Walimu wakuu wa shule za ,msingi,sekondari na waratibu elimu kata wakiwa katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Saidi Mwambungu aliyesihi kuwahamasisha walimu wote kuacha mgomo na kurejea kazini mara moja wakati maswala yao yakishughulikiwa.Kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria Manispaa ya Songea. 
Picha na Revocatus Kassimba

)


Walimu katika mkoa wa Ruvuma wametakiwa kurejea kazini na kuachana na mgomo ambao unawaumiza wanafunzi kwa kuwanyima haki yao ya kupata elimu.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakati alipofanya kikao cha pamoja na walimu wakuu wa sekondari,shule za msingi na waratibu elimu kata wa wilaya ya Songea mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu huria Manispaa ya Songea.
 Mkutano huu aliuitisha ili kurejea kauli ya serikali kuwa mgomo unaoendelea mkoani Ruvuma na nchi kwa ujumla si halali kwani suala hilo lipo katika Mahakama Kuu  divisheni ya kazi.
“Nawasihi sana walimu wote rejeeni madarasani wakati huu suala hili likiendelea kushughulikiwa na mamlaka husika” alisema mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Mkoa amewapongeza walimu wote ambao toka mgomo huu ulipoitishwa hawajasitisha kutoa Huduma ya kuwafundisha wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo wameonyesha uzalendo na heshima kwa serikali ambayo ndiyo mwajili.
Mwambungu alikemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa chama cha walimu mkoani Ruvuma kupita katika shule na kuhamasisha walimu kugoma na kueleza kitendo   hicho ni utovu wa nidhamu kwani shule zote ni mali ya serikali wala si za chama cha walimu (CWT).
“CWT si mwajili wa walimu bali ni chama cha kitaaluma hivyo kinapaswa kuheshimu maagizo ya mahakama na kusitisha mgomo kwa kuwatakia walimu wote warejee madarasani”
Mwambungu amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa CWT kuwahamasisha walimu kugoma kwa kupita mashuleni ambapo ameeleza kuwa serikali inawafuatilia na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa makosa ya uchochezi.
Aliongeza kusema kuwa uamuzi wa kugoma ni kuwadhurumu watanzania wengi wakiwemo watoto wa shule wasio na makosa hivyo akawasihi walimu wakuu wa shule za msingi , sekondari na vyuo kuwahamasisha walimu wao kurejea kazini kazi ambayo walimu wakuu wamekubali kuifanya ili kurejesha hali ya ufundishaji katika utaratibu wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Angalau huyu ameonesha ukomavu na busara kwa KUWASIHI waalimu waache mgomo, sio kulazimisha na kutoa vitisho kama viongozi wengine wanavyofanya. Walimu wana haki ya kugoma na wamevumilia muda mrefu. Ifahamike kwamba 100% wanazotaka ziongezwe ni ndogo sana kwa kuwa mshahara wao ni mdogo. Watu wasipotoshwe kwa asilimia. Mshahara wa TZS 200,000 ukiongezwa kwa kiasi hicho maana yake wanadai TZS 400,000 ambazo zinalipika kama serikali ikibadili vipaumbele vyake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...