Kwa niaba ya watanzania tunaoishi nje ya nchi, tumepokea kwa masikitiko tarifa za ajali ya meli ya abiria na mizigo MV SKAGIT iloyotokea July 18,2012 na kupoteza maisha ya watanzania wenzetu.

Ajali hiyo mbaya ilitokea karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar na kusababisha vifo, majeraha, watu kupotea na kupoteza mali zao.

Watanzania tuishio nje ya nchi tunaungana na familia za watanzania wenzetu waliotharika na ajali hii katika kipindi hiki kigumu.

Vile vile, tunatoa pongezi kwa serikali ya Jamhuri ya muungano na serikali ya Zanzibar, jeshi la ulinzi na usalama na mamlaka ya usafiri wa baharini katika jitihada za uokoaji wa abiria na kutafuta mili ya ndugu zetu hawa baharini usiku na mchana.

Katika kipindi hiki kigumu, sisi watanzania tuishio nje ya nchi tunaungana na familia zilizo athirika na ajali hii mbaya ya meli.

Tunamuomba mwenyezi mungu azilaze roho hizi za marehemu peponi na kuwapa unafuu wa haraka wale wote waliopatwa na majeraha katika ajali hii.

Amin

Yacob Kinyemi
Katibu wa tawi CCM
Washington,DC ( DMV)
Marekani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...