Katika harakati za kuimarisha zoezi la ukataji tiketi za treni ya abiria Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imetoa Mwongozo ufuatao:TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WATEJA WETU KWAMBA, KUANZIA JUMATATU JULAI 16, 2012 MTEJA YEYOTE ANAYETAKA KUNUNUA TIKETI YA TRENI LAZIMA AONESHE KITAMBULISHO CHAKE KWA KARANI MUUZA TIKETI BILA HIVYO HATUTAWEZA KUMHUDUMIA.
VITAMBULISHO VINAVYOTAMBULIKA NI VIFUATAVYO; KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA, LESENI MPYA YA UDEREVA, KITAMBULISHO CHA MUAJIRI, HATI YA KUSAFIRIA, KITAMBULISHO CHA SHULE, BARUA KUITOKA KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MITAA NAKADHALIKA UTARATIBU HUU MPYA NI KWA AJILI YA KUONGEZA UFANISI NA KUBORESHA HUDUMA ZETU KWA WATEJA WETU!
IMETOLEWA NA MENEJA UHUSIANO ( MIDLADJY MAEZ) KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU
DAR ES SALAAM
JULAI 16, 2012


mambo ya kupeana kula baada ya kupungua yanazidi
ReplyDelete"Nakadhalika" ni vitambulisho vya namna gani?? be clear bwana!neno hilo linaweza leta usumbufu kwa wale watakaoleta vitambulisho nje ya vilivyoorodheshwa kwenye tangazo.
ReplyDeletekwa hiyo kama huna kitambulisho chochote huwezi kusafiri na treni?,mbona nyie hamjaweka ule utaratibu wa kutowatoza abiria nauli zisizo na mpangilio? kazi ipo!
ReplyDeleteWhat??? Leseni yangu ya udereva inahusiana nini na mimi kusafiri na treni??? Leseni yangu itanisaidiaje kuniboreshea huduma katika usafiri wa treni??? Null hypothesis!
ReplyDeleteEti Dr. Mwakyembe, nini kinaendelea hapa kiongozi wetu?
Sijui mimi ndo sijaelewa hii kitu au waliofanya huu uamuzi hawakufikiria sana.Nadhani kitambulisho ni cha muhimu pale mtu anapokwenda kupanda garimoshi kwa sababu haiwezekani kuwa ati kila mtu anauwezo wa kwende TRL kukata ticket wengine ni vikongwe na wagonjwa na wengine wanakuwa ni wasafiri toka safari za mbali hivyo wanahitaji wanahitaji ticket in advance.
ReplyDeletemmmh, mie napita tu inaonekana hamtaki kufanya biashara nyie au karani anapewa madaraka zaidi.
ReplyDeleteMheshimiwa Zebedayo, mzalendo wa kuigwa..Inapendeza kuona treni za kisasa Tanzania zinadunda. Nashangaa yule jamaa aliyetoa mada kuwa watu walioko ugahibuni warudi kwa sababu Tanzania siku hizi mambo mswano. Kwa mtu niliyesafiri na treni miaka ya themanini na tisini, naona mabadiliko makubwa. enzi hizo mabehewa yalikuwa yamechakaa sana. sasa hivi treni nzuri, daraja la tatu la leo ni sawa na daraja la kwanza leo. Tunasonga mbele sana. Hakuna hata mwalimu wa shule ya msingi anayelalamika kuhjsu mshahara, wanapata pesa nzuri na wanaweza kumudu masiah bila shida. Kuna mpango sasa hivi kusitisha mikopo ya eelimu ya juu, kwani watu sasa wanaweza kuwalipia wanao bila shida. Nasikia hata benki ya nyumba inashida kupata wateja, itamkopesha nani wakati pesa nje nje Tanzania? Nadhani wabongo walio majuu inabidi watambue kuwa pesa iko nje nje, umeme tuna wa gesi, kinyesi cha ng'ombe, wa maporomoko, wa jua na jenereta..sasa shida ya umeme itoke wapi. hata dala dala watu hawapandi, wanatumia magari yao..bod boda hazina wateja, watu wa bajaji wameelekea Ulaya kutafuta soko jipy la wateja. Na huwezi kwenda Uwanja wa fisi siku hizi ukaogopo kuporwa, kule kuna mamilionea!!
