Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu alitembelea Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi ulioko wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kujionea uharibifu wa mazingira unaofanywa na kikundi cha watu wanaotaka kujitwalia maeneo ndani ya msitu kuanzisha makazi yao.

akizungumza baada ya kujionea uharibifu huo na kukagua mipaka kama inavyoelekezwa na Tamko la Serikali no 306 la Septemba 1954 ambalo lilianzisha rasmi msitu huo wa hifadhi kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani na vizazi vijavyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akipitia ramani ya eneo hilo la Msitu wa Kazimzumbwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akipatiwa maelezo na Mmoja wa viongozi wa Wilaya ya Kisarawe juu ya Msitu wa Kazimzumbwi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2012

    mbona hakuna msitu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2012

    Mhe Nyalandu, angalieni pia wajibu wa serikali za vijiji na halmashauri yake (kijiji). Mkitaka ninyi ndiyo mje kutokea taifani kulinda maeneo ambayo yako chini ya Halmashauri za Wilaya, ambako yupo hata DNRO, basi mtakuwa mnakuta hali kama hiyo. Wapeni serikali za vijiji, na halmashauri za Wilaya husika, nafasi ya kuwajibika. Ndiyo maana tulizichagua serikali hizo ati!
    Mzoefu wa uongozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...