Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.
Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.
Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Taarifa zinasema kwamba Marehemu Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.
Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Hii dunia sijui tunakwenda wapi? Yaani unamtupa binadamu mwenzako hivihivi? Rest in peace my dear Agnes we still love you forever
ReplyDeleteJamni jamani!!Nani kafanya ukatiri huwo wa kinyama kwa bint mdogo kama huyo!..Eeh Mungu wangu,,Nimeumia sana kusoma hii historia!
ReplyDeleteMwenyzi Mungu awape Moyo wa Subira wazazi wa marehemu!Ingawa inauma sana jamani!bora angeumwa ikajulikana,lakini kuuwawa!Masikini huwezi juwa alikuwa akijitetea namna gani ili aweze kunusurika na watu hao..Inauma sana!Wamemtanguliza na wao siku wakifa watamkuta Agnes anawasubiri kwa kesi hiyo!
Ahlam,,,UK
Jamni jamani!!Nani kafanya ukatiri huwo wa kinyama kwa bint mdogo kama huyo!..Eeh Mungu wangu,,Nimeumia sana kusoma hii historia!
ReplyDeleteMwenyzi Mungu awape Moyo wa Subira wazazi wa marehemu!Ingawa inauma sana jamani!bora angeumwa ikajulikana,lakini kuuwawa!Masikini huwezi juwa alikuwa akijitetea namna gani ili aweze kunusurika na watu hao..Inauma sana!Wamemtanguliza na wao siku wakifa watamkuta Agnes anawasubiri kwa kesi hiyo!
Ahlam,,,UK
Ni simanzi nzito kwa kweli. Poleni sana wafiwa wote.
ReplyDeleteRest in peace!!!
ReplyDeleteinauma saana kufiwa I have been there. Poleni mama na Baba Agnes poleni.
ReplyDeletepoleni sana wafiwa, Mboa tanzania sio salama tena wenzangu? nini kifanyike so painful binti mdogo jaman. imenikumbusha miaka kama 4 hivi iliyopita mtot wa kiume wa ndugu yangu alikuwa IFM mwaka wa 1 akitoka chuo jioni hakurudi nyumbani na simu ilikuwa haipatikani wazazi wakatoa ripoti polisi baada ya siku kama 2 waliitwa kuja kuutambua mwili uliokotwa bonde la msimbazi sasa najiuliza hivi jeshi letu la polisi linashindwa jamani kudhibiti hali hii mbona inauuma sana sana Mungu tuhurumie na kuponya inchi yetu
ReplyDelete