Habari ankal Michu,
Naomba kuulizia ati ni Hospitali gani Kwa Tanzania madaktari wake ni stadi kutibu dalili za kiharusi?(kupooza au Stroke).Nina mzee wangu aliwahi kufanyiwa opresheni flani baada kama mwaka ameanza kupoza sehemu ya kidole kimoja kisha kufuatiwa cha pili.
Baadhi ya wataalamu wamesema ni dalili za kiharusi na aanze matibabu haraka.
Amejaribu matibabu ya mitishamba lakin bado sasa amefanyiwa uchunguzi na kuambiwa kuwa ni mishipa yake imeblock usambazaji wa damu na atumie dawa za kuyayusha.
Kwa huku Ulaya matibabu haya hufanyika within 24 hours na mgonjwa hurudia hali yake ya kawaida sasa naomba kuliza je Kwa Tanzania pamoja na Zanzibar kuna Hospitali yoyote inayotoa huduma bora kabisa kwa aina hii ya kiharusi ( ni vidole tu viwili kwa sasa lakini kuepusha kuendelea).
Nahitaji msaada wa kujua hizo hospitali kwa hali na mali pia kama kutakuwa watu wanafahamu na Bei za matibabu hayo either kwa dawa au hata kwa operesheni
Ahsante
Mdau UK oversees Island
Mdau pole kwa kuuguza kwa shida zote za masuala ya maradhi ya macho, mishipa ya fahamu, kupooza na ulemavu wasiliana na CCBRT
ReplyDeletewww.ccbrt.or.tz
Address: P O Box 23310
Dar es Salaam, Tanzania
Tel: + 255 (0) 22 260 2192
Fax: + 255 (0) 22 260 1544
Email: info@ccbrt.or.tz
Pole sana kwa ajili ya mzee wako mdau. wakati mzee anasubiri hilo jibu waambie nyumbani wamenye vitunguu swaumu kijae kikombe cha chai na tangawizi nusu kikombe wapime vikombe vitatu vya maji (vikombe vya chai) waweke kny sufuria wachemshe mpaka kibaki kikombe kimoja. wachuje na kumpa mzee anywe kabla ya kula kitu chochote asubuhi halafu akae bila kula kwa masaa mawili then afungue kinywa na matunda tu. baada ya hapo anaweza kula kama kawaida. tiba hii inayeyusha damu na kufungua mishipa iliyo block. atumie kwa siku saba tu. anaweza kupungua uzito baada ya hii therapy kwani huo mchanganyiko unaenda kuattack HDL Cholesterol ambayo ndiyo inaivimbisha mishipa na kusababisha blockage.
ReplyDeleteTUMIA DOZI YAB MACHUNGWA WAKATI UNATAFUTA HOSPITAL. MACHUNGWA DOZI HIZI: SIKU YA KWANZA 5- SIKU YA PILI SIKU YA TATU 10- SIKU YA NNE 15 - SIKU YA TANO 20 - SIKU YA SITA 25 - SIKU YA SABA 20 - SIKU YA NANE 15 - SIKU YA TISA 10 - SIKU YA KUMI 5, AKIPONA KABLA MWAMBIE NA WENZAKO.
ReplyDeleteAisee, kila la kheri, pia fanya hima!
ReplyDeletewewe upo UK ambayo iko ndani ya EUsasa kama karatasi zako ziko sawa usiumlete Huku huyo Baba yako!? Au una karatasi ya kuchakachuliwa!!!? Ndio hapo utakapoona Watz wakiwa na uongo na yakiwazidi huku Majuu, kijasho kinawatoka lakini angekuwa mwanadada anaumwa ungemleta huku ili ujitukuze kumbe mambo yako ni ya kubabaisha tuuu, rudi home kama unataka kumsaidia au mlete huko ataishi zaidi ya miaka 90 kama Wazungu na kupona mpaka siku yake ya mwisho!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletehuu ugonjwa siku hizi kule nyumbani umeenea sana ila kwa ushauri wangu kama upo uk, nenda hospitalini hapo hapo uk, wao watakuwa na vidonge vya kuzibuwa hio mishipa iliyoziba kupitisha damu kama wewe mwenyewe unavyosema kwahapo ulipo ni kitu kidogo tu
ReplyDeletebinafsi hili tatizo lilinifikia mzee wangu huko nyumbani nikapatiwa hivi vidonge hapa germany na tatizo limeondoka la ukimtafutia dawa huko nyumbani utaambiwa mamilioni ya tsh na ugonjwa utakuwa pale pale
jaribu hio wewe mwenyewe kwanza hususan hospitali zilizoko vijijini au jaribu kwenda kwenye maduka ya dawa ya wazungu sio wahindi hapo uk
wao watakulenga ni hospitali gani utapata hio tiba,
ishallah utafanikiwa tu, mara nyengine nakushauri ukiandika kitu kama hichi andika e mail yako unaweza kupata msaada zaidi wa mawazo
shukran sana
Pole sana Mdau. Hospitali nzuri ni Regency na Aga Khan. Hata M2 wanaweza lakini huu mgomo inakuwa shida kidogo.
ReplyDeleteMsafirishe baba yako hadi uko uliko apate matibabu 24hrs. Pole sana kwa kuuguliwa.
ReplyDeleteSijui kama hi massage itakufikia Direct ila.Kuna Clinic ipo Mwenge njia ya CocaCola.ni ya Wahindi,ili tokea kama bahati sehemu niliyo kuwa nakula nikawa namuelezea jaa mayangu matatizo ya kisukari ya ndugu yangu mmoja .ndi huyo Dkt akaingilia na kuniambia about hosptali yao.jina nimelisahau ila nadahni iko peke yake mita ya cocacola mwenge,nili muliza maswali mengi ya kumpima,na aliniabia wana tibu cancer na ina isha kabisa Kisukari ,na vidonda vya tumbo vina isha kabisa,kitu ambacho hospitali za kawaida huz=wezi tibiawa hivyo.ameniambia 90% ya wagonjwa wa cancer wamepona ila pia inategemea hiyo cancer ime fikia stage gani,kwa sababu kuna stage hiki fika haiwezi pona tena ila wanaweza punguza makali.hope nime help kidogo.
ReplyDeletePole sana mkuu,kwa huduma ya kwanza nashauri kuwa mzee aachane na nyama ya ng'ombe kama anatumia,aiche kabisa,badala yake atumie samaki,kuku na mbuzi(kwa mbuzi iwe kiasi),nyama ya ng'ombe ina zidisha ganzi hivyo kuwa na uwezekano wa kuongeza upoozaji.
ReplyDeleteKwa Hospital ipo moja ya kisuni pale kigogo luhanga,hawa jamaa wanatibu kwa mujibu wa sunnah dawa zao mashaallah zinatibu.
Waweza pia kuwaulizia pale msikiti wa Mtoro K.Koo
Pole mdau. Kama alivyosema mchangiaji hapa juu, mpeleke mzee Aga Khan au Regency. Uliza clinic ya Neurosurgeon. Ikishindikana, mpelekeni India ambako watu kama hao wamewahi kutibiwa na kupona 100%.
ReplyDeletekama utakua una uwezo msafirishe India hatapata matibabu TZ, watamzibua mishipa ya damu gharama ya matibabu si kubwa saana ukimuacha sehemu isiyofika damu atapata vidonda visivyotibika na itabidi akatwe vidole NK.
ReplyDelete