Mchezaji wa Timu ya Azam,Khamis Mcha (22) akipimana ubavu na Shomari Kapombe wa Simba katika mchezo wa Mashindano ya Cecafa Kagame uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Azam ndio iliyoibuka kidedea kwa kuilambisha Simba Bao 3 -1.
Wachezaji wa Simba,Felix Sunzu (alieshika Mpira) na Haruna Moshi wakijiandaa kuanza mchezo baada ya kufungwa goli la kwanza.mpira umemalizika hivi punde uwanjani hapa na Azam wameweza ibuka washindi na kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya kombe hilo la Kagame kwa ushindi wa Bao 3-1.
Kipa wa Azam,Deogratius Munisi akiondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.
Mshambuliaji wa Azam,Kipre Tchetche akiwazungusha Mabeki wa Simba katika mchezo wao uliopigwa jioni hii Uwanja wa Taifa Jijini Dar.Azam imeshinda bao 3-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    Simba leo hawachomoi ,Azam wana kila hali na uwezo wa kushinda .Azam vs yanga fainal,big up mdau big Joe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Piga hao, Simba gani asounguruma?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    HAHAHAAAAAAAAAAAA SIMBA MDEBWEDO

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    Simba hawana lolote acha waburuzwe

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    hahahahahaniwakatiwamabadiliko

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2012

    Simba walikuwa na mpango toka mwanzo wa kutoendelea na mashindano haya kwa sababu ya kupindishwa kanuni. Kwa jinsi walivyocheza ni wazi wamliamua kuishia hapa ila kwa namna ambayo CECAFA na TFF watapata message bila kuwa na namna ya kuwabana viongozi. Maamuzi haya ya viongozi hayakuwatendea haki Kocha, wachezaji wa wapenzi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2012

    Mnyama yanayojiri siku yake ya kuchinjwa.!!!

    Ni ile siku endapo wewe ni kiumbe 'mnyama' upo ndani ya zizi la Mfugaji wako huna hili wala lile ni asubuhi na mapema

    1.Mfugaji anakuja zizini anaangaza macho anachagua mnyama mmoja wapo,,,

    2.Mara ahhh unaona unakamatwa wenzio wanaachwa,,,

    3.Ahhh unaona kisu kinachomolewa,,,

    4.Ahhh dakika moja kisu kimeelekezwa kwenye koromeo lako....hayo ndio yaliyomkuta Simba SC.

    Mwishowe AZZAM 3 SIMBA 1

    Halafu naomba mnijuze, kama alivyofanya Azzam jana hivi ni kwa nini kila Mfugaji hupendelea kuchagua kuchinja mnyama (simba) aliyenona zaidi?

    Je waliokonda hawana nyama?

    Mjoma Michuzi naomba jibu tafadhali!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2012

    Ukiona manyoya usiulise!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2012

    vijana wa simba laini kweli

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2012

    Ahhh nimeshuhudia Azzam anatafuna finyango ya mnyama, na mimi nimepata uchu,,,,ahhh mchuzi mtamu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...