Habari ankal Michu,

Naomba kuulizia ati ni Hospitali gani Kwa Tanzania madaktari wake ni stadi kutibu dalili za kiharusi?(kupooza au Stroke).Nina mzee wangu aliwahi kufanyiwa opresheni flani baada kama mwaka ameanza kupoza sehemu ya kidole kimoja kisha kufuatiwa cha pili.

Baadhi ya wataalamu wamesema ni dalili za kiharusi na aanze matibabu haraka.

Amejaribu matibabu ya mitishamba lakin bado sasa amefanyiwa uchunguzi na kuambiwa kuwa ni mishipa yake imeblock usambazaji wa damu na atumie dawa za kuyayusha.

Kwa huku Ulaya matibabu haya hufanyika within 24 hours na mgonjwa hurudia hali yake ya kawaida sasa naomba kuliza je Kwa Tanzania pamoja na Zanzibar kuna Hospitali yoyote inayotoa huduma bora kabisa kwa aina hii ya kiharusi ( ni vidole tu viwili kwa sasa lakini kuepusha kuendelea).

Nahitaji msaada wa kujua hizo hospitali kwa hali na mali pia kama kutakuwa watu wanafahamu na Bei za matibabu hayo either kwa dawa au hata kwa operesheni

Ahsante
Mdau UK oversees Island

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2012

    Mdau pole kwa kuuguza kwa shida zote za masuala ya maradhi ya macho, mishipa ya fahamu, kupooza na ulemavu wasiliana na CCBRT

    www.ccbrt.or.tz

    Address: P O Box 23310
    Dar es Salaam, Tanzania
    Tel: + 255 (0) 22 260 2192
    Fax: + 255 (0) 22 260 1544
    Email: info@ccbrt.or.tz

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2012

    Pole sana kwa ajili ya mzee wako mdau. wakati mzee anasubiri hilo jibu waambie nyumbani wamenye vitunguu swaumu kijae kikombe cha chai na tangawizi nusu kikombe wapime vikombe vitatu vya maji (vikombe vya chai) waweke kny sufuria wachemshe mpaka kibaki kikombe kimoja. wachuje na kumpa mzee anywe kabla ya kula kitu chochote asubuhi halafu akae bila kula kwa masaa mawili then afungue kinywa na matunda tu. baada ya hapo anaweza kula kama kawaida. tiba hii inayeyusha damu na kufungua mishipa iliyo block. atumie kwa siku saba tu. anaweza kupungua uzito baada ya hii therapy kwani huo mchanganyiko unaenda kuattack HDL Cholesterol ambayo ndiyo inaivimbisha mishipa na kusababisha blockage.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2012

    TUMIA DOZI YAB MACHUNGWA WAKATI UNATAFUTA HOSPITAL. MACHUNGWA DOZI HIZI: SIKU YA KWANZA 5- SIKU YA PILI SIKU YA TATU 10- SIKU YA NNE 15 - SIKU YA TANO 20 - SIKU YA SITA 25 - SIKU YA SABA 20 - SIKU YA NANE 15 - SIKU YA TISA 10 - SIKU YA KUMI 5, AKIPONA KABLA MWAMBIE NA WENZAKO.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2012

    Aisee, kila la kheri, pia fanya hima!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2012

    wewe upo UK ambayo iko ndani ya EUsasa kama karatasi zako ziko sawa usiumlete Huku huyo Baba yako!? Au una karatasi ya kuchakachuliwa!!!? Ndio hapo utakapoona Watz wakiwa na uongo na yakiwazidi huku Majuu, kijasho kinawatoka lakini angekuwa mwanadada anaumwa ungemleta huku ili ujitukuze kumbe mambo yako ni ya kubabaisha tuuu, rudi home kama unataka kumsaidia au mlete huko ataishi zaidi ya miaka 90 kama Wazungu na kupona mpaka siku yake ya mwisho!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2012

    huu ugonjwa siku hizi kule nyumbani umeenea sana ila kwa ushauri wangu kama upo uk, nenda hospitalini hapo hapo uk, wao watakuwa na vidonge vya kuzibuwa hio mishipa iliyoziba kupitisha damu kama wewe mwenyewe unavyosema kwahapo ulipo ni kitu kidogo tu

    binafsi hili tatizo lilinifikia mzee wangu huko nyumbani nikapatiwa hivi vidonge hapa germany na tatizo limeondoka la ukimtafutia dawa huko nyumbani utaambiwa mamilioni ya tsh na ugonjwa utakuwa pale pale

    jaribu hio wewe mwenyewe kwanza hususan hospitali zilizoko vijijini au jaribu kwenda kwenye maduka ya dawa ya wazungu sio wahindi hapo uk

    wao watakulenga ni hospitali gani utapata hio tiba,

    ishallah utafanikiwa tu, mara nyengine nakushauri ukiandika kitu kama hichi andika e mail yako unaweza kupata msaada zaidi wa mawazo

    shukran sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2012

    Pole sana Mdau. Hospitali nzuri ni Regency na Aga Khan. Hata M2 wanaweza lakini huu mgomo inakuwa shida kidogo.

    ReplyDelete
  8. Msafirishe baba yako hadi uko uliko apate matibabu 24hrs. Pole sana kwa kuuguliwa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2012

    Sijui kama hi massage itakufikia Direct ila.Kuna Clinic ipo Mwenge njia ya CocaCola.ni ya Wahindi,ili tokea kama bahati sehemu niliyo kuwa nakula nikawa namuelezea jaa mayangu matatizo ya kisukari ya ndugu yangu mmoja .ndi huyo Dkt akaingilia na kuniambia about hosptali yao.jina nimelisahau ila nadahni iko peke yake mita ya cocacola mwenge,nili muliza maswali mengi ya kumpima,na aliniabia wana tibu cancer na ina isha kabisa Kisukari ,na vidonda vya tumbo vina isha kabisa,kitu ambacho hospitali za kawaida huz=wezi tibiawa hivyo.ameniambia 90% ya wagonjwa wa cancer wamepona ila pia inategemea hiyo cancer ime fikia stage gani,kwa sababu kuna stage hiki fika haiwezi pona tena ila wanaweza punguza makali.hope nime help kidogo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2012

    Pole sana mkuu,kwa huduma ya kwanza nashauri kuwa mzee aachane na nyama ya ng'ombe kama anatumia,aiche kabisa,badala yake atumie samaki,kuku na mbuzi(kwa mbuzi iwe kiasi),nyama ya ng'ombe ina zidisha ganzi hivyo kuwa na uwezekano wa kuongeza upoozaji.

    Kwa Hospital ipo moja ya kisuni pale kigogo luhanga,hawa jamaa wanatibu kwa mujibu wa sunnah dawa zao mashaallah zinatibu.

    Waweza pia kuwaulizia pale msikiti wa Mtoro K.Koo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2012

    Pole mdau. Kama alivyosema mchangiaji hapa juu, mpeleke mzee Aga Khan au Regency. Uliza clinic ya Neurosurgeon. Ikishindikana, mpelekeni India ambako watu kama hao wamewahi kutibiwa na kupona 100%.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2012

    kama utakua una uwezo msafirishe India hatapata matibabu TZ, watamzibua mishipa ya damu gharama ya matibabu si kubwa saana ukimuacha sehemu isiyofika damu atapata vidonda visivyotibika na itabidi akatwe vidole NK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...