ReplyDeleteZebedayo hupo?
Lengo ni kuzuia ulanguzi wa Tiketi kukatwa na wasiokuwa wasafiri.
ReplyDeleteKama ni hivyo, je idadi ya ukataji wa Tiketi ni vipi hapo?
Ingefaa uratibu utumie Komputa kwa kila mkataji Tiketi jina lake liingizwe ktk Komputa ili asiweze kurudia kukata Tiketi mara zaidi ya moja, ama kukatia Tiketi watu zaidi ya mmoja.
NAONA TRL HATWATAKI KUFANYA BIASHARA KWANI MTU AKINUUNUA TIKET ZOTE TRL WANAPATA HASARA GANI C NDIO FAIDA KWAO! WACHE BIASHARA YA ZAMANI WAJARIBU KUPUNGUZA URASIMU
ReplyDeleteMnaposema ulanguzi umekithiri halafu hakuna anayejitolea kutuonesha nani 'mlanguzi' hatua hii ya kumtaka msafiri ajitambulishe ni hatua moja, nyingine itafuata ndani ya treni ! Mkaguzi anaweza kukutaka uoneshe kitambulisho kuthibitisha kama unasafiri kwa tiketi halali..Hata kama umeuziwa kwa hila na Mtumishi wa TRL itabidi umtaje ili achukuliwe hatua stahiki..!Tunafahamu huduma zitakapoongezeka na kufikia 4 au zaidi kwa wiki suala la ulanguzi litakuwa limefikia tamati.Kwa sasa hii ni hatua mojawapo katika nyingi zinazopaswa kuchukuliwa ili kudhibiti watu wenye nia mbaya na kuendekeza ubinafsi wanaopenda kuwataabisha wananchi kwa kuwalangua tiketi za safari za treni kutoka Dar kwenda Kigoma na pia kuitoka Kigoma kuja Dar! Tunachoomba kutoka kwa Wateja wetu kuangalia hatua hii kwa mtizamo chanya na wasaidie kupiga vita ulanguzi wa tiketi za treni nchini popote pale walipo.! Ikiwezekana wananchi na wateja wetu wajitokeze katika vyombo vya dola kufichua mtandao wa walanguzi wa tiketi katika stesheni zetu kuu zikiwamo Dar, Morogoro, Ddoma, Tabora na Kigoma..! Tunawasihi Wananchi na Wateja kwa jumla mtuelewe nia ya hatua sio kuleta usumbufu bali kutangaza vita dhidi ya walanguzi Shime thushirikiane..ili tushinde vbuita hii ambapo tunasema 'Huduma ya usafiri wa reli bila Ulanguzi nchini INAWEZEKANA pindipo kila mtu mahala husika atatimiza wajibu wake! Midladjy Maez PRM- TRL
ReplyDeletehii haiwezi leta ufanisi wowote ila kuleta karaha na maudhi kwa wananchi...au ndio mpango mpya wa jamaa wa UASAMA/USALAMA wa taifa kuweza ku track watu wanaenda wapi?
ReplyDeletekama ilivyokuwa kusajili simu,hapo kuna program mpya ya sirikalikujua watu/nani anaenda wapi...shajua janja yao...
ReplyDeletemaoni yagu yamekaliwa. niliongelea kuhusu umuhimu wa kuwa na kibali/kitambulisho kwani hata wanaokata tiketi za ndege hawaulizwi vitambulisho. iweje usafiri wa ndani waulizwe id?
ReplyDeleteZebedayo nipo. na asante kwa kuninyoa kavu kavu,ubarikiwe ndugu.Ila kurudi bongo ni lazima ,maana huku siku hizi kuna vichwa tupu ,kama kina Magufuri, Mwakyembe,dogo janja nakadhalika. Please usiogope. Zebedayo.
ReplyDeleteKwa hili la vitambulisho bado sijaona kama litaondoa matatizo ya ulanguzi wa Tiketi hasa katika stesheni ya Kigoma, wakataji huwauuzia wafanyabishara wa nje na wao uziuza mara mbili ya bei ile ya halali, unataka nunua hutaki acha na ww ndio mwenye shida ya usafiri lazima utanunua!biashara hii inafanyika toka kitambo!kwa hili Mwakiyembe ujishike.
ReplyDelete