Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2012

    Hii kali... jamaa anatumia majini. Hivi hamna Humane Society Tanzania? Kuua wanyama wakufugwa nyumbani ni makosa ya jinai, hii ni kwa ajili ya kulisha hayo majini? Angekuwa anafanya hata kuku basi akichinjwa watu watamla. Huko Marekani anakotaka kwenda nani atampa paka wa kuchinja atajikuta yupo jela. Wahurumieni hao paka!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2012

    Tusipoangalia watanzania tulivyo huyu Jamaa twaweza kumpatia UBUNGE kama mwenzake hapo 2015.. hatuangalii vigezo tunaangalia unatambulika kwa kiasi gani ndani ya Jamii

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2012

    Kichwa kinaniuma na kuogopa kurudi nyumbani pale ninapojiuliza Tanzania tumejiandaa vipi na shirikisho la Afrika mashariki, Sisi kila kukicha matatizo na kuendekeza ujinga usiokuwa na maendeleo yoyote wakati wenzetu wanajipanga hasa kwa kuitamani ardhi yetu.. Vijana wa Tanzania tubadilike

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2012

    Tanzania ni nchi pekee iliyojaliwa na jamii yenye imani za ajabu inasikitisha.siku hizi watu wa dili ni waganga wa jadi wa waanzisha dini za ajabu ajabu.ndo maana babu anapeta sa hivi.si utani research inabidi ifanyike katika jamii yetu. wawe wasomi kwa wasiosoma ni hatari.wachungaji wa dini mpya ndo matajiri wa kupindukia huku akina manyaunyau wakipamba jiji kwa matangazo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2012

    Dogo janja mwanangu... ale wapi? Anadai anakidhi mahitaji ya watu ... kama mdau alivyosema hapo juu inaonekana "uganga" dili Bongo... Ama kweli Bongo tambarare....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2012

    Tusipoamka sasa, ushirikina na imani za kipumbavu zitaizamisha jamii na nchi yetu. Ankal, tafadhali sana usiipe publicity mijitu mijahili kama huyu "mganga" feki. Mwaka 2004, katika gazeti la Majira Jumapili kulikuwa na picha ya paka akichomwa hai Morogoro hadharani. Ninavyokumbuka, hakuna hata kiongozi moja wa dini au wa siasa aliyekemea unyama na ushenzi huo! Pili, mbele ya Mwenyezi Mungu wanaadamu tuna wajibu wa kuwaonea huruma wanyama badala ya kuwafnyia ukatili. Wengi wetu bado tunakumbuka jinsi mwaka jana watu walivyofurika kwa "babu" wa Loliondo eti kufuata dawa ya miujiza licha ya madaktari wengi Arusha na Moshi kuwaonya wagonjwa wao wasiwache dawa zao za hospitali! Matokeo ni kuwa mamia ya watu wamepoteza maisha yao, bila kuhesabu watu waliopata kiharusi au kukatwa vidole kwa kuwa waliacha kutumia insulin. Karne ya 21 ni karne ya sayansi na imani ya Mungu Muumba...si karne ya abrakadabra ya enzi za giza la kijahiliya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2012

    TATIZO LA BONGO WATU KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. WEWE NDIO MGANGA NA UNATOA MSHUKIWA NA KUMUADHIBU. ETI BONGO IMEENDELEA TURUDI NYUMBANI, WATU WANATIBIWA NA NYAU. JAMANI BALAA HII HUU WIZI MCHANA. HUYU MGONJWA AONE DAKTARI

    ReplyDelete
  8. dr.manyaunyau mimi na muaminia sana kwani kuna mambo mengi tu kaya fanya nami nimeyashudia

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2012

    Nchi yetu inakokwenda.ukishuka tu airport njia nzima imejaa mabango ya hawa jamaa na hasa mganga toka Nigeria,sumbawanga,sijui Tanga.watu bongo wana imani za ajabu ajabu kuanzia mawaziri hadi mtu wakawaida kabisa.Na mbaya zaidi mabango yameenda hadi katikati ya jiji pale bibi titi emergine mabango yamesheheni ya waganga wa jadi.OH my GOD.nilifika kwa Kagame Kigali nikaangalia how people are cilvilized watu wanaangaliana ni nani anadondosha taka taka huwezi kuuona upuuuzi kama wa miji ya bongo.TUBADILIKE MAMLAKA ZIFANYE KAZI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2012

    Hakuna lolote ni utapeli tu huu, kudanganya watu na kuwachukulia fedha zao,. Kweli kuishi mjini akili,

