ushauri, wewe muweke kwenye kajichupa hivi, toboa juu kitundu cha hewa ,mpeleke Muhimbili-research center, labda tunaweza kupata jibu sahihi,kama labda hiki ni kizazi kipya cha mbu au huyo katumwa ?? Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Ni kweli huyo mbu pia anapatikana majira ya joto katika nchi za scandinavia, huwa hata wakikuuma hawana madhara yoyote.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    Anaitwa Crane fly ,family Tipulidae ,ni harmless na hasababishi magonjwa coz it doesnt bite humans

    Pa1 mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    Must be dragon mosquito. Aitwe Zebediatosis hahahahahaha tehtehteh

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    Huyo katumwa, nakushauri ndugu yangu eidha uende kwa Kakobe au Mwingira akakusafishe. Alternative mjulishe Pro Manyaunyau aje afanye vitu vyake hapo kwako.

    January.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2012

    Nyie mnaosema akikuuma hana madhara napingana nanyi, hasa kwa upande wa Canada. Mbu hawa kwa Canada huwang'ata ndege, na kuna ndege aina fulani (simkumbuki jina) ambaye hubeba virus wanaomdhuru binadamu na wanyama. Sasa endapo mbu aliyemtafuna huyo ndege akikubebena mwanawane ni hoi. Inasemekana kuna watu wameshapoteza maisha kwa kutowahi matibabu wakiamini kuwa hawa mbu ni salama.

    Kwa wanaotaka kujifunza zaidi fungua hii URL:

    http://bodyandhealth.canada.com/channel_condition_info_details.asp?disease_id=288&channel_id=1020&relation_id=70907

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2012

    Mbu hawezi kubeba virus wa ukimwi kutokana na maumbile yake, hivyo sio kweli kusema kuwa anaweza kuambukiza ukimwi.

    ReplyDelete
  8. Maneno GungurugwaJuly 25, 2012

    Wote mmechemsha huyu ni JINI na ametumwa kummaliza huyu jamaa! kwa macho yenu mnamuona ni MBU kumbe ni jini!
    Nakushauri wahi haraka kwa FUNDI aje asafishe nyumba yako.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2012

    Ankali,

    Somo lako la kupiga picha limefanikiwa sana!

    Nimestaajabu kuona jinsi jamaa alivyompata mbu na kumfotoa!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2012

    Kabla ya yote umejuaje kwamba ni mbu? Anaweza akawa ni mdudu tu anafanana na mbu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2012

    Mdau huyu sio mbu,hili ni jini aina ya msukule,haraka sana nenda kwa mtaalam.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2012

    Mdau kaa mkao wa kula, huyo sio mbu na hata hao wanaosema mbu wa Canada wanakupotosha, hicho ni chombo kutoka Zanzibar kinapatikana micheweni, Dole, Sebuleni, Mchambawima hata Mwanakwerekwe a.k.a yake anaitwa POPO BAWA!! So be ready for a party tonight!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2012

    Hivi wewe Mgori mi nakushangaa, unasema mbu wa ajabu.....ni wa ajabu kwako kwasababu wewe ni wakishua. Huku kwetu kunamijimbu noma zaidi ya hako kakwako ulokatuma, unaambiwa mbu wanaushirikiano wameshiba utadhana wanapiga chuma: ukopishana nae unahisi umegongana na kitu, wanauwezo hawa wakuinua jeans wakanyonya mguu, hata ukivaa helment ya pikipiki wanashirikiana kuipiga chini wakupe cha kichwa. Lol!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2012

    kweli bado bado mambumbumbu wa fikira kwa kuendekeza ushirikina, bado tuna safari ndefu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2012

    Acha nicheke tu kuna watu humu wamepinda kweli!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2012

    Kamwone Manyaunyau, na hao wanaopuuza kuwa hakuna majamboozi basi hawaamini biblia au Korani kwani dini zote zimesema kuna ushirikina. Kaa chonjo babake huyo sio mbu wa kawaida. Huku Unguja twawaita popo bawa ati.

    Nahodha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...