Mdau Ahmed Ramadhan Dau akiwa ni mwenye furaha baada ya kulamba Nondozz yake ya Bachelor of Engineering (Aerospace Engineering) katika Chuo kikuu cha Keene University of Sheffield United Kingdom Leo.
Dr Dau akiwa na mwanae Ahmed aliyekula nondozzzz na nduguze pamoja na Haruna Mbeyu 'Meya wa London' |
Mdau Ahmed akifurahia na familia yake
Wadau Ahmed Dau (kushoto) na rafikiye Haruna Mbeyu 'Meya wa London' wakiwa kwenye bustani ya Garden ya Chuo hico mara baada ya kulamba nondozz zao.
Mtoto wa simba ni simba: Dk. Ramadhan Dau akiwa na Mwanae Ahmed Dau baada ya kulamba Nondozz yake leo huko nchini Uingereza.
Mdau Ahmed Dau akipongezwa na wadau kwa kula nondozzz |
Congratulation MEYA wa Sheffield!!
ReplyDeletesafi sana kijana na hongera sana,uje sasa utumikie nchi yako na sio utumikie tu bali utumishi wenye weledi kama wa baba yako.
ReplyDeleteJamaa wa kwanza kulia kakaa kiupambe upambe
ReplyDeletehongera doctor Dau kwa kumpatia msingi mzuri wa elimu kijana Ahmad, ng'oa mti panda mti.
ReplyDeleteMdau Coventry UK
Nasikiaga hivi 'vyuo' ni vya 'mifukoni' na vipo majumbani kwa watu! ndio maana wakija hapa wanashindwa kupata kazi kwani hawawezi ku deliver kile ambacho wanadai wamesoma!
ReplyDeletehongera ahmed
ReplyDeleteHawa watu wanaosema Vyuo ni vya mfukoni... chuo gani bongo kilichofanya ubunifu na vitu vikatumika dunia nzima... zaidi ya kusoma mavitu kibao amabayo yameandikwa na hao wenye vyuo vya mfukoni... hiviufikiri wetu uko wapi...wachina wamepeleka watu kibao kwenye hivyo vyuo vya mfukoni na kuiba mengi na sasa wanaongoza ubunifu.. sisi tumepata wachache hawa wakija wakatoa maoni yao wanakuwa kikwazo kwa wenye vyeo wanawaogopa na kuwawekea fitina kwamba watachukua vyeo vyao na kuwapa sababu eti "ku deliver" mbona miaka 50 na kitu na hatuoni "ku deliver huko mnakusema" kwakwkawkakwakw mtabaki huko huko... hongera kaka kwa kupata cheti cha mfukuno ikiwezekana omba kazi huko huko usirudi....
ReplyDeletesasa imekuwaje tena hakuna KANZU, BARAGASHIA, KOTI na makubazi au huko haiswihi?
ReplyDeleteHongerasana Ahmed...walau sasa WAWTU WETU sasa wanazo hizo degree...kisingizio kuwa hatukusoma hakuna
Hongera Ust. Ahmed Dau na Mstahiki Meya wa Londoni Al Akh Haruna Mbeyu kwa Nondozzz zenu!
ReplyDeleteInshallah Allah SW awafungulie!
MashAllah Congratulations Ahmed, tukisomea tanzania wanaiba matokeo yetu yanabadilishwa basi bora kwenda nje ya nchi. Allah atakuongoza InshaAllah
ReplyDeleteMkibosho ndugu yangu naomba uingie google kisha uangalie sheffield Uni ni nn? Kisha fanya tafiti pevu kujua ni watanzania wangapi mpaka sasa wanadegree ya Aerospace Engineering! Kisha angalia kwenye Taasisi za kifedha na za misaada duniani zinaongozwa na wenye sifa gani? Kisha tambua tu kuwa Boeing na Airbus wanategemea kila mwaka wataalamu kutoka hapo "chuo cha mfukoni" ndugu yangu acha wivu na uvivu wa kufikiri. Hakuna mkibosho hata mmoja dunia nzima mwenye sifa hizo!
ReplyDeleteJamani huyu Mkibosho aneyesema Sheffield ni chuo cha mfukoni yeye kasoma kweli? namshauri aende google akaone. Na pia namuuliza watanzania wangapi wana degree ya Aerospace Engineering? Jamani tuacheni wivu wa 'kigala', namshauri akubali matokeo, ikibidi na yeye aende shule maana "tumeshaamka" sasa
ReplyDeletehttp://www.shef.ac.uk/about/rankings
ReplyDeleteWewe unayesema hicho ni chuo cha mfukoni soma rankings hapa juu June unasema nini
Mbona wewe wa Wed Jul 18, 09:33:00 AM 2012 unaumia sana na kanzu nk. hayo yanakuchoma sana na bado kwani nyie simnapeana tu na vyuo vyenu tunawapa kamba mjinyonge ni timing bomb tutawaumbua kwa vimaster vyenu feki ili mkalie ofisi.Yawachoma sana wamfumo hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho.
ReplyDeletehongera bwana Ahmed Dau, mengine waachiye waja wa Mungu kila mtu atasema lake hakuna mtu asiyejua kwamba elimu ya vyuo vikuu ilikuwa kwa watu maalum enzi zile za ujima, sasa kila mtu anakwenda mbele baba yako ni msomi wewe ni msomi familia yako wasomi la ajabu lipi?usijibu chochote kibaya unachimbwa na watu ambao hawampendi baba yako. Hongera Kijana umeonekana wa nguvu kabisa hivi vindege vyao njoo uvibomoe uvisasambue wanunue mpya au wazisimamishe.
ReplyDeletekaka mkibosho do your research first before leaving a comment here! University of Sheffield ni miongoni mwa "Russel group" universities( am a UK university graduate). Hongera kaka Ahmed! piga Masters na Phd kabisa ndo urudi! sky is the limit!
ReplyDeleteHongera sana Ahmed kwa kupata hiyo Nondo yako mwanangu, Allah akulinde na husda zao ambao tumeambiwa ndani ya Quran kuwa wanazo na mfano ni huyo Mkibosho hapo juu ambae ataishia kufanya biashara za magendo na wizi wa kwenye magodown usiku, huku mchana anajifanya anauza duka! Au ataishia kupewa post kwa vyeti feki pale TRA kwa wajomba zake.
ReplyDeleteSalaam nyingi na hongera nyingi sana kutoka kwa Auntie Naima na Uncle Feruz!
MMMMH YANGU MACHO JUKWAA LIMEKUWA MIPASHO HILI.NADHANI MKIBOSHO AMESHINDWA TU KUULIZA SWALI LAKE VIZURI KUWA BAADHI YA VYUO NI VYA MFUKONI. NI KWELI VILIKUWEPO ILA KWA SASA VINGI VIMEFUNGWA. ILA HIKI SI UCHWARA KINATAMBULIKA TUVYEMA. CHA MUHIMU NI MTU MWENYEWE KUPROVE ALIYOSOMA KWANI NIMEWAHI KUKUTANA NA MTU WA CHUO MAARUFU SANA LAKINI AKAWA HAWEZI NA WENGINE WAKO VYUO VIDOGO WANAFANYA MAMBO MAKUBWA TU.
ReplyDeleteMWISHO WA SIKU TUSIANGALIE UKUBWA WA JINA LA CHUO BALI MHITIMU ANAJUA NINI. COURSE ZOTE DUNIANI NI MUHIMU NA WOTE TUNATEGEMEANA, KAMA MTU KAWA RUBANI BASI AJUE HATA NESI ANAFAA KWA NAFASI YAKE.
MDAU SWEDEN
kwa wale wanaokichukulia poa sheffield university labda niwape fact moja ukiachana na mambo ya ranking..chuo hiki kimeshatoa washindi watano wa Nobel (tuzo inayoheshimika sana duniani), tuambieni UDSM wametoa wangapi au the whole of Tanzania for that matter.
ReplyDeleteWadau msiumize vichwa bure. Kila kitu sasa hivi ni transparent. Google university ranks worldwide majibu ya maswali yako utayapata. Chuo bara cha kwanza Africa kinashika nafasi ya 542 katika ubora wa vyuo duniani ambacho ni university of Pretoria. University of Dar Es Salaam ni cha 1500 na kitu nilipoangalia mara mwisho. Hapo ndipo utagundua ni vyuo vipi vinavyopeleka engineers international space station na vile vinavyopeleka enginees kutoboa mv bukoba.
ReplyDelete