Wanafunzi wa Shule ya Msingi Michungwaniiliyopo kijiji cha michungwani, Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tangawakijisomea kitabu kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977 katika mkutano kukusanyaji maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni.
 Abdallah Mohamedi (31) mkaziwa kijiji cha Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga akitoamaoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano wa kukusanya maoni kijijini hapo hivi karibuni.
 Mzee Idrisa Omary (70),mkazi wa kijiji cha Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni mkoani Tangaakitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya Mpya katika mkutano wa kukusanya maonikijijini hapo hivi karibuni. (Picha kwa hisani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC))
 Wananchi wa Kata ya Nkwenda, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wakiwa katikamkutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wa kukusanya maoni yao kuhusu KatibaMpya.
 Bi.Teodezea John, ambaye ni mlemavu, mkazi wa Kata ya Kilimikile, Wilaya ya Misenyi,mkoani Kagera akitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanyamkutano wake wilayani hapo. hivi karibuni.
Wiliam Wilbard Ishengoma, mkazi wa Kata ya Bwanjai, Wilaya ya Misenyi mkoani Kageraakitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wakewilayani hapo hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nyie mliyoko majuu ,angalieni umati uliofurika hapo juu, watu wote wamependeza ,nyuso za furaha mavazi mazuri ya kawaida,mwangalieni huyo mzee mwenye miaka 70,uso bado imara hauna mikunjo mikunjo. Lakini Tv za kwenu huko UK na USA huonyesha africa watu tumechoka mbaya, eti tumejaa tongotongo na inzi machoni. Ukifanya kijisafari kidogo kwenda nje ,ukikutana na mzungu ,maongezi yenu yakigusa jina AFRICA tu basi umeharibu-ataanza ,dah ,huko mnashida sana,sijui vita vya wenyewe kwa wenyewe,sijui viongozi wenu corrupt,sijui nini !!!basi ataongea yeye tu.Ukimuuliza, hivi wewe ni nchi gani africa umewahi kutembelea ?? jibu lake ni kwamba,anaangalia kwenye TV. Unaona ushenzi huo ?? Jamani niambieni, huu tu uite ujinga ,Ushenzi, Ushamba?. Sasa cha ajabu, kuna dada zetu nao wakifika huko wanakuwa hawana tofauti na huyu mzungu ambaye hajafika africa. Jamani waelimisheni hao,kuweni mabalozi wetu na wenye kuupenda uzalendo. Ni mimi Zebedayo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Inasikitisha TZ bado watoto wanakwenda shule miguu peku na wengine malapa/ndala. Ni aibu kwa nchi yenye utajiri mkubwa wa dhahabu, diamond, tanzanite, gas asilia, mbuga nzuri za wanyama to name a few.
    Aibu kwa viongozi wa nchi hii.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2012

    kudadadeki yaani hao ndio wanafunzi wa kutegemewa kujenga taifa lijalo? NI aibu hatuwezi kufika huko tuendako, kamwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...