Home
Unlabelled
Taa hizi zinamulika nini Mchana wote huu??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kwa uelewa wangu, taa hizi huwa zimetengenezwa kwa utaalamu ambao huwa hujiwasha zenyewe panapotokea gizi na hujizima mchana. Sasa uzito wa giza unatofautiana, kuna giza la mawingu mazito na giza la usiku. Magiza yote haya husababisha taa hizi kuwaka. Kwa hiyo basi kama ilikuwa machana na hapakuwa na wingu zito hiyo ni hitilafu lakini kama palikuwa na wingu zito basi ndio utendaji wa kawaida wa taa hizo za mitaani.
ReplyDeletemafisadi wamezidi na utumizi potovu ndo huu tena taa zinawaka mchana wakati usiku taa zina zimwa ha ha ha bongo bongo
ReplyDeleteNDIO UFISADI WENYEWE HUO KAZI KUKAMATA WATU MBAGALA NA MANZESE NA TEMEKE ILA HAO WANAACHIWA SIO WAAZNE BASI NA KUTIZAMA BILLI ZA VIONGOZI ZA SIMU MAKAZINI WAONE WANALIPA??????? MSEMA KWELI.
ReplyDeleteMdau wa juu kabisa nakubaliana na wewe,labda kuelezea kitaalamu kidogo ni kwamba taa izo za barabarani zinakuwa na kitu kinachoitwa kwa lugha ya kitaalamu ni (light-sensitive photocells),Kwaiyo endapo kama kutatokea hali yoyote ya mwawingu hizo light-sentive photocells Upelekea kusababisha taa izo kujiwasha wakati wa Mchana.
ReplyDeleteMdau,
Institute For Multi-sensor Processing & Content Analysis
curtin University
Australia.
sasa mdau mwenzangu wa institue for multi sensor processing and content analysis curin university austarali, sisi kwa nini tunaweka hizi light sensitive photocells, zinatupa manufa gani wakati uchumi wetu mdogo mafisadi wanatanua tu tunajifanya kukimbilia katika dunia ya watu wa kwanza marekani na ulaya wakati sisi ndo kwanza tunatambaa.
ReplyDeletei know very well light hizi za sensitive photocells huku marekani wanazitumia sana watu katika majumba yao pia kwa kujilinda kama ana garden kubwa. lakin kwa tanzania ni ufisadi wa hali ya juu
tanzania ni nchi tajiri sana laki mafisadi ndo wanao haribu nchi na watu wawekezaji wezi wa mali asili zetu
mungu tusaidiye.amin
THANKS MAN MDAU WA AUSTRALIA KWA UFAFANUZI WAKO
Nakerwa sana na watu mnaolaumu mafisadi. Baada ya kuona viongozi ni mafisadi na hatua gani mlichukua kukomesha ufisadi huo kama sio kulalamika tu? Ulalamishi hautaondoa ufisadi hata siku moja. Maneno ya ulalamishi kuhusu ufisadi nimeanza kuayasikia tangu awamu ya pili na tatu lakini sijaona mchango wowote toka kwa wananchi ili kukomesha tabia hii. Pia mkumbuke baada ya Slaa na Kabwe kuanika ufisadi nchini, REDET walifanya utafiti wakati uchaguzi wa 2015 unakaribia ili kubaini kama ufisadi ni tatizo kwa wananchi na hivyo pengine wangechagua watu wengine waingie kwenye system. Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba kwa wananchi wa Tanzania ufisadi si issu ya kuacha kumchagua kiongozi. Pia mkumbuke hao viongozi wametoka kwa wananchi. Hivyo basi tabia za ufisadi walizo nazo ni reflection ya tabia za jamii nzima. Ndo mana kuna baadhi ya watu (hasa kule kwa akina Manka) wanamsifia mtu aliyeibia mashirika ya umma na kuyafilisi. Wananchi hawahwa wanamlaumu kiongozi kama atatoka kwenye uongozi mkubwa halafu akaonekana masikini.
ReplyDeleteJengo lenye taa hizo ni la 'Benki ya watu wa Zanzibar' (The Peoples Bank of Zanzibar-PBZ) hivyo hapo wanaomulikwa ni jamaa wa UAMSHO ili wasije wakavuka bahari kupenya na kulipua kwa mabomu Rasilimali za Zanzibar!
ReplyDeleteMimi ndio yule mdau wa kwanza juu kabisa. Naomba kuongezea kuwa taa za nje nyumbani(security lights) kwa walio wengi ikifika usiku unawasha mwenyewe. Je za barabara zote Tanzania utampa nani kazi hiyo?? basi hiyo ndio sababu zimetengenezwa ziwe na uwezo wa kujiwasha na kuzima mwenyewe (automated) kwa kutumia electronics ambapo kama alivyosema mdau mmoja hapa kuna vifaa vinavyoitwa photo detectors au photosensitive cells vinavyoweza kutambua giza na mwanga.Hivyo nafikiri suala hili halipo upande wa ufisadi.
ReplyDeleteJamani, mie naishi nairobi na security light zangu including gate lights ni za photocell, nairobi mara nyingi jua huwa haliwaki mchana hasa wakati huu wa baridi but sijaona hizo taa zikiwaka mchana hata kama kuna mawingu. Huwa zinajiwasha saa 12 jioni na kujizima saa 1 asubuhi.
ReplyDeleteMdau Anonymous Thus Jul 26, 08:24:00 AM 2012, unaposema Je taa za barabara zote Tanzania utampa nani kazi hiyo ya kuziwasha?. Na mie nikuulize, mbona bendera za taifa ni nyingi kuliko hizo taa za barabarani lakini ikifika saa 12 bendera zote zimeshushwa, kipi ni bora hapo kuendelea kupoteza umeme ambao ungetumika kwa matumizi mengine au kuweka taa ambazo zinawashwa manually (fanya cost-benefit analysis uone hali halisi)
ReplyDelete