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 05, 2012

    Huyu ni Tapeli jamani..anatapeli sana watu kuwa anawapa utajiri then mwishowe ni kuwakomba pesa zao zote..Michuzi,Mahakama za Dar ana kesi kibao tu ambazo zinamtuhumu..pia anacheza deal za kuwashika watu uchawi kumbe si kitu wala nini..tahadhari..ni tapeli huyu..wengi wameshatapeliwa nae na kushuhudia haya..
    yani sijui niwambieje..huyu si mganga..alimtapeli rafiki yangu mpaka akataka kuuza gari lake..dakika za mwisho ndo kutoa issue tukamzuia..anamtindo ule wa kutoa mahela kwa njia ya mazingaombwe then anakwambia kalete kiasi flan ili uweze kumiliki hizo pesa..ukipeleka tu umeliwa..anakupeleka sehemu maporini eti kuonana na mapepo na mizimu..wivi..kumbe ni watu wamevalishwa nguo za kutisha tu..mwizi..mwizi mkubwa..hakuna cha mganga hapa..na wala msiamini kama waganga watabadilisha maisha yenu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 05, 2012

    ndo unatuwekea watu gani hawa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 05, 2012

    watu wengine mlishafulia zamani ndio maana mnaogopa kurudi bongo, kwahiyo huyu dogo isiwe kisingizio. yeye hiyo ndio njia yake ya kujipatia mkate wake kama nyinyi mlivyokimbia kwenu ili wenda kubeba box na kubadilisha nepi wazee wa kizungu. tena hao mnaowaabudu siku hizi ndio washirikina bila ya kuficha maaana movies zao zote ni za misukule, swali ni kwamba walijifunza Africa? aliekua kocha wa England world cup 1998 alilalamika kwamba fa walidharau kuhusu alivyowaambia kwamba mganga wake ameona kadi nyekundu kwa mchezaji nyota wa England hivyo wasafiri nae ili akaifute lakini wakagoma na matokeo yake ni beckham aliepewa hiyo kadi katika mechi dhidi ya Argentina, euro 2000 walisikika Holland wakiwapa onyo France kwamba wawe makini sana na Italy katika mechi ya fainali kwani wachawi mno. champions league final 1999 sir alex alisema waliambiwa ili kushinda ile mechi basi wafanye mazoezi wakiwa wamevaa jezi ambazo zilikua zikitumiwa na kikosi chao kilichopoteza maisha katika ajali ya ndege. HAPA NAOMBA MUELEWE KITU KIOMJA, SINA LENGO LA KUTETEA VITENDO VYA KISHIRIKINA ILA NATAKA MFAHAMU KWAMBA HATA HAO MNAOWAABUDU PIA WANAJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO KWAHIYO MSIJISHAUE MAANA MKIISHI ULAYA MNAONA MMESHAMALIZA WAKATI WENGINE MLIENDA HUKO KWA JUHUDI ZA BIBI ZENU KUKESHA MAKABURINI. NA WENGINE WAKO HUKO LAKINI MPAKA LEO WANA WAGANGA WAO BONGO.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 05, 2012

    UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI !!!

    Baada ya binaadamu kukutana na changamoto anapata akili na anajikwamua!

    Wazungu wanasema 'Learn through challenge'',,,

    Vitu kama:

    1.Ukosefu wa ajira
    2.Ushindani wa Kibiashara
    3.Ugumu wa maisha
    4.Changamoto ktk jamii
    5.........

    Na mambo kadha wa kadha vinapelekea binaadamu kama kiumbe mwenye akili kupata ubunifu wa jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo na kuyamudu maisha!!

    Baada ya kukabiliana na ile life challenge (changamoto ya maisha) na kutumia akili ndio hapo unajikuta Kijana Mdogo kabisa unaitwa 'Babu' au Mganga wa Jadi!

    Hakuna nini wala nini ni maisha tu!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 05, 2012

    Dakitari,

    Ziara yako ya Marekani itapata mafanikio endapo utashirikiana na Ubalozi wetu Washington DC wakupe barua ya kuwa utaendesha zoezi au Jaribio la Kisayansi 'sio uganga' ya kuwa ktk jaribio kutakuwa na mauaji ya viumbe kama paka!

    Hapo ndio utachomoka bila ya hivyo utakumbana na Maandamano na Wanalibeneke Wanaharakati wa Haki za Viumbe!

    Itakuwa hapatoshi, unaweza kukatisha ziara!

    Wana Mtalimbo Majuu wanasomeka?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 05, 2012

    Nimewasikia wote na maoni yenu. Nitawamulika sawa sawa!!! Mnatukana kazi za watu eti???

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 08, 2012

    Unavyozidi kuelekea Western Africa kuanzia Congo mpaka Senegal pamoja na nchi zote zilizopo hapo kati uchawi na uganga wa kienyeji ni OFFICIAL, wanaitwa ''Marabout''.
    Na ni watu wenye hadhi ya VIP, kuendeana na 'uzoefu' wao.

    Ukienda sokoni kutafuta kuku wa kienyeji kama vile umeenda mwenge sokoni au buguruni sokoni kwa ajili ya supu unaangaliwa na macho ya ajabu ajabu. Kuku wa kienyeji wa sokoni ni wa DAWA!!! hawaliwi!!!!
    Wanahifadhiwa ndani ya 'visalfeti'

    Tembea uone!

    TZ hatujafikia hali hii bado.

    Sio kwamba nakubaliana au naamini manyaunyau ni mambo ambayo nimeyaona mwenyewe. Mambo kuzidiana. Nyumbani TZ hali haijafikia wenzetu West Africa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...