Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanza mchakato wa uhakiki wa utayari wa Jamhuri ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya hii. Mchakato huo unaongozwa na matakwa ya kifungu cha ....cha Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Timu ya wataalamu kutoka nchi wanachama pamoja na Sekretariat tayari ipo Juba na leo ilikuwa na kikao na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Prof. Elias Wakson Nyamlel ambaye Liihakishia timu ya wataalamu wa Jumuiya kuwa nchi hii ipo tayari kujiunga na pia kutekeleza matakwa ya mkataba.Pichani ni Mjumbe wa timu moja kutoka Tanzania,Brig Gen Daniel Matiku (wa pili kulia) akijadiliana na baadhi ya viongozi wa nchi ya Sudan Kusini nje ya ukumbi wa mkutano katika hotel ya Aron, jijini Juba.
picha ya pamoja baina na timu ya wataalamu kutoka nchi wanachama wa EAC pamoja na maofisa wa serikali ya sudan kusini wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhes. prof. Eliasi Wakson Nyamlelnje ya ukmbi wa mikutano wa hotel ya Aron jijini Juba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2012

    Sudan ilitaka kujiunga kama sikosei ikakataliwa? hope am not wrong.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2012

    East African crussader alliance.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...