Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joe Bendera (kulia) akitabasamu huku akiinua juu kombe la ubingwa wa 2012 Copa Coca-Cola kwa msaada wa nahodha wa timu ya Morogoro Hassan Mganga wakati wa sherehe za kufunga michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Timu ya Morogoro iliibuka bingwa baada kuichapa Mwanza 1-0. Wengine ni Meneja Mkazi Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan (kushoto) na Rais wa TFF Leodgar Tenga (nyuma).
Menaja Mkazi Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs750,000/- mfungaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola Mtalemwa Abogasti wakati wa sherehe za ufangaji wa michuano ya Copa Coca-Copa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joe Bendera (kati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs750,000/- kipa bora wa michuano ya Copa Coca-Cola Shukuru Mohammed wakati wa sherehe za ufangaji wa michuano ya Copa Coca-Copa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan akiwakabidhi medali wachezaji wa timu ya Mwanza baada ya kuibuka mshindi wa pili kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012.
Afisa wa maendeleo ya soka katika ukanda wa Africa Mashariki na Kusini wa FIFA Ashford Mamelodi, akiwatuku waamuzi wa michuano ya Copa Coca-Cola 2012 iliyomalizika Jumapili, Julai 15 kwa Morogoro kuibuka bingwa baada ya kuifunga Mwanza 1-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    Jamani mjomba michuzi mm nilisema moro noma kwasoka...go go moro vijana wanatisha kinoma..kama kuna mtu yoyote anabisha kama moro sio noma kisoka alete mjadala hapa hapa..kazi kwenu wadau..naitwa mzazi toka mji wa leicester uk.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Safi sana wa mikoani waoneshe kuwa Dar siyo kila kitu. Nawapongeza waluguru mkoa ufanye jambo kuwapongeza na kuweka kumbukizